Dhambi adui mkubwa wa Imani,Ujasiri na Mamalaka

http://touchyaneighbor.files.wordpress.com/2011/05/sin12.jpg?resize=533%2C180HAKUNA ADUI MKUBWA wa IMANI, UJASIRI na MAMLAKA kama DHAMBI… Dhambi inakuvua mavazi ya WOKOVU, HAKI, SIFA na NEEMA… Badala ya Mungu kuwa BABA wa karibu na RAFIKI wa kumkimbilia na kumfurahia, anaonekana kama ADUI na MHUKUMU wako… Badala ya FURAHA, AMANI na UHAKIKA, DHAMBI inaleta HUZUNI, MASHAKA, WOGA na HOFU… Badala ya kumsogelea SHETANI kwa UJASIRI na JEURI YA KIFALME na kumgusa machoni,

Unaanza KUKIMBIA HATA KIVULI CHAKO…Hata paka au bundi akilia nje ya nyumba yako UNAANZA kumwona SHETANI NA JESHI LAKE wakija kukumaliza… DHAMBI ZOTE zina RADHA NZURI na zinaonekana kama zinalipa au zina faida kwa muda ule mchache wa kuzifanya, NGOJA UMALIZE ndipo utakapojua DHAMBI INAVYOUMIZA NA KULEMEA KULIKO MZIGO MWINGINE WOWOTE…AMNONI alipombaka dadake TAMALI alifurahia kwa dakika kadhaa kukaa mapajani mwake [KAMA WEWE DADA/ KAKA MZINZI UNAYEDHANI KUBADILI WANAWAKE/WANAUME NI FAHARI] lakini alipomaliza ALIMCHUKIA KWA MACHUKIO MAKUU MNO… Wakati YUDA ISKARIOTI anakusanya vipande 30 vya FEDHA [KAMA WEWE MFANYAKAZI WA UMMA UNAYEPOKEA NA KUTOA RUSHWA HALAFU UNASEMA SIKUWA NA JINSI HATA MUNGU ANAJUA] alipomaliza kumuuza Yesu hakufaidi hata ile hela aliishia KUJINYONGA… Petro alipomkana YESU mara 3 hakuona kuwa ni issue sana lakini JOGOO alipowika mara ya 3 aliangua kilio kama mtoto mdogo kwa uchungu[Kama wewe unavyomkana Yesu na Imani yako kama mwanafunzi wa Yesu kwa ajili ya kupata manufaa mawili matatu lakini mwisho wa siku unaishia kuumia, kulia na kukosa amani na furaha ya maisha pale SHETANI ANAPOANZA KUKUSHITAKI NA KUULIZIA JUU YA UKRISTO WAKO]…DHAMBI NI MBAYA…Itakupeleka umbali ambao hukutaka kwenda…Itakufanya ulipe gharama ambazo hukuwa umejiandaa nazo!
UKIONA MTU ANATESWA NA MAPEPO, WACHAWI, MIZIMU, SHETANI, MAGONJWA, KUJITUMA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII SANA ILA ANAISHIA KUPATA MATOKEO YA CHINI AU HAKUNA…UWE NA UHAKIKA MAISHA YAKE SI MATAKATIFU…KUNA MIFEREJI YA DHAMBI MAISHANI MWAKE NA YEYE AMEIKUMBATIA… HATA KAMA ANANENA KWA LUGHA ZA WANADAMU NA ZA MALAIKA…PALIPO NA MZOGA NDIPO WAKUSANYIKAPO TAI… PALIPO NA MAVI NDIPO WAKUSANYIKAPO NZI… PALIPO NA MAUA NDIPO WAKUSANYIKAPO NYUKI!
“ATENDAYE DHAMBI NI WA IBILISI KWA MAANA YEYE HUTENDA DHAMBI TANGU MWANZO”
“YEYE MWENYEWE[YESU] ALICHUKUA DHAMBI ZETU MWILINI MWAKE JUU YA MTI, ILI TUKIWA HAI KWA MAMBO YA HAKI, TUWE WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI”
“ALIYEZALIWA NA MUNGU HATENDI DHAMBI MAANA UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE”
“AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA,BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA ATAPATA REHEMA”
“TUKIZIUNGAMA DHAMBI ZETU, YEYE NI MWAMINIFU NA WA HAKI HATA ATUONDOLEA DHAMBI ZETU NA KUTUSAFISHA UDHALIMU WETU WOTE”
(Hakikisha una-SHARE ujumbe huu kadiri uwezavyo kwa utukufu wa Mungu au Post kwenye wall yako)!
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »