FUNGUKA

Utajiri/Umasikini ni juu yako
Utajiri/Umasikini ni juu yako

Biblia Inasema, “Yesu Kristo Kwa Neema Yake, ALIFANYIKA MASIKINI Ili Sisi (WALIOOKOLEWA) Kupitia UMASIKINI WAKE Tupate Kufanyika MATAJIRI” (2Wakorintho 8:9).
SASA
Nilipokuwa Nasoma Habari Za Kuzaliwa Kwa Yesu, Nikakutana Na Wale MAMAJUSI Ambao Siku Ya BIRTHDAY Yake Walimletea DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE.
Halafu Nikawaza, Ikiwa “MASIKINI-YESU” Alipewa Vyote Hivyo Kama Zawadi Ya Birthday, Je Sisi ALIOTUTENGENEZEA UTAJIRI Kwa Umasikini Wake TUTAKUWAJE??

Ukiamua Kuwa Masikini Umeamua, Kwenye Msalaba Wa Yesu Umasikini Umeshughulikiwa Kama Ilivyokuwa Kwa DHAMBI, SHETANI NA MAGONWA… Damu Iliyokomesha Utemi Wa Dhambi Ni Hiyohiyo Imemaliza Utawala Wa Umasikini… Lakini Ili Hayo Yatokee Kwako Unapaswa Kujifungua Kwenye MAFUNDISHO YALE ULIYOPOKEA “KULE” Yanayokufanya Kuwa Mkristo ASIYE NA BALANCE… Yale Mafundisho Ya “UTAJIRI NI MBAYA UTAKUFANYA USIINGIE MBINGUNI”… MAFUNDISHO MANYONGE!!
Amka Wewe Usinziaye,
Jaa Yesu, Fikiri Kwa Upeo Na Akili Ya Kifalme Na Kikuhani, Halafu Utakuwa MTAKATIFU SANA NA MKAMILIFU KULIKO AYUBU NA BADO UTAKUWA TAJIRI SANA KAMA IBRAHIMU: Katika FEDHA, DHAHABU NA MIFUGO (Mwanzo 13:1-2).
WOKOVU WA KUOMBA OMBA SI WA BIBLIA NINAYOSOMA MIMI.
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »