1. Uthibitisho pekee kwamba unaamini kitu fulani au jambo Fulani ni pale unapotenda. Pasipo na utendaji hapana Imani.
2. Unaweza kusikia jumbe nzuri zenye kuhamasisha na kusisimua, lakini utakiishi kile ulichokiamini tu na sio ulichokisikia.
3. Tunasikia Mengi, tunajifunza mengi, lakini wengi hatuna muda wa kuyachakata yajenge imani ndani yetu. Kwa hiyo tuna maarifa bila Imani, hivyo tunakosa matokeo.
4. Mwenye haki anaishi kwa imani yake. Utaishi na kutenda kulingana na kiwango cha imani yako. Lile usiloliamini huwezi kulitimiza.
5. Nini unaamini? Itakuwa kwako kulingana na imani yako. Bila imani, maarifa yote unayopata yataishia kuwa kibirudisho tu.
IMANI YAKO, MAISHA YAKO!
_For Me, My Future & My World!_
Bro. Emmanuel Mahenge
0714 530 295
emmastiv@yahoo.co.uk
HII NAYO YA MUHIMU SANA KWA YULE UNAYEJIANDAA KUWA MME/MKE WAKE!
Luka 1:5 inasema kitu kuhusu Kuhani Zekaria, na Mke wake Elisabeth…na kuna mambo kadhaa ya kujifunza; 1.Zekaria alikuwa kuhani, lakini Elizabeth alikuwa wa Kabila la