HEKIMA YA LEO [07-04-2017]


ILI KUWEKEZA VIZURI MAISHA YAKO (5)
5. Jiongezee Uwezo
Utawekeza vizuri maisha yako kama utawekeza vizuri ndani yako. Ubora wa utu wako wa ndani utaamua ubora wa maisha yako.
Wekeza maarifa na ufahamu ndani yako, vitafungua macho yako na kukufanya uone maisha kwa sura ya tofauti.
Utaweza kutimiza mambo katika maisha kulingana na uwezo ulionao. Uwezo wa kiakili, uwezo wa kupambanua mambo, na uwezo wa kufanya mambo (ujuzi)
Kila siku una nafasi ya kujiongeza na kujiboresha, Hakuna mwisho wa ukuaji, unaweza kuendelea kukua kwa kadiri unavyotaka.
Utakuwa wa faida duniani kulingana na uwezo ulionao. Ongeza thamani yako kwa kujiongezea ujuzi, maarifa na uwezo.