HUWEZI KUWA BORA MAISHANI MWAKO ZAIDI YA VILE UNAVYOJIONA NAFSINI MWAKO;

 

Kiwango Cha Maisha Utakayoishi Na Kuyafurahia Au Kuyachukia Hapa Duniani Kinategemea Kiwango Cha Vile UJIONAVYO NAFSINI MWAKO…MAANA VILE UJIONAVYO NAFSINI MWAKO, NDIVYO WEWE ULIVYO NA NDIVYO UTAKAVYOKUWA…”AJIONAVYO NAFSINI MWAKE [NDANI YAKE] NDIVYO ALIVYO” (Mithali 23:7).
Tuone Mifano Ya Watu Kadhaa Kwenye Biblia;
1.Yusufu ALIJIONA NAFSINI MWAKE Kuwa Ni Mtawala Mkuu Ambaye Watu Wote Wakiwemo NDUGU ZAKE NA WAZAZI WAKE Watamsujudia. Na HAKUKUBALI Kupoteza Hiyo PICHA NA UHALISI Wake Hata Ndugu Zake Walipotaka KUMUUA, Walipomtupa SHIMONI, Walipomuuza Kwa Wafanyabiashara Wa KIISHMAELI, Alipouzwa NYUMBANI KWA POTIFA, Alipotakiwa Na Kushawishiwa KIMAPENZI Na Mke Wa Potifa, Alipotupwa Gerezani Kwa Uongo Wa Mke Wa Potifa. HAKUPOTEZA PICHA YAKE YA VILE AJIONAVYO NAFSINI [NDANI YAKE] MWISHO AKAWA WAZIRI MKUU MISRI!
2.Nimrodi Na Wenzake Waliokuwa Wakijenga MNARA WA BABELI WALIJIONA NAFSINI MWAO Kuwa Wanaweza Kujenga Mnara Wa Kufika Mbinguni… Wakaanza Kujenga Kwa UHAKIKA NA PASIPO SHAKA…Mungu AKAGUNDUA KUWA NDIVYO WAONAVYO NAFSINI MWAO, Akasema, “WATU HAWA HILI WALILOAMUA HAKUNA AWEZAYE KUWAZUIA…” Ikabidi Ashuke Kuwachafulia Lugha!
Watu Wa Babeli Walivyojiona Nafsini Mwao Ndivyo Ambavyo Walielekea Kuwa Mpaka Pale Mungu Alipoona Kuwa LAZIMA WATAFIKIA LENGO LAO Akaamua Kuja Kupangua Hilo Maana Yeye Alitaka Wao Wasambae Juu Ya Nchi Na Kuijaza Ila Wao Walitaka Wajikusanye Sehemu Moja Ili Wasitawanyike. Walikuwa Kinyume Na Mungu Hicho Pekee Ndicho Kilimfanya Mungu AWAPINGE. Japo Mungu Mwenyewe Alikiri Wazi Kuwa Hilo Lililokuwa NDANI YAO LINGEFANIKIWA Kama Wasiposhuka Na Kuwachafulia Lugha.

3.WAPELELEZI 10 Waliorudi Na Ripoti Mbaya Kwa Musa Na Waisraeli, Wao Waliona UZURI WA NCHI YA AHADI; Kuwa Kuna MAZIWA NA ASALI…Tena Wakaja Na Baadhi Ya Mazao Ya Nchi Kama Uthibitisho, Lakini NAFSINI MWAO [NDANI YAO] WALIONA WAO NI MAPANZI NA HAWAWEZI KUIMILKI ILE NCHI MAANA INA MAJITU, NA YA KUWA NCHI ILE INAWALA WATU WAKE… Hii Picha Waliyokuwa Nayo ILIAMUA Kiwango Cha Maisha Yao. Wote Walikufa JANGWANI, Hawakuweza KUINGIA NCHI YA AHADI Sawa Na Wao Walivyoona.
Joshua Na Kalebu Wao Walikuja Na Ripoti NJEMA; Waliyaona MAJITU KAMA CHAKULA, NA WALIONA KUWA LAZIMA WAIRITHI NCHI YA AHADI, NCHI YA MAZIWA NA ASALI, NA HAKIKA WALIIRITHI, MAANA VILE WALIVYOONA NAFSINI MWAO [NDANI YAO] NDIVYO WALIVYOKUWA HAKIKA!
4.Masikini Lazaro, Alikuwa Akiishi Kwa Kula MAKOMBO Chini Ya Meza Ya TAJIRI… NDANI YAKE ALIJIONA YEYE NI SAWA NA MBWA, AKAWA ANAGOMBEA MAKOMBO CHINI YA MEZA YA TAJIRI. Na Hakika Hakuwa Na Maisha Bora Au Ya Maana Zaidi Ya Kiwango Hicho Alichojiona Nafsini Mwake.
ALIKUFA AKIWA MASIKINI CHOKA MBAYA; Sawa Na Picha Yake Ya Kujiona Sawa Na Mbwa Na Kugombea Chakula Chini Ya Meza Na Hao Mbwa!
NAMNA YA KUKUZA PICHA [MTAZAMO WA WEWE NI NANI] NDANI YAKO;
Kuna Njia Moja Kuu Ya Kukuza KIWANGO CHA PICHA YA VILE UJIONAVYO NAFSINI MWAKO, NA NJIA HIYO NI KWA WEWE KULISOMA NENO LA MUNGU, KULISIKIA SANA NENO LA MUNGU, KULIAMINI ZAIDI YA UNAVYOAMINI AKILI ZAKO NA UFAHAMU WAKO, KULIJAZA MOYONI MWAKO, KUANZA KUWAZA, KUTENDA, KUONGEA NA KUISHI SAWA NA NENO LA MUNGU, HATA KAM MAZINGIRA YAKO AU HALI YAKO INASEMA KINYUME NA WEWE… NENO LA MUNGU NI NDOTO YA MUNGU, NENO LA MUNGU NI AKILI YA MUNGU, NENO LA MUNGU NI HEKIMA NA UFAHAMU WA MUNGU, NENO LA MUNGU NI MAWAZO YA MUNGU Ambayo Yako Juu Sana Kuliko Mawazo Ya Mwanadamu Wa Kawaida Kama Vile Mbingu Zilivyo Juu Sana Ya Nchi (Isaya 55:8)… JINSI UNAVYOBOBEA KWENYE NENO LA MUNGU, NDIVYO AMBAVYO UNAANZA KUYAWEKA MAISHA YAKO KWENYE MSTARI WA NENO LA MUNGU [MAWAZO YAKE, PICHA YAKE, NDOTO YAKE, MTAZAMO WAKE Nk]. Na Kama UKIZIAMINI NA KUZIISHI AHADI ZA MUNGU, UKAZINGOJA HATA ZIJAPOKAWIA MAANA HAZITASEMA UONGO, BAADA YA MUDA KIDOGO ZITAKUWA HALISI KWAKO!
Mungu Akupe Neema Ili Baada Ya Miaka 5, 10 Ijayo Tukutane Ukiwa Na Ushuhuda Wa Mabadiliko Na Maisha Ya Maana Na Thamani… UJIONAVYO NAFSINI MWAKO; NDIVYO ULIVYO NA PIA NDIVYO UTAKAVYOKUWA Kama Hautachukua Ahadi Za Mungu Na Kuziishi!
Mwl D.C.K

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »