Je kuna Dhambi ilikuwa inakutesa kwa siri :…..

: NA UNAHANGAIKA KUJIKWAMUA BILA MAFANIKIO??? UJUMBE HUU NI WAKO…

Dhambi Yoyote Ambayo UTAIFICHA Na Kutofanya BIDII [Kwenye Maombi Na Kufunga] Na Kumweleza ROHO MTAKATIFU Akusaidie KUJINASUA, Hakika ITAKUANGUSHA!
Wakristo Wengi WANAANGUKA DHAMBINI Na Kuacha MINONG’ONO MINGI NYUMA YAO Kwa Sababu WANAFUGA DHAMBI NDANI YAO Halafu Inafikia Wakati Ile DHAMBI INAZAA MAUTI [ANGUKO] Ambalo LINATIA AIBU ZAIDI NA LINA GHARAMA KUBWA Kuliko Gharama Ya Kwenda Kwa YESU AKUTUE HUO MZIGO NA KUMTWIKA HIYO FEDHEHA YAKO!
Biblia Inasema, “HATUJAFANYA VITA NA DHAMBI KIASI CHA KUMWAGA DAMU”…. Kama Kweli UMEDHAMIRIA KUWA MTAKATIFU NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, Hakikisha UNAFANYA VITA NA DHAMBI Inayokutesa Na Kukusumbua KWENYE MAOMBI Ukimsihi ROHO MTAKATIFU AKUPE NGUVU YA KUJIKWAMUA!
Yafuatayo Ni Mambo Yatakayokusaidia Kujinasua Kutoka Kwenye Dhambi Yoyote Inayokutesa:

1.USIIFICHE DHAMBI YAKO MBELE ZA MUNGU:

Mweleze Mungu Waziwazi [Kweney Maombi] Kwamba Unateswa Na Dhambi Fulani, Na Hauna Nguvu Yako Binafsi Ya Kujinasua
Wakristo Wengi Wanateswa Na Dhambi Kwakuwa HAWAKIRI DHAMBI NA MADHAIFU YAO MBELE ZA ROHO MTAKATIFU AMBAYE NI “MSAIDIZI” MWENYE NGUVU YA KUTUNASUA.
Biblia Inasema, “AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA, BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA ATAPATA REHEMA” (Mithali 28:13).

2.AMINI NA KUBALI KWAMBA YESU HAKUFA KWA AJILI YA MSAMAHA WA DHAMBI TU, BALI ALIKUFA ILI AIHARIBU DHAMBI NA NGUVU YAKE INAYOKUTESA:

Wakristo Wengi Wanadhani Na Kuamini Kwamba YESU KRISTO Alikufa Ili Atupe MSAMAHA WA DHAMBI Na Pia Atupe UWEZO WA KUTUBU NA KUSAMEHEWA TENA ENDAPO TUTAKOSEA AU KUTENDA DHAMBI BAADA YA KUOKOKA… Hii Ni Sahihi Lakini Si Sahihi Sana!
YESU Amefanya Hayo Yote NDIYO Lakini Pia Amefanya Kitu Kikubwa Zaidi Ya Hicho, AMEUVUNJA UTI WA MGONGO NA UBONGO WA DHAMBI… Yesu AMEISHAMBULIA NA KUIANGUSHA DHAMBI… AMEISHINDA DHAMBI NA KUIPANGUA JUMLA KWA AJILI YETU Ili “TUKIWA HAI KWA MAMBO YA HAKI TUWE WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI” (1Petro 2:24).
Biblia Inasema KUPITIA KRISTO YESU “TUMEIFIA DHAMBI NA KUUVUA UTU WA DHAMBI NA KUVAA UTU MPYA KWA KUFUFUKA KWAKE, ILI TUSIITUMIKIE DHAMBI TENA” (Warumi 6:4-6).
Bila KUAMINI KWAMBA “YESU ALIIVUNJA NGUVU YA DHAMBI NA KUIHARIBU” Hakika HAUTAWEZA “KUTEMBEA NJE YA UKANDA WA DHAMBI [SIN ZONE]”
Biblia Inasema, “YESU ALIDHIHIRISHWA ILI AZIONDOE DHAMBI [ZISIWEPO TENA]” (1Yohana 3:4-5).
BADILI MTAZAMO WAKO: “YESU ALIIVINJA NGUVU YA DHAMBI NA KUPATA SULUHISHO LA KUDUMU KUHUSU SWALA LA DHAMBI” Ukiamini Na KULIPOKEA MOYONI HILI, Na Kisha KULIOMBEA KWA MZIGO KWENYE MAOMBI YAKO, UTASHANGAA DHAMBI IMEPOTEZA NGUVU NA UTAWALA JUU YAKO NA NDANI YAKO!

3.NENO LA MUNGU LINA UWEZO WA KUKUFANYA KUWA MTAKATIFU NA KUZUIA USITENDE DHAMBI TENA; LISOME NA KULIAMINI, LITUMIE KAMA “STANDARD YA MAISHA YAKO” HALAFU DHAMBI ITAKUWA HISTORIA

“Na ya kuwa tangu utoto UMEYAJUA MAANDIKO MATAKATIFU, ambayo YAWEZA KUKUHEKIMISHA [KUKUFANYA MWENYE HEKIMA] HATA UPATE WOKOVU KWA IMANI ILIYO KATIKA KRISTO YESU… KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU [Lililovuviwa na ROHO MTAKATIFU] Lafaa KWA MAFUNDISHO, NA KWA KUWAONAYA WATU MAKOSA YAO, NA KUWAONGOZA, NA KWA KUWAADABISHA KATIKA HAKI ILI MTU WA MUNGU AWE KAMILI [PERFECT] AMEKAMILISHWA KA KILA TENDO JEMA” (2Timotheo 3:15-17).
Hii Mistari Hapo Juu Innaonyesha Waziwazi NGUVU NA UWEZO WA MUNGU WA KUMTOA MTU DHAMBINI NA NGUVU YA DHAMBI Kupitia MAANDIKO MATAKATIFU Pale ROHO MTAKATIFU Anapopewa NAFASI YA KUYAPA UHAI [PUMZI YA MUNGU]!

Lakini Pia Daudi Anatufundisha SIRI YA KUISHINDA DHAMBI, Naye Anatuambia NAMNA YA KUFANYA:
“MOYONI MWANGU NIMELIWEKA NENO LAKO ILI NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI” (Zaburi 119:11).
Unapoweka UAMUZI Wa Kulisoma NENO Na Kuliweka nafsini mwako [kwenye AKILI NA KUMBUKUMBU YAKO] Kisha Ukapata MUD WA KULITAFAKARI KWA IMANI NA SHAUKU, Litaingia MOYONI MWAKO Na Kukujengea MFUMO WA MAISHA MATAKATIFU Unaokataa Na Kupinga KILA NAMNA YA UASI NA UOVU.

Ukiufanyia Kazi Ujumbe Huu UTAJINASUA TOKA KWENYE DHAMBI YOYOTE, TABIA YA SIRINI INAYOKUTESA, Ila Usipoifanyia kazi Utaishia kusema WOKOVU NI MGUMU NA UTAKATIFU NI KAZI NGUMU… Weka Kwenye Matendo na UTAVUKA HAKIKA!!!

Salamu Toka Tabora,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »