JIFUNZE KUWEKA NA KUWEKEZA AKIBA

Akiba

; USILE KILA KITU UPATAPO TOKA KWA BWANA!
Kosa Kubwa Wanalofanya Wana Wa Mungu, Hasa Wale Waliookoka, Wanaoishi Kwa Imani, Ni Kutojua Kuwa Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Ndani Ya Muda Maalumu, Na Hurudi Kutupa Tena Baada Ya Muda, Na Sio Kwamba Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Kila Siku… Hii Naizungumzia Kwenye Maeneo Ya Mahitaji Yetu Ya Kifedha, Chakula, Vyakula, Mavazi Nk… Mungu Anapokupa Kitu, Mahitaji Yako, Huwa Anakupa NA ZIADA, Hakupi Kipimo Cha Kula Au Kutumia Muda Ule Tu… Huwa Anatoa NA CHA ZIADA AU NYONGEZA JUU… Lengo Kubwa La Mungu Kukupa KITU CHA ZAIDI AU ZIADA Ni Ili Akusaidie Kwenye KESHO YAKO (Future)… Narudia Tena, Mungu Huwa Anatupa Na Ziada, Lengo Lake Kubwa Ni Kufidia MUDA ULIOPO KATIKATI HAPA Kati Ya Pale Alipokupa Hadi Pale Atakaporudi Tena Kukupatia Tena!
NDIO MAANA Mungu Anatufundisha Habari Za Chungu, Wasio Na Msimamizi Wala Kiongozi Ambao Wakati Wa MAVUNO Hawali Chakula Chote Bali HUJIWEKEA AKIBA Inayowasaidia Wakati Wa UKAME NA NJAA… Lakini Pia Mara Nyingi Kwenye NENO LAKE, Mungu Amezungumza Kuhusu GHALA… Ambayo Ni Sehemu Ya Kuhifadhia Au Kutunzia MAVUNO/ ULICHOPATA Kwa Ajili Ya KESHO YAKO… Pia Mungu Mara Nyingi Amesema Kuhusu HAZINA… Inayomaanisha SHEHENA ILIYOHIFADHIWA Kwa Ajili Ya MATUMIZI YA BAADAYE… Na Mara Nyingi Mungu Anapokuja KUTUBARIKI, Huwa Analenga HAZINA NA GHALA ZETU… Utamsikia Akisema, “Nipate KUZIJAZA HAZINA NA GHALA ZENU” (Malaki 3:7-11).
Lakini Hata Yesu Mwenyewe Alijua Kanuni Hii Na Aliitendea Kazi… Hata Wakati Alipowalisha Wale Wanaume 5000, Wanawake Wengi Na Watoto, BADO YEYE NA TIMU YAKE WALIKUSANYA CHAKULA KILICHOBAKI (Marko 6:42-43, Yohana 6:12-13)
YESU Alikuwa Na Uelewa Wa Kutosha Kuhusu Mungu, Baba Yake Ya Kuwa Huwa Anatoa ZIADA, Lakini Usipoitunza Na KUTUMIA KILA ULICHOPATA, BILA KUWEKA AKIBA, Kuna Muda Unakuja Ambao Utakuwa Na Uhitaji Na Hata Ukimlilia Na Kumwita Mungu, HATAKUJIBU AU KUKUPA Kingine Mpaka Muda Ule Aliopanga Utakapofika!
Mungu Anapokufungulia MLANGO Wa Kupata MSHAHARA, Au Kipato Kizuri Kwenye Biashara Au Shughuli Zako Za Uzalishaji, USITUMIE KILA ULICHOPATA… JIWEKEE AKIBA… WEKA GHALANI Kwa Ajili Ya Kesho Yako Au Itumie Ile Ziada Kwa Ajili Ya KUZALISHA FAIDA ZAIDI [WEKEZA ILE ZIADA] Kwenye shughuli Au Jambo Litakalokupa Zaidi Ya Ile Na Kukuvusha Kipindi Cha UGUMU Kitakapokuja!
Jifunze Kuweka Akiba… Lakini Mara Baada Ya Kupata Hiyo Akiba, Iwekeze Mahali Ambapo Unaweza Kuiongeza Ili Uwe SALAMA Wakati Wenzako Watakopokuwa WANALIA NJAA NA UHITAJI!

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »