MFUNGO WA SIKU 10 WA MWISHO WA MWEZI. [SIKU YA NNE]

 

NGUVU YA KUTAMKA VITU VIKATUKIA/ VIKAWA (THE POWER TO SPEAK THINGS INTO EXISTENCE).

Maandiko:

“MUNGU AKASEMA iwe nuru; IKAWA NURU…. MUNGU AKASEMA, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga (KWA MANENO YAKE), akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; IKAWA HIVYO… MUNGU AKASEMA, maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; IKAWA HIVYO….”
(Mwanzo 1:3-15).

“Basi Eliya Mtshibi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ILA KWA NENO LANGU”
(1Wafalme 17:1).

“Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala HAKULIACHA NENO LAKE LOLOTE LIANGUKE CHINI”
(1Samweli 3:19).

“Nawe UTAKUSUDIA NENO, NALO LITATHIBITIKA KWAKO; Na mwanga utaziangazia njia zako”
(Ayubu 22:28).

“NILITHIBITISHAYE NENO LA MTUMISHI WANGU, NA KUYAFIKILIZA MASHAURI YA WAJUMBE WANGU….”
(Isaya 44:26).

“Mimi (Mungu) NAYAUMBA MATUNDA YA MIDOMO…”
(Isaya 57:19).

MAMBO YA KUJIFUNZA

1. Kuna watu wenye maarifa ambao wamejua siri hii, kile wanachokitamka kinatokea na dunia inawashangaa!

2. Huu ni urithi wa Wana wa Mungu na watumishi wa Mungu na kila mmoja anapaswa kutembea katika nguvu hii (Isaya 54:17, Isaya 44:26)

3. Ni silaha ya kipekee aliyotoa Mungu, itakayotutofautisha na wanadamu wengine walio nje ya Ufalme wa Mungu (Mathayo 16:18-19).

4. Si jambo la ajabu kwa Mwana wa Mungu kufanya kama Baba yake, kuyasema mambo na yakatukia… Mtoto wa mbwa ni mbwa na Mwana wa Mungu ni muungu (Zaburi 82:6, 1Yohana 5:4).

5. Nguvu hii si ya baadhi ya watu, ni ya kila mwana wa Ufalme, lakini ni wachache tumeijua na tunaifaidi (Ayubu 22:28)… Chukua fursa twende zetu!

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UTEMBEE KATIKA NGUVU YA KUTAMKA MAMBO YAKATUKIA!

1. SURA NA MFANO WA MUNGU.

Kila mwanadamu amebeba sura na mfano wa Mungu alioumbwa nao (Mwanzo 1:26-27, Mwanzo 5:1-2).

Mungu ametupa asili yake na utambulisho wake ili tuishi na kufanya kile ambacho Yeye anafanya.

Mungu hutamka vitu na vikawa vilevile kama alivyotamka na sawa na picha aliyonayo ndani yake!
(Mwanzo 1:3-15).
Kwa kutupa sura na mfano wake, ametupa kinachomfanya aseme vitu vitokee, nasi tunaweza kusema na vikatukia bila shaka!
UKIJUA HII UTAJUA THAMANI YAKO HALISI, NA HAUTAACHA GIZA, UTUPU NA UKIWA VITAWALE MAISHA YAKO… UTATAMKA KILE UNACHOTAKA KUKIONA!

2. ROHO MTAKATIFU (UWEPO WA MUNGU).

Ukisoma kitabu cha Mwanzo utaona Mungu hakuanza kutamka chochote mpaka alipohakikisha Roho Mtakatifu yupo juu ya uso wa maji!

Yesu hakutangaza kuhusu vipofu kuona, waliofungwa kufunguliwa, habari njema kwa masikini na mengine mengi mpaka alipohakikisha ROHO WA BWANA YU JUU YAKE (Luka 4:18-19)!

Petro hakuanza kuhubiri (kutamka) mpaka pale Roho wa Mungu alipokuja juu yake, na WATU ELFU TATU WAKAAMINI WOKOVU (Matendo 2 yote)!

Habari njema kwetu watu wa agano jipya, TUNA ROHO MTAKATIFU MUDA WOTE…. Ni suala la kumuamsha ndani yako kwa wimbo wa sifa, mahubiri au mafundisho ya motomoto, halafu ukishachaji ANZA KUTAMKA VITU KATIKA UWEPO ULE WA MUNGU, HALAFU ROHO MTAKATIFU ATAVITHIBITISHA!
(Isaya 44:26, Isaya 57:19, 1Samweli 3:19).
KILA SIKU ISHI MAISHA AMBAYO UWEPO WA MUNGU UKO NAWE, NA HII ITAWEZEKANA ENDAPO;

I)Utakuwa mtu wa maombi walau mara tatu kwa siku (asubuhi, mchana, jioni/usiku)!
Mara kwa mara una ushirika na Mungu kupitia maombi.
Hata ukiwa ofisini, moyoni unanena kwa lugha au kumsifu na kumuabudu Mungu moyoni.

ii) Kuwa na ratiba inayoeleweka ya usomaji Neno la Mungu na kusikiliza na kutazama video za mafundisho ya watumishi wa Mungu wenye moto!
Uungu ulionao ndani yako unahitaji KUCHAJIWA MARA KWA MARA kama kweli unahitaji kuona ubora wa juu wa Maneno yako na mamlaka uliyobeba!

iii) Uwe rafiki wa kudumu wa mifungo.
Watu wa mifungo ni watu wa nguvu.
Mifungo huwa inapasua mwili na kufanya nguvu aliyobeba mtu kutoka nje kufanya miujiza mikubwa!
Ukiwa mtu wa kula wiki nzima, utakuwa pia mtu asiyeweza kusema vitu vikatokea!

iv) Epuka kusikiliza na kutazama vitu visivyokuza imani yako.

Hapa siongelei vyenye dhambi tu, hapana!
Chochote ambacho kinalisha hisia zako badala ya imani yako, hakifai kukitazama au kukisikia.
Movies, tamthilia, series, miziki, talk shaws, zinaweza zisiwe dhambi, lakini najua hakika HAZIKUZI IMANI WALA HAZIONGEZI UPAKO.
Yesu alisema, “Jicho lako ni taa ya mwili wako. JICHO LIKIWA SAFI NA MWILI WOTE UNAKUWA SAFI”
Usafi wa jicho unategemea unalipa kuangalia visafi au vichafu.
Uamuzi ni wako.
KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SI KITU LELEMAMA, LAZIMA UKUBALI KUVIACHA VINGI WAPENDAVYO WANADAMU NA UWEKEZE KWENYE UWEPO WA MUNGU!

3) NAFASI YA UFALME TULIYOPEWA.

“…Wastahili mwanakondoo wa Mungu uliyechinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu, watu wa kila lugha, kabila, jamaa na taifa, na UKAWAFANYA KUWA WAFALME NA MAKUHANI kwa Mungu wetu, NAO WANAMILKI JUU YA NCHI”
(Ufunuo 5:9-10).
“…Kwa maana neno la Mfalme lina nguvu…”
(Mhubiri 8:4).
Wafalme hutawala kwa maneno yao!
Kile watamkacho ndicho huthibitika hata kama wamekosea.
Mfalme Herode kwa furaha iliyopitiliza alimwambia binti wa Herodia kuwa atampa chochote, na hata aliposema NIPE KICHWA CHA YOHANA MBATIZAJI, ilibidi AKIKATE maana kwa maneno yake alishasema atampa chochote… Japo alimpenda Yohana lakini alilazimika kutenda neno lake kama Mfalme!
Mfalme akisema imekuwa, hakuna wa kupinga, HATA YEYE MWENYEWE HAWEZI KUPINGA ALICHOSEMA!

Kama Wafalme na Makuhani, tunapaswa kujua nafasi ya Ufalme tuliyonayo chini ya Mfalme wa Wafalme Yesu, na tuanze KUTOA MATAMKO AMBAYO YATATUKIA.
Watu, mazingira, hali za maisha, vyote vinasubiri maneno yetu kama Wafalme chini ya Mfalme Yesu!

Angalizo: Usichezee maneno yako ukishaokoka, unaweza kuharibu maisha yako kwa mdomo wako na ukamsingizia Shetani kumbe ni UPUMBAVU ulionao (Mithali 6:2).

MAOMBI

ASUBUHI

1. Mungu akupe kiu ya kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu, na kiu isiyoisha ya kuomba, kusoma Neno, kuangalia na kusikiliza mafundisho, vitabu na vyanzo vingine vya kukujaza maarifa na imani ya kusema vitu vikawa.
(Zaburi 27:4-14, Zaburi 23:6, Zaburi 63:1-9).

2. Muombe Mungu akusaidie kuyajua Mapenzi yake yaliyo mema, ya kumpendeza na makamilifu, ili iwe rahisi kwako KUHUKUMU KILA KIOVU NA KIBAYA MAISHANI MWAKO kwa maneno yako.
(Yeremia 29:11, Warumi 12:1-2).

3. Muombe Mungu akunasue kila mahali ambapo maisha yako yamenaswa kwa maneno ya midomo yako uliyojitamkia (Mithali 6:2).

MCHANA

1. Muombe Mungu, Uungu ulioubeba ndani yako uwe dhahiri ili maneno yako utakayotamka yazae vitu chanya na vyema kwenye maisha yako na watu wako.
(Warumi 8:16-17,19, Zaburi 82:6).

2. Muombe Mungu akiguse kinywa chako, ili kitamke mambo ya utukufu, ya kujenga na kugeuza maisha ya watu.
(Wakolosai 4:6, Waefeso 4:29).

3. Muombe Mungu akupe Roho ya imani, inayofanya mtu aamini lolote na kulisema kwa ujasiri bila mashaka (2Wakorintho 4:13, Marko 11:23).

JIONI

1. Mshukuru Mungu kwa kujibu maombi yote uliyoomba leo.
(Zaburi 66:20, Isaya 65:24).

2. Omba lolote unalotaka Mungu akutendee leo na kabla ya mwezi huu au mwaka huu kuisha!
(Marko 10:51, Luka 18:41, Mathayo 8:1-13).

NB: TAMKA NENO LA IMANI, LA BARAKA, LA ULINZI, USHINDI NA LA KUTUPA KUPIGA HATUA KWANGU MIMI MCHUNGAJI DICKSON, MKE WANGU MERCY NA KANISA LAKE LA ABC TUNALOCHUNGA!

Tukutane kesho siku ya tano,
Wewe ni jibu la maisha ya wengi,
Umebarikiwa mno!

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji kiongozi,
Assembly Of Believers Church (ABC),
25/03/2019

 

Pia usisahau kusoma Nyaraka zetu nyingine kama

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »