MFUNGO WA SIKU KUMI WA MWISHO WA MWEZI [SIKU YA SITA]

NEEMA YA KUTUEPUSHA NA MABAYA YANAYOWAPATA WENGINE

(THE GRACE TO BE EXCLUDED IN EVIL THAT BEFALL OTHERS).

•Ni kweli kwamba wote tumeumbwa na Mungu mmoja, tena wote tuna sura na mfano wake (Mwanzo 1:26-27).

•Wote tumetamkiwa baraka, ili tuzae na kuongezeka na kuijaza nchi na kuitiisha na kutawala mazingira yetu na kila kilichomo (Mwanzo 1:28).

•Ni kweli kwamba kila mmoja wetu ameumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha (Zaburi 139:13-16).

Lakini ninaweza kukuhakikishia jambo moja la muhimu, “Si kila linalompata mtu mwingine linaweza kunipata mimi…”

Tuna neema tofauti linapokuja suala la mabaya na majanga yanayowapata watu!

•Nuhu alikuwa na NEEMA MAALUM YA MUNGU iliyomuepusha kufa na wengine zama zile hasira ya Mungu ilipowaka na akaipiga dunia kwa gharika!

Nuhu alikuwa mtu wa haki, mcha Mungu na Mkamilifu katika vizazi vyake (Mwanzo 6:9), kutokana na Mfumo wake huu wa maisha, “ALIPATA NEEMA MACHONI PA MUNGU” (Mwanzo 6:8).
Na neema hii ilimuokoa Yeye, mke wake, watoto wake watatu na wake zao, na hata baadhi ya wanyama na viumbe!

Neema hii juu ya Nuhu ilimuokoa na kuokoa watu wake pia!

Neema hii ni halisi na ipo… Ukiyachunguza maandiko kwa uangalifu utaiona.

•Lutu naye alikuwa na neema hii maalum ya kuepushwa na mabaya yanayowapata watu wengine…

Ukisoma Mwanzo 18, Ibrahimu alikuwa anamshawishi Mungu kutopiga miji ya Sodoma na Gomora endapo atakuta wenye haki!

Hatuoni hata sehemu moja ambayo Ibrahimu analitaja jina la Lutu, au akimuomba Mungu asimuangamize Lutu.

Lakini NEEMA HII YA AJABU JUU YA LUTU ilimpa kuwatambua Malaika waliokuja kuangamiza Sodoma na Gomora kiwanjani, na kwa neema ya Mungu juu yake aliweza kuwashawishi kuja nyumbani kwake!

Neema hii maalumu juu ya Lutu ilikuwa na uwezo wa kumponya yeye, mkewe, mabinti zake wawili na wachumba zao!

Lakini wale vijana (wachumba wa binti za Lutu) waliichezea NEEMA JUU YA LUTU kwa kutomsikiliza, WAKAFIA SODOMA NA GOMORA!

Mkewe pia hakunufaika na neema hii juu ya mumewe, maana aligeuka njiani akaangalia nyuma akawa nguzo ya chumvi!
“Uwepo wa neema si kibali cha kutenda dhambi”

Mabinti zake walishikilia neema ile wakaponywa!

Lakini si Nuhu na Lutu pekee waliofaidika na Neema hii maalum ya Mungu ya kutuepusha na mabaya yanayowapata wengine…

•Hata kule Jangwani, Mungu alipoamua kuwauwa watu wazima wote wa Israeli waliomtilia Mashaka na kuyaogopa majitu (Hesabu 13 na 14), bado JOSHUA NA KALEBU WALIPATA NEEMA HII ILIYOWAEPUSHA NA MABAYA YALIYOWAPATA WENGINE…Wao hawakufia jangwani, walikuwa watu wazima pekee walioingia Kanani!

Na maandiko yanatuambia ni neema ya Mungu ndiyo iliyowaepusha na Upanga jangwani;

“BWANA asema hivi, WATU WALE WALIOACHWA NA UPANGA WALIPATA NEEMA JANGWANI…”
(Yeremia 31:2).

Kuna NEEMA YA MUNGU YA KUTUEPUSHA NA UPANGA unaoua wengine jangwani.

-Mpendwa wangu kuna neema ya Mungu ya kukuepusha na laana za ukoo wako!

-Kuna neema ya Mungu ya kukuepusha na matatizo ya ukoo wako!

-Kuna neema ya Mungu ya kukuepusha na ugumu na shida wanazoteseka nazo watu wengine.

-Kuna neema ya Mungu ya kukusaidia usife na magonjwa yaliyoua ndugu zako kwenye ukoo wenu.

Neema hii ni NEEMA MAALUM YA MUNGU YA KUTUEPUSHA NA MABAYA YANAYOWAPATA WATU WENGINE!

Ukipata muda ipitie Zaburi 91, ina mistari 16 tu.

Katika zaburi hii utajifunza siri za utendaji wa neema hii ya Mungu.

“Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo”
(Zaburi 91:3).

“Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio, Uaminifu wake ni ngao na kigao”
(Zaburi 91:4).

“Hutaogopa hofu ya usiku wala mshale urukao mchana”
(Zaburi 91:5).

“Wala tauni ipitayao gizani, wala uele uharibuo adhuhuri”
(Zaburi 91:6).

“Ijapokuwa watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam kumi elfu mkono wako wa kuume! HATA HIVYO HAUTAKUKARIBIA WEWE (Utaepushwa na hayo mabaya yanayowapata wengine wote)…”
(Zaburi 91:7).

Utakuwa tu mtazamaji wa mabaya yanayotokea kwa wasio haki (Zaburi 91:8).

Ndugu yangu, kama ulikuwa na mimi toka mwanzo, nadhani umeuona uhalisia wa neema hii ya kuepushwa na mabaya yanayowapata watu wengine!

Nakuombea Mungu akupe jicho la tofauti yanapokuja mambo ya muhimu sana kama haya, yaingie moyoni mwako na nafsini na uyang’ang’anie na kuyafaidi!

MAOMBI

ASUBUHI
1.Muombe Mungu akupe neema hii ya ajabu ambayo ni ya muhimu sana hapa duniani ambako ulimwengu wote uko chini ya mikono miovu ya Ibilisi (1Yohana 5:19)!

2. Muombe Mungu akupe neema ya kuepushwa na upanga, kama ilivyokuwa kwa Yoshua na Kalebu walivyoepushwa kufa na wengine (Yeremia 31:2).

MCHANA

3. Muombe Mungu akupe imani itakayokufanya uondolewe ili usipatwe na mabaya na uharibifu (Waebrania 11:5).

4. Muombe Mungu, pale hasira na ghadhabu yake inapopita popote ulipo UPATE NEEMA MACHONI PA BWANA kama ilivyokuwa kwa Nuhu (Mwanzo 6:8).

JIONI

5. Muombe Mungu akuondoe kwenye orodha ya wale ambao madhara na uharibifu vinaweza kuwatokea (Zaburi 91:1-10).

6. Muombe Mungu akupe Roho ya neema na maombi, ili uweze kutembea katika neema hii maalum (Zekaria 12:10).

NB: Tuombee mimi mchungaji Dickson, mke wangu Ikupa tudumu katika kutembea katika neema hii ya kuepushwa na mabaya yanayowapata wengine, kuhuduma, kifamilia, uchumi nk!

Tukutane kesho siku ya 7,
Umebarikiwa, wewe ni baraka kwa dunia yako!

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,
Assembly Of Believers Church (ABC),
27/03/2019.

 

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »