MOJAWAPO YA SABABU ZILIZONIFANYA NIKAZANE KUWA BORA- 02

“FURSA NI NYINGI MNO KWA WATU AMBAO NI BORA KWENYE WANACHOFANYA”

NILIGUNDUA, HAKUNA UHABA WA FURSA, HAKUNA UHABA WA MILANGO YA MAFANIKIO!

NILIGUNDUA HAKUNA UHABA WA PESA, HAKUNA UHABA WA MALI NA VITU KWENYE MAISHA HAYA!

NILICHOGUNDUA HAYA YOTE, AMBAYO NDIYO WATU HUAMKA MAPEMA NA KUCHELEWA KULALA WAKIYATAFUTA, HUWA YANAWAFUATA WATU AMBAO WAMEKUWA BORA KULIKO WENZAO!

NILIGUNDUA YA KWAMBA, UKIWA MTU BORA HUHITAJI MATANGAZO WALA KUSHINDANISHWA NA YEYOTE, UNASHINDA KABLA YA SHINDANO!

NILIGUNDUA WATU WENYE UBORA WA KIWANGO CHA JUU, HAWATAFUTI SOKO, BALI SOKO LINAWATAFUTA!

NILIGUNDUA YA KUWA WATU BORA, HAWATAFUTI MARAFIKI BALI MARAFIKI WANAWATAFUTA WAO!

HABARI NJEMA…

UBORA UNATENGENEZWA NA MTU YEYOTE TU, SI KITU CHA WATU MAALUM KAMA AMBAVYO WENGI TULIAMINISHWA…

UBORA NI MATOKEO YA:

-Wingi wa maarifa sahihi

-Nidhamu kwenye unachofanya

-Uaminifu

-Uadilifu

-Weredi

-Kutambua nafasi ya Mungu anayepandisha na kuinua wasio na vigezo

-Bidii katika kila jambo unalifanya

-Kuchukulia mikwamo, changamoto na magumu kama daraja la kukuandaa kufanya vizuri zaidi

-Matumizi mazuri ya kila siku yako moja

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

21/05/2019

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »