Ni muhimu uzingatie haya

katika Roho

Ili ukue katika maeneo yote ya utu wako; roho, nafsi na mwili!
Mtu ni roho, anayo nafsi (sehemu ya akili, uamuzi, utashi; mental faculty) na anaishi ndani ya mwili.

Biblia inatufundisha juu ya uwepo wa maeneo haya matatu ambayo kwa pamoja yanaunda kiumbe mmoja aitwaye mtu!

“Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake bwana wetu Yesu kristo” (1 wathesalonike 5:23).

Kila siku mtu anapaswa kukua kwenye maeneo yote matatu; lazima ujizoeze kulisha maeneo yote matatu, roho yako, nafsi na mwili wako; hakikisha kuna uwiano mzuri wa kiukuaji!

Roho yako; ilishe neno la Mungu, lisome, litafakari kwa kina katika hali ya maombi, na kisha anza kulitendea kazi kwenye maisha yako ya kila siku!
“mtu [ambaye ni roho] hataishi kwa mkate tu [chakula cha mwili] bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu [chakula cha roho]” (mathayo 4:4).
Vyakula vingine vya lazima na vya kuikuza roho yako ni pamoja na maombi na kufunga; usijidanganye kukua kiroho wakati unakula kila siku ya wiki, huna muda wa kuomba walau mara 3 kwa siku (asubuhi, mchana kabla au baada ya chakula na jioni baada ya harakati za siku); wengine wameshakwenda mbali kiasi kwamba kila saa wana dakika za kuomba bila kujali wako wapi na wanafanya nini!

Nafsi yako; hii inahitaji sana neno la Mungu, neno lina nguvu ya kuumba upya asili na tabia ya Mungu na kuifanya akili yako isiwe inayumbishwa na kila upepo unaokujia!
Hili eneo lijenge kwa kujenga tabia ya kujisomea vitabu mbalimbali vya kiroho, mafundisho na machapisho ya watumishi mbalimbali wa Mungu; eneo la nafsi yako hupokea taarifa kupitia mlango wa “macho yako na masikio yako”… Kile unachotazama sana; kile unachosikia sana kinajenga mfumo wako wa kimawazo na kifikra; na mfumo wako wa kifikra na kimawazo unajenga aina ya mtazamo wako kwenye kila jambo jema na zuri linalokuja maishani mwako; na mtazamo wako ndio unaoamua kiwango cha mafanikio au kushindwa kwako katika maisha ya kila siku na jumla ya siku zako duniani!

Mwili wako; huu unahitaji kula mlo kamili na ulio bora, wenye virutubisho vyote muhimu; wanga, protini, vitamini, fati na maji safi na salama ya kutosha!

Angalizo kuhusu mwili; usiuendekeze mwili na chakula, hapa ndiko ambako mwili huwa unapata nguvu na kukuelekeza kwenye uovu na dhambi… Jenga tabia ya kula wakati kuna ulazima wa kula; usipende kulakula; kula wakati una njaa, wakati wa ulazima; na uzoeze mwili wako kufunga na kumfanyia ibada; anza taratibu na kadri Mungu akuwezeshavyo utiishe mwili wako mbele za Mungu; dhambi kule edeni ilitokea kwenye kulakula; shetani alipotaka kumjaribu Yesu kule nyikani alikuja kwa sound ya chakula [mawe kuwa mikate] ; jizoeze kuutiisha mwili wako usipitilize kwenye kulakula sana!

Mwl d.c.k

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »