SIKU 30 ZA MAOMBI YA MIUJIZA NA MAAJABU [Day 2]

http://www.johnteranceturner.com/images/portfolio/general/large/p_gen_4b_x.jpg
Day 2, 06/02/2016.
NEEMA

ASUBUHI
“NEEMA YA KUEPUSHWA NA MABAYA YANAYOTOKEA KWA WENGINE”
“Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”
(Mwanzo 6:8).
Haijalishi wengine wanakwama, wanashindwa, wanaugua, wanakufa, wanafilisika, wanapoteza ndoa, wanakufa…. Kuna NEEMA MAALUM YA KUKUEPUSHA NA MABAYA YANAYOWAKUMBA WENGINE WOTE.
“Japokuwa elfu wataanguka mkono wako wa kushoto na kumi elfu mkono wako wa kuume lakini HAUTAKUKARIBIA WEWE. Ila kwa macho yako UTATAZAMA NA KUONA MALIPO YA WASIO HAKI… MABAYA HAYATAKUPATA WEWE…WALA TAUNI HAITAKARIBIA HEMA YAKO…”
(Zaburi 91:7-10).
Naizungumzia NEEMA aliyokuwa nayo Lutu, ikamwokoa asife pamoja na watu wa Sodoma na Gomora.
(Mwanzo 19:15-22).
Naizungumzia NEEMA aliyokuwa nayo Yesu; iliyomuepusha asife na watoto wote waliouwawa kule Israeli wakati anazaliwa.
(Mathayo 1:7-18).
Naizungumzia NEEMA iliyokuwa juu ya Shedraka, Meshack na Abednego na kuwafanya wasife kwenye moto ambao uliwaua askari waliokuwa wanataka kuwatupa motoni na ukakata kamba zao.
Naongelea neema ambayo inamsukuma MTU WA NNE aje kukusaidia katikati ya mipango mibaya na mibovu ya adui dhidi yako.
(Danieli 3:20-30).
Naizungumzia NEEMA iliyokuwa juu ya Danieli, kiasi kwamba alipotupwa kwenye SHIMO LA SIMBA WENYE NJAA, ilibadilisha appetite zao, wakasahau hata biashara ya kumla.
Neema iliyopelekea MALAIKA KUJA NA KUWAFUNGA MIDOMO SIMBA ili wasimguse Danieli.
Nataka ukimaliza maombi haya, kila mdomo uliofunguliwa kukumeza ujifunge.
Na maadui zako waingie mahali pako katika jina la Yesu!
Naizungumzia NEEMA iliyokuwa juu ya Daudi kumuokoa na kila mpango wa Sauli wa kumuua.
Neema ya Mungu ya kukutoa kwenye mabaya yanayowakuta na kuwatokea wengine.
Tukutane mchana ukiwa umeipokea neema hiyo ya ajabu.
Mwl D.C.K
www.yesunibwana.org
(Nimeona niwamegee kidogo japo nilishasema sitaweka kwenye group nyingine, ili walau ujue tunapokea nini huko kwenye mbio za siku 30).
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »