SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 28]

https://i0.wp.com/previews.123rf.com/images/gstockstudio/gstockstudio1405/gstockstudio140500386/28169259-Great-news-Happy-young-African-man-in-formalwear-talking-on-the-mobile-phone-and-expressing-positivi-Stock-Photo.jpg?resize=954%2C63501/02/2016.
“SABABU KUMI NA MBILI ZA KIBIBLIA KWANINI USIWE MASIKINI (TWELVE BIBLICAL FACTS WHY YOU ARE SUPPOSED NOT TO BE POOR AT ALL)”
1. Umebeba sura na mfano wa Mungu ambaye ni tajiri (Zaburi 24:1, Hagai 2:8), aliyefanikiwa katika kila eneo na hana mpango wa kuwa masikini.
Kilichomfanya Mungu apumzike siku ya 7, ni ile kujua amekuumba wewe ambaye ni “udhihirisho wa Yeye” katika dunia.
(Mwanzo 1:26-27).
2. Ndani yako Mungu ameweka uwezo na ufahamu wa “kumilki na kutawala” rasilimali alizoumba kwa siku 5 kabla ya kukuumba siku ya 6. Kama ukijielewa na kujipambanua, na ukatafuta tu maarifa kidogo kuhusu matumizi ya hizo rasilimali, hauwezi kuwa masikini.
(Mwanzo 1:28).
3. Tangu siku ya kwanza Mungu alipokuumba amekubariki. Na baraka ya Mungu ikiwa juu ya mtu humfanya kuwa tajiri, maana inatajirisha.
Yakobo hakurithi mali hata moja ya Isaka, maana alikimbia mikono mitupu ili asiuwawe na Esau, lakini aliondoka na BARAKA YA MUNGU JUU YA ISAKA NA IBRAHIM ambayo ndani ya miaka 15 tu ilitosha kumfanya tajiri mkubwa mno zaidi ya Esau.
(Mwanzo 1:28, Mithali 10:6, 22).
4. Mungu ameweka ndani yako uwezo wa “kuzaa vitu na kuviongeza” ambao ni mtaji mkubwa sana wa utajiri. Ukijua kutumia hiyo nguvu ya baraka na picha ulizonazo “kuanzisha (kuzaa) vitu, na kisha “kuvipanua (kuongezeka)” hakika hautakuwa masikini.
Yesu alijua kanuni hii, alipokutana na Petro bila samaki, alipolisha wanaume elfu tano, alipotengeneza divai kule Kana ya Galilaya nakadhalika.
Vyote hivi Yesu alivizaa na vichache aliviongeza.
Una nguvu ya kuzaa vitu na kuviongeza.
Akili, nguvu na maarifa uliyotumia kuanzisha biashara moja hayohayo yanatosha kuanzisha kitu kingine tena na tena.
Sasa unakuta mtu ana duka hilo moja miaka na miaka. Ina maana ile akili iliisha ulipoanzisha (ulipozaa) hilo duka? Amka fanya tena na tena na tena!
(Mwanzo 1:26-28).
5. Mungu ameweka kila kitu alichokiumba chini ya utawala na udhibiti wa mwanadamu, akiwa na kusudi kubwa la kumfanya mwanadamu asi struggle kuwa succesful kwenye kila eneo la maisha.
(Zaburi 8:4-8, Zaburi 115:16).
6. Mungu tunayemwabudu katika Kristo Yesu, ndiye anayetoa nguvu za kupata utajiri. Yeye hutajirisha. Na kwake kuna utajiri na heshima.
(Kumbukumbu 8:18, 1Samweli 2:7-8, Mithali 8:18-21).
Hakuna haja ya kuwa masikini ilhali unamuabudu Mungu atoaye nguvu (upako) wa kutajirisha.
Mungu ainuaye wanyonge toka mavumbini na kuwaketisha juu na wakuu.
7. Mungu tangu mwanzo alitenga utajiri maalum kwa ajili ya wana wa Israeli, wazao wa Yakobo, wazao Ibrahimu… “Utajiri wote watakaopewa Israeli” (1Samweli 2:32), Kuna utajiri maalum kwa ajili ya Israeli, wazao wa Ibrahimu, na kila aliyeokoka ni mzao wa Ibrahimu na mrithi wa ahadi hii (Wagalatia 3:7, 9, 13-14, 29, Wagalatia 4:28-31).
Wazao wa Ibrahimu tu warithi sawa na ahadi.
Zaidi ya yote tu “wamilki wa ulimwengu” (Warumi 4:13).
8. Kusudi mojawapo la Mungu kumfufua Yesu ni ili ATUBARIKIE NA KUTUTOA KILA MMOJA KATIKA DHAMBI ZAKE. Si kututoa tu kwenye dhambi bali pamoja na kugeuza hali zetu kwa baraka zake kwetu.
(Matendo 3:25-26).
Yesu amebeba baraka zako nyingi sana, ni suala la kufumbuka macho na kumwambia akusaidie ujue namna ya kuzipata katika uhalisia.
9. Kuna neema maalum ambayo Yesu aliiachilia ambayo inamsaidia mtu kutoka kwenye umasikini. Itumie hiyo “neema ya Bwana wetu Yesu Kristo” ambaye hapo mwanzo alikuwa tajiri, lakini alifanyika masikini ili sisi tupate kuwa matajiri kwa umasikini wake.
Ni neema maalum inayofuta umasikini kwa kila anayepata kuielewa.
(2Kor 8:9).
Rejea somo la NEEMA YA UTAJIRI.
10. Biblia inasema tunapookoka, tunapata haki kisheria ya kupata utajiri, bila kujali ni Myahudi au Myunani. Kwa maana Yesu Kristo ni BWANA wa wote “mwenye utajiri kwa wote wamwitao”
(Warumi 10:11).
NI HABARI NJEMA KUJUA YESU ANA UTAJIRI “KWA WOTE WAMWITAO” …. Si utajiri kwa baadhi ya watu, bali kila ANAYELIITIA JINA LAKE!
11. Kati ya vitu saba (7), ambavyo Yesu alivipokea “kwa ajili ya kanisa” baada ya kukubali kufa na kufufuka, ni utajiri.
Si utajiri kwa ajili yake, ni utajiri kwa ajili ya mwili wake, yaani Kanisa.
(Ufunuo 12:12-13).
Huu utajiri ambao Yesu ameupokea baada ya kukubali KUCHINJWA SI KWA AJILI YAKE KAMA KICHWA TU, NI WETU PIA KAMA MWILI WAKE!
Kilicho mali ya kichwa kinanufaisha mwili wote.
Kilicho mali ya mzabibu kinanufaisha matawi (Yohana 15)!
12. Kila aliyeokoka ni mwana wa Mungu tajiri. Kila aliyeokoka ni mrithi halali kisheria wa kila alichonacho Mungu. Kila aliyeokoka anarithi kila kitu alichonacho Mungu pamoja na Kristo Yesu. Na huwezi kuelewa hili ukakubali kuwa masikini.
(Wagalatia 3:29, Wagalatia 4:28-31, Warumi 8:16-17, Warumi 4:13, 16).
Ukitafakari hizi sababu kumi na mbili, hakuna haja ya kuwa masikini.
JITAMBUE:
“WEWE NI TAJIRI NA SI MASIKINI KAMWE. UKIAMUA KUWA MASIKINI UNAIDHALILISHA KAZI YA MSALABA NA KWELI ZA NENO LA MUNGU”

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »