SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 4]

https://learningthewayofwisdom.files.wordpress.com/2014/05/closer2god.jpg?w=350&h=200&crop=1
Day 4, 08/01/2016.
ASUBUHI

“KUTEMBEA NA MUNGU”

Mwanzo 5:22,24
“Henoko AKATEMBEA PAMOJA NA MUNGU…Henoko AKATEMBEA PAMOJA NA MUNGU, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa”
Kutembea na Mungu! Kutembea na Mungu!
Daaah, ninavyotamani kutembea na Mungu… Henoko ananifanya nami nitake kutembea na Mungu.
Henoko alitembea na Mungu kwa miaka 300 mfululizo baada ya kumzaa Methusela, kiasi kwamba ule ushirika na urafiki kati yake na Mungu ulimfanya Mungu AMCHUKUE MBINGUNI MZIMA MZIMA.
Natamani kutembea na Mungu kwa viwango hivi bora.
Imagine miaka 300 bila kupoteza ushirika na Mungu.
Bila kurudi kuishi maisha ya dhambi.
Bila kuvutwa na dunia na tamaa zake.
Bila kushawishiwa na marafiki wa dunia hii.
Miaka 300 akiwa katika viwango vya upekee… Naamini alibadilika na kuwa kama “muungu pia” kiasi cha Mungu kuona huyu hafai kukaa na wanadamu wengine wa kawaida.
Huyu Mungu hajabadilika.
Anatafuta watu ambao atakuwa na ushirika nao na kutembea nao.
Yesu alisema anatafuta watu kama hao; “Maana Baba hutafuta watu kama hao wamwabudu” (Yohana 4:23).
Watu ambao maisha yao yote yatakuwa yanamueleza na kumfunua Mungu hata wasipofungua mdomo kusema chochote.
Watu ambao ndoa zao zitamuonesha Mungu, watu ambao biashara zao zitamfunua Mungu, watu ambao uwepo wao ofisini/ makazini mwao utapelekea watu wa-notice kuwa hawako na huyo mtu peke yake bali na Mungu mzima mzima (Mwanzo 39:2-4).
Ukifika level hizi; Watu watajua kuwa una Mungu. Hautaomba kupanda vyeo, wakinotice uwepo wa Mungu watakuweka kuwa msimamizi na kiongozi juu ya wengine.
Natamani utembee katika neema hii.
Utembee katika viwango hivi.
Siri yake kubwa iliyomfanya atembee na Mungu ni KUKATAA KUFANYA DHAMBI.
MUNGU NI MTAKATIFU, HAFANYI KAZI NA WATU WACHAFU; USIJARIBU KUTENDA UBAYA HUO NA KUMPOTEZA MUNGU NA UWEPO WAKE; MAFANIKIO YAKO YAMEFUNGWA KWENYE UWEPO WA MUNGU ULIONAO.
(Mwanzo 39:7-10).
Dhambi inakula na kupunguza UTUKUFU WA MUNGU (Warumi 3:23).
Utukufu wa Mungu ukiondoka, kibali na mvuto umeondoka.
Utukufu ukiwepo, hautatumia nguvu kufanya vitu vitokee.
(Isaya 60:1-4).
Usipoishi maisha matakatifu kama LIFESTYLE giza linalofunika wengine litakufunika na wewe.
Badala ya kung’aa na kuwa nyota katikati ya giza, utafunikwa.
Tembea katika utakatifu kama unavyopumua.
Namkumbuka Daniel mwanaume aliyepata kuwa Waziri mkuu chini ya Wafalme watatu tofauti.
Ilifikia hatua hata wapagani wakasema hivi kuhusu yeye;
“Roho ya Miungu watakatifu inakaa ndani yako”
(Daniel 4:18, Daniel 5:11, Daniel 5:14).
Huyu jamaa alikuwa busy sana na kazi, lakini bado alikuwa anaweza kukutana na Mungu kuzungumza naye MARA TATU KWA SIKU (Asubuhi, mchana na jioni); Danieli 6:10.
Wewe ni waziri wa nini vile? Na una round ngapi za kuwa na Mungu?
Tafakari njia zako.
Kuna gharama ya kulipa ili utembee na Mungu.
Mungu anataka moyo wako.
Mungu anataka muda wako.
Mungu anataka mali yako.
Mungu anataka elimu, kazi na kila ulichonacho.
Anataka umuabudu kupitia hayo pia.
Yesu naye ametembea na Mungu sana.
Maandiko yanasema hivyo; “…akapita huko na huko akiponya wote walioonewa na Ibilisi KWA KUWA MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE”
(Matendo 10:38).
Siri ya miujiza na maajabu aliyofanya ni UWEPO WA MUNGU (KUTEMBEA NA MUNGU)… Nikodemo aliona na kujua hilo, kuwa Yesu anatembea katika miujiza na maajabu kwa sababu MUNGU YUKO PAMOJA NAYE (Yohana 3:2).
Hakuna miujiza, ishara na maajabu kama hakuna UWEPO WA MUNGU.
Nataka baada ya mfungo huu, uwe mtu wa miujiza, ishara na maajabu.
Ila hayatatokea kama MUNGU HATAKUWA ULIPO NA HATAKUWA NA KILA USEMACHO.
Samweli alikuwa nabii mkubwa anayeheshimika na anayetembea katika miujiza kwa sababu, MUNGU ALIKUWA PAMOJA NAYE NA HAKUACHA NENO LAKE HATA MOJA LIDONDOKE CHINI.
(1Samweli 3:19).
Kama ukiweza kutunza uwepo wa Mungu, kila neno usemalo na kukusudia litathibitika kwako (Ayubu 22:28).
Nenda kaweke mikakati hii katika maombi.
Nataka nikuone ukitembea na Mungu kwa viwango vya ajabu mno.
Ikimpendeza Mungu uonane na kuongea naye uso kwa uso.
(Mwanzo 32:30, Kutoka 33:11, Hesabu 14:14).
TUKUTANE MCHANA SHUJAA WANGU

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »