Thamani ya Yesu

Mungu akiangalia hapa duniani, anaona vituko, anawaona wanae (tulionunuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu) tunaishi maisha chini ya kiwango. Anashangaa kwanini hatuna tofauti na watu wengine wa kawaida wasiomjua. Anashangaa kwanini sisi ni masikini ilhali Yesu alishafanyika masikini ili sisi tuwe matajiri kwa Yeye.

Anashangaa kwanini miili yetu imekuwa masikani ya magonjwa, maradhi na madhaifu ya kila namna badala ya masikani ya Roho wake mtakatifu. Anashangaa kwanini tuna tabia kama za binadamu wa kawaida ilhali Roho wake mtakatifu yumo ndani yetu na anayo MATUNDA YA ROHO KWA AJILI YETU.

Anashangaa kwanini tuna mawazo ya ubinafsi wakati Yesu alishaonesha kielelezo kwamba lazima tuishi kama SADAKA kwa ajili ya wengine. Anashangaa kwanini tunakimbilia miujiza wakati sisi wenyewe ni miujiza, ni wanadamu pekee wenye kuishi katika dunia iliyochafuka na bado hatutendi dhambi. Anashangaa kwanini tumekazana kutafuta umaarufu na majina hapa duniani ilhali hapa ni mahali pa muda tu na kuna siku tutang’ara kama jua (si zaidi ya miaka 100 toka sasa).

Anashangaa kwanini tunayaamua mambo yetu kwa kutegemea milango 5 ya fahamu badala ya NENO LAKE. Anashangaa kwanini tunaenenda kama mataifa wasio na akili ilhali sisi wa dunia hii kama Kristo Yesu asivyo wa dunia hii. Anashangaa kwanini tunawekeza muda wetu na nguvu zetu katika vitu visivyo na thamani ya milele.

Ebu amua kuwa wa tofauti, ishi sawa na Neno la Mungu, kipimo chako cha ubora kisiwe mtu fulani bali Neno la uzima. ** MUNGU ANASHANGAA- Na Mwl. Dickson**

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »