UJASIRIAMALI UNAHITAJI ROHO YA PAKA..!!

https://yesunibwana.files.wordpress.com/2016/10/c581a-daladala.jpg?w=1200
Wakati fulani huko nyuma nimepata kufanya biashara ya daladala ambapo nilifanikiwa kuwa na daladala kadhaa(Hiace) na mauzo ya “kumwaga” yalikuwa yanaingia “daily”. Kisha nikafanya uamuzi wa kuuza magari yote ili niingie kwenye biashara ya majengo. Ile biashara ya majengo ikanitenda na nikapigwa mweleka wa “kuingizwa mjini” hela za magari yote. Siku nagundua kuwa nimepigwa zile hela kwenye akaunti nilikuwa na Tsh. 56,000/= (elfu hamsini na sita pekee!) na madeni juu. Watu wangu wa karibu wakanihurumia na wakanishauri kuwa kwa hasara niliyopata na maisha yanavyoniendea ni bora nitafute ajira ili nijipange upya. Hawakuishia kunishauri bali wakanifanyia na mpango wa ajira mahala fulani. Nilipofika maeneo yale ya ajira moyo wangu ukakataa kata-kata na nikagoma kuajiriwa. Niliwaudhi na kuwahuzunisha hawa watu wangu wa karibu kiasi kwamba wengine walilia sana na wakaamua kama kunisusa. Nikawaambia kati yenu hakuna anaenielewa sasa, lakini kuna siku mtanielewa. Sina hela ya kuishi, sina mtaji lakini nina wito wa kujiajiri, pamoja na yaliyonipata ninaendelea kujiajiri! Anewei stori ni ndefu namna nilivyoingia kupambana hata sasa nimeendelea kujiajiri lakini wale wale ambao hawakunielewa nilipokataa ajira sasa hivi, wote wananiita shujaa! Nimeona nikupe huu mchapo ili pointi nne zifuatazo zikuingie kirahisi:
1) Ujasiriamali sio sawa na kucheza draft, kwamba ukisogeza kete hapa unakula pale. Ujasiriamali ni mapambano na hakuna garantii ya kupata. Unaweza kuingiza mtaji na kupigwa mweleka na ukabakiwa na madeni. Nasema hii pointi kwa sababu Mtumbua majipu kawapiga presha wafanyakazi kiasi kwamba wengi wanafikiria kwenda kujiajiri. Niwaeleze wazi ya kwamba presha za mtumbua majipu hazitii mguu kwa presha za ujasiriamali. Fikirini kwa umakini maana huku kuna hela lakini sio nyepesi kama kupata mshahara! Karibuni lakini mtazamo wa kimshahara(kwamba ni lazima kila mwezi uingie) ziacheni huko huko!
2) Suala la kujiajiri msingi wake ni maamuzi na nia ya kujiajiri kamwe sio mtaji. Ukiamua kujiajiri maana yake ni njia umeamua kuipita. Mtaji hauanzishi safari ya kujiajiri isipokuwa ni matokeo ya wewe kuamua kujiajiri. Ninaposikia mtu anasema “Nimeamua kuajiriwa, ili nijipange na kutafuta mtaji ndipo nikajiajiri”: huwa nagundua mtu huyo, “Hajui alisemalo”! Ni nadra sana ajira kukukusanyia mtaji wa ujasiriamali kwa kuwa sayansi ya mshahara inakataa mfanyakazi kulipwa mshahara unaotosha. Kama mshahara unafeli kutosheleza mahitaji yako ya mwezi kwa asilimia 100, (huo mshahara) utatoa wapi jeuri ya kukukusanyia mtaji? Hata ukifanikiwa kuupata huo mtaji kupitia ajira, ikatokea sasa mtaji unao, umeacha ajira na kwenda kuanzisha biashara then ukaja ukapigwa mweleka(kama mimi), Je, utarudi tena ajirani kutafuta mtaji mwingine? Usisahau kuwa kwenye ujasiriamali kuna mieleka ya “kumwaga”!
3) Ukiamua kujiajiri(hasa nyie mnaotaka kuacha ajira na kwenda kujiajiri) usisubiri ama usitake kila mtu akuelewe ama akuunge mkono. Maamuzi ya kujiajiri (hasa kama umesoma) huwa hayaungwi mkono na jamii zetu. Usishangae utakapoona hata mke, mme, wazazi na marafiki wa karibu watakapokuwa wapinzani namba moja. Ukiamua kujiajiri, wewe nenda, wasiokuelewa sasa watakuelewa mbeleni. Uzuri ni kwamba muda utafika hata waliokupinga ama kukukatisha tamaa watakusifu sana. Eleweni kwamba maamuzi ya kujiajiri hayahitaji demokrasia bali unayafanya kidikteta kuanzia ndani yako mpaka kwa wanaokuzunguka.
4) Mafanikio ya vitu katika ujasiriamali na hata maisha kwa ujumla, sio jambo la kujivunia. Unachotakiwa kujivunia ni akili ya utafutaji iliyojengeka katika kuvisaka hivyo vitu. Unapopata hasara kama nilivyopoteza magari yote, kinachobaki kukuokoa ni akili ya utafutaji. Maisha yamenifundisha kuwa ukibahatika kumiliki vitu kama nyumba, magari, mashamba n.k, usithubutu kujisifia navyo ama kuwaringishia wengine maana ni kama maua ambayo yanaweza kunyauka. Na hata visipoyeyuka: kuwaringishia wengine kwa vitu unavyomiliki ni “utoto”.
#SmartMind
Albert Nyaluke Sanga

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »