UKARIMU NA UTOAJI HAVIANGALII HALI YA MAISHA NA UCHUMI

Mtu Anayesubiri Hali Yake Ya Kimaisha Na Uchumi Iwe Nzuri Ndipo Awe Mtoaji Kwa Mungu Na Baraka kwa Wengine KAMWE HALI YAKE HAITABADILIKA!
Mungu Anazitumia MBEGU NDOGO NDOGO Tunazopanda Katika Viwango Vyetu Vya Chini Vya Maisha Kutupa Maisha Tunayoyatarajia.
PESA Haiwezi Kubadili TABIA YA MTU… Kama Alikuwa MNYIMI Akiwa MASIKINI Akiipata Hataweza KUITOA Maana Atasema KUNA SEHEMU ANAIWEKEZA… Hata Siku Moja, Pesa Haitakuja Kutosha, Kadri Kiwango Chako Cha Maisha Kinavyopanda Na HADHI YAKO PIA INAPANDA Na Hiyo INAONGEZA MATUMIZI YA PESA HUSIKA… Hakika Kama Huwezi Kuwa Baraka Kwa Kidogo Ulichonacho Leo, Sahau Kuwa Baraka Kesho Ukipata Kikubwa!
UTOAJI NA UKARIMU NI TABIA, SI KIASI CHA VILE ALIVYONAVYO MTU
UTOAJI NA UKARIMU NI MATOKEO YA MOYO WA UPENDO ULIOMO MOYONI MWA MTU AMBAO WINGI AU UCHACHE WA MTU HAUWEZI KUUGEUZA!

“Akaja Mwanamke Mmoja, Mjane, Masikini, Akatia Senti Mbili, Kiasi Cha Nusu Pesa. [Yesu] Akawaita Wanafunzi Wake Akawaambia, Amin, Nawaambia, Huyu Mwanamke Mjane, Masikini Ametia Zaidi Kuliko Wote Wanaotia Katika Sanduku La Hazina; Maana Hao Wote Walitia Baadhi Ya Mali Iliyowazidi; Bali Huyu Katika Umasikini Wake Ametia Vyote Alivyokuwa Navyo, Ndiyo Riziki Yake Yote Pia” (Marko 12:42-44).

“Tena Ndugu Zetu, Twawaarifu Habari Ya Neema Ya Mungu, Waliyopewa Makanisa Ya Makedonia; Maana Walipokuwa Wakijaribiwa Kwa Dhiki Nyingi, Wingi Wa Furaha Yao Na Umasikini Wao Uliokuwa Mwingi Uliwaongeza Utajiri Wa Ukarimu Wao. Maana Nawashuhudia Ya Kwamba Kwa Uwezo Wao Na Zaidi Ya Uwezo Wao, Kwa Hiari Yao Wenyewe Walitoa Vitu Vyao” (2Wakorintho 8:1-3).

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »