UNAWEZA KUWA NA BWANA YESU NA UWEPO WAKE KILA SEKUNDE NA KILA MAHALI KAMA UKIFANYIA KAZI KANUNI HII

mfuate Yesu

Kila MKRISTO Anataka Pale Yesu Atakapokuwa Na Yeye Awepo Kila Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Na Mwaka!
Yaani Kila Mmoja Wetu Anataka Akae Kwenye Uwepo Wa Bwana Yesu.
Hili Ni Jambo Linalowezekana, Lakini Linahitaji Gharama Ambayo Yesu Aliisema Kwenye Yohana 12:26, “MTU AKINITUMIKIA, NA ANIFUATE; NAMI NILIPO, NDIPO NA MTUMISHI WANGU ATAKAPOKUWA”
Kuna Mambo Mawili Hapa Kama Unataka Kila Sekunde Uwe Na Yesu Na Uwepo Wake;
1. MTUMIKIE YESU
Wengi Wanadhani Watumishi Wa Mungu Ni Wale Wa Madhabahuni Kanisani… Siyo Kweli. Kila Mtu Aliye Ndani Ya Yesu ni Mtumishi Wa Mungu. Ila Tunatofautiana Kwenye Swala La Uaminifu Wetu Katika Kutumika Katika Hizo NAFASI AU MADHABAHU Alizotupa Kazi Bwana Yesu Alipotuokoa!
“MTU NA ATUHESABU HIVI, YA KUWA TU WATUMISHI WA KRISTO NA MAWAKILI WA SIRI ZA MUNGU… NA KINACHOTAKIWA KATIKA UWAKILI, YAPASA MTU AWE MWAMINIFU” (1Wakorintho 4:1-2).
Maana Yake Utumishi Wako Mungu Anaupima Katika Yale Maeneo Ambayo Mungu Amekupa Nafasi Ya Kuhusika Nayo Moja Kwa Moja. Yaani Yale Maeneo Yanayokuhusu Na Kukugusa Moja Kwa Moja!
Mungu Amekununua Kwa Damu Ya Yesu Ili Uwe Wakili (Mwakilishi) Kwenye FAMILIA YAKO, NDOA YAKO, KAZINI KWAKO, KANISANI KWAKO, KAMPUNI YAKO, BIASHARA YAKO Nk. Yaani Ukiwa MWAMINIFU Hapo, Na Kuwa Chumvi Na Nuru Hadi Mungu Kupata Utukufu Kupitia Wewe, Hapo Unakuwa Umekuwa Mtumishi Mwema Na Uwepo Wa Bwana Yesu Lazima Uwe Nawe Kila Sekunde!

2.MFUATE YESU
Biblia Inatuambia Katika Waefeso, “HIVYO MFUATENI MUNGU KAMA WATOTO WANAOPENDWA” ( Waefeso 5:1). Ukiusoma Mstari Wa 26 Wa Yohana 12, Kipande Cha Pili Cha Mstari Huo, Yesu Anasema Baada Ya Kuwa MTUMISHI WAKE, Kinachofuata Anasema Ni KUMFUATA!
Nini Maana Ya kumfuata Yesu?
Kumfuata Yesu Ni Kufuata KIELELEZO CHAKE… Ni Kuendesha Maisha Kwenye VIWANGO VYA YESU… Kama Yeye Alivyoishi Na Kuenenda Ndivyo Tupaswavyo Kuenenda!
Yesu Anatuambia Katika Mathayo 11:29, “JITIENI NIRA YANGU MKAJIFUNZENI KWANGU, MAANA MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU WA MOYO”
Lakini Pia Ni Muhimu Ukumbuke Kuwa Yesu Ni NENO LA MUNGU KATIKA MWILI (Yohana 1:1-3, 14). Kama Ukiishi Kwa Kulifuata Neno La Mungu, Na Kulitii, Unakuwa Umemfuata Kristo!
MUNGU AKUSAIDIE KUFANYA HAYA MAWILI: MTUMIKIE YESU LAKINI PIA MFUATE YESU!
Wako Katika Kristo,
Mwl D.C.K

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »