WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

 

USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA!

Image may contain: Ibrahim Amasi

Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA.

Huu ni USHUHUDA wangu mwenyewe!

Hivi nikikuambia kati ya Februari 2015 na Desema 2016 nilipoteza zaidi ya 10,000,000/- (milioni kumi) kwa kubeti utaamini? Sina sababu ya kuendesha ligi isiyo na kikombe kubishana na wewe! Ni zaidi ya 10m please niamini

Aisee nilianza kama utani;

Washikaji wakaniambia ni moja ya dili zinazolipa sana mjini. Eti unaweza kubeti kwa dau la jero au buku ukipatia mkeka wako unaweza ‘kula’ hadi laki nne!
Nikaanza kujipinda kusuka mikeka, awali hizo nikawa sijui bado kubeti mtandaoni. Nikawa siku zangu za off (ambazo sipo kazini) nakalia viti vya MERIDIAN BET pale jirani na Azania bank kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manani.
Mimi na mikeka, mikeka na mimi!

Kubeti ni hatari wa kubahatisha, hakuna cha huyu ni mzoefu au huyu ni underdog.. wote ni ‘kuliwa’ mtindo mmoja!
Basi bwana, yani nililiwa hadi nikahisi kupata presha. Nikirudi home nina full hasira, namnunia wife as if yeye ndiye aliyenituma. Ni wazi kuwa zaidi ya nusu ya mshahara wa Acacia Buzwagi uliishia kwenye kubeti!
Tulikuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba na wife kwenye akaunti separate na ile ya mshahara lakini niliifilisi kwa ku draw fedha kwa siri ili nikakomboe hela niloliwa lakini nashtukia naliwa tena.

Baada ya kama miezi 6 nikapata dili la kubeti mtandaoni (online football betting). Nikaendelea kukomaa ili nirudishe Mpunga wangu ulopotea kwani kwa almost nilikula elfu arobaini na sita tu kwa mkeka wa 5000. Nilizokuwa nimeliwa hapo usiulize!

Kwa kuwa tayari nilikuwa na kompyuta mpakato(Laptop), nilianza zoezi kwa sura mpya! Najaza mb za kutosha na hela ya kubetia.
Hapa nilifanya kazi deep na kisomi zaidi kumbuka nipo serious kukomboa hela.
Kabla sija place betting slip naichunguza timu vizuri kwa maana ya uwezo wake, rekodi yake at least six meetings, injury za key players n.k.
Hii haikunisaidia!! Niliendelea kuliwa vibaya sana! Hadi nikajisemea haya makampuni ya kubetisha ni ‘wachawi’ hatari!
Unamwamini Barcelona kwa umahiri wake lazima ashinde kwa Espanyol, natupia laki unashangaa anatoa droo! Najisemea moyoni, sitabeti tena na huu ujinga sitaki tena lakini utashangaa umerudimo tena. Believe me kuna roho za kipepo kwenye betting! Ukiingia huwezi kutoka kwa nguvu na juhudi zako!

Nilikuwa nakaa sebuleni hadi usiku wa saa saba,SAA nane nasuka mikeka! Wife analala anachoka anakuja kunicheki anauliza kulikoni, namjibu nina assignment kibao za kazini please niache! Ndoa ilikuwa hatarini sana sana!

Jambo kubwa kabisa nililojifunza kwenye michezo hii ya KAMARI, bora uliwe tuu hadi mwisho kwani ukila au ukisikia fulani amekula, ndo hamasa ya kucheza inazidi na kuzidi.
Hii ilitokea pale nilipo kula milioni moja nablaki mbili kwa mtaji mdogo wa 25,000.
Ni kama robo tatu yote ilirudi kubeti na kuliwa tens!
Hali iliendelea kuwa mbaya kwani nilizidi kupanda dau hata kufikia laki mbili kwa tiketi moja! Ninapokuambia milioni kumi ilikata na zaidi namaanisha!!

Ninayo mengi ya kukuambia ila ngoja niikatishe ili nikitonye jambo muhimu zaidi.
Pamoja na kwamba nilikuwa ninasali na nimeokoka hali hii ilizidi kunitesa! Nilikuwa mtu mwenye hasira kiasi kwamba…ready to kill or to be killed!
Wapo watu hapa fb ni mashuda hasa wale tulofanya nao mgodini Buzwagi. One time niliwahi kumbana mtu akiwa anaendesha gari tena eneo hatari la Ramp kuelekea chini shimoni. Hii story nitakupa siku nyingine.

Namna nilivyochomoka;

Siku moja nikiwa kazini Jamaa mmoja alinitonya juu ya kanisa la ABC lililopo Nyahanga kaibu na Kahama Fm Redio. Aliniambia kuna watumishi wawili wa Mungu hatari! Akadai watu wengi wanafunguliwa na wagonjwa wanapona! Akasema hata walevi, wavuta sigara na wote wenye tabia sugu wanawekwa huru.

Niliamini 50/50 hivyo sikuwa na haraka ya kukimbilia hiyo huduma, nikaendelea kubeti!
Kuna siku nililiwa almost laki 3 na at the same time mm na wife hatuongei. Nikaona niende ABC nione kuna jipya gani..
Aisee wewee! Nilikutana na shoti ya Umeme wa Gredi! Mashuhuda wanaweza kueleza vizuri kuliko mimi. Nilifika nikakalia kiti wala sikumweleza yeyote shda yangu.

Kuanzia siku ile tamaa ya kubeti – KWISHA, hasira – KWISHA! Yapo mengi tu Bwana Yesu aliyafanya kwangu kupitia mikono ya watumishi wake na kwa hakika nipo HURU! Kwa sasa nalelewa na watumishi hawa wenye maarifa mengi ya ki Mungu na for sure maisha Yangu sasa ni tofauti sana kiroho na kiuchumi.

USIKUBALI KUTESEKA, MAJIBU YAKO YAPO!! NJOO ABC NYAHANGA KIVULINI (KWA KAHAMA ANAKOCHUNGA Pastor Ibrahim Amasi) na ABC DAR ES SALAAM (SALASALA KINZUDI KWA MTENGA) ANAKOCHUNGA Mchungaji wetu kiongozi Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

Barikiwa.
Ni mimi Victor Tarimo
Nov 17, 2018.

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »