YAH: BUDGET YA KAZI YA INJILI TABORA, WIKI LA PASAKA 2014

[KWA KILA MWANAFUNZI WANGU NA MDAU WA INJILI]

Budget Hii Inahusisha Maeneo Makuu Manne:
1.CHAKULA CHA WATENDAKAZI
2.GHARAMA ZA USAFIRI WA WATENDA KAZI
3.GHARAMA ZA VYOMBO VYA KUHUBIRIA INJILI, VYOMBO VYA KUCHUKULIA KUMBUKUMBU ZA MATUKIO [KAMERA ZA PICHA NA VIDEO] NA VIFAA VYA SINEMA
4.MATIBABU NA DHARURA ZA KIAFYA

1.CHAKULA CHA WATENDAKAZI
Huduma Hii Itahusisha Watenda Kazi 50, Na Itakuwa Ya Siku 6 Yaani Tangu Tarehe 16-21/04/2014.
Tarehe 16 Ni Siku Ya Safari Ya Kuelekea Tabora, Tarehe 21 Ni Siku Ya Kurejea Toka Huko.
Tarehe 17 Hadi 20 Ni Siku 4 Za KUPIGA KAZI HUKO TABORA.
Chakula Cha Mtu Mmoja Kwa Kujibana Ni Sh.5000 Yaani Sh. 1000 Kifungua Kinywa, Sh.2000 Lunch Na Sh.2000 Dinner.
Kwa Watumishi 50 Kwa Siku Moja Ni : 50 x 5000/=[250, 000/=].
Kwa Siku 6 Za Huduma Ni: 6 x 250, 000/= [1,500,000/=].
MAKADIRIO YA GHARAMA YA CHAKULA NI SH. 1.5 MILIONI [Kwa Kubana Hivi]!

2.GHARAMA ZA USAFIRI WA WATENDAKAZI
Gharama Ya Kawaida Ya Kusafiri Kwa Mtu Mmoja Toka Dar Hadi Tabora Ni Kati Ya Sh. 38,000 Hadi 42,000/= Kutegemeana Na Ubora Wa Gari Husika.
Hivyo Tumechukua Wastani Wa Shilingi 40,000/= Kama Gharama Ya Usafiri Wa Mtu Mmoja Toka Dar Hadi Tabora.
Ukiweka Na Kurudi Inakuwa Mara 2 Yake Yaani 80,000/=
Hivyo Kwa Watenda Kazi 50 Kwenda Na Kurudi Inakuwa:
50 x 80, 000/= [4, 000, 000/=]
Lakini Kutokana Na Uzoefu Wa Masuala Haya Ya Huduma Za Umisheni Mikoani; Ukikodi Usafiri Gharama Inakuwa PUNGUFU KIDOGO Kulinganisha Na Kutumia Mabasi.
MAKADIRIO YA GHARAMA YA USAFIRI NI SH. 4 MILIONI

3.GHARAMA ZA VYOMBO VYA KUHUBIRIA INJILI, VYOMBO VYA KUCHUKULIA KUMBUKUMBU ZA MATUKIO [KAMERA ZA PICHA NA VIDEO] NA VIFAA VYA SINEMA
Hapa Kuna Gharama Zifuatazo:
1.Kuna Vifaa Kama Spika, Vyombo Vya Muziki, Nakadhalika Vitahitajika
Hapa Kutakuwa Na Gharama Kukodisha Mahali [Itahitaji Pesa].. Na Hili Kubana Matumizi Vyombo Sehemu Kubwa Vitatoka Hukohuko Tabora
2.Kuna Gharama Za Kuvisafirisha Pia kuvileta Na Kuvirudisha
3.Vifaa Vya Kuchukulia Matukio Na Kutunza Matukio [KAMERA ZA VIDEO NA PICHA]
Hizi Zinahitajika Sana Maana Tutakuwa Na Mikutano Ya Injili Sehemu Kama Tatu KILA SIKU KWA SIKU ZOTE NNE ZA MKUTANO Na Pia Kwenye USHUHUDIAJI WA NYUMBA KWA NYUMBA. [Ni Pesa Itatumika Kuzikodi Kwa Siku Zote Za Huduma].
4.PROJECTOR NA LAPTOPS Kwa Ajili Ya Huduma Ya SINEMA: Tutakuwa Na Huduma Hii Ya Sinema Kwa Siku Zote Za Huduma Na Katika Maeneo 3 Tofauti, Hivyo Tutahitaji PROJECTOR 3 NA LAPTOP 3 [Itahitajika Pesa Hata Kwa kukodisha]
5.Genereta Na Mafuta Ya Genereta Kwenye Maeneo Yasiyokuwa Na Umeme Kwa Ajili Ya MIKUTANO NA SINEMA [inahitajika Pesa Kukodisha Genereta Na Mafuta Kwa Siku Zote Na Kwa Maeneo Yote Matatu]
MAKADIRIO YA HARAKA KWENYE HIKI KIPENGELE KUTOKANA NA MISHENI ZA WATU WENGINE NA ZILE NILIZOWAHI KUTUMIKA NIKIWA CHUO NA KWA HUDUMA BINAFSI; HAIWEZI KUWA CHINI YA MILIONI 2!
[Hakuna Makadirio Ya Tarakimu Moja Kwa Moja Kama Namba 1&2 Kwakuwa Gharama Zinabadilika Na Kuna Mahaliengine Yanaweza Kupatikana Bure]
MAKADIRIO YASIYO NA TARAKIMU NI MILIONI 2 [kwa kubana]!

4.MATIBABU NA DHARURA ZA KIAFYA
Tunakwenda Kwenye Kazi Ya Mungu Na Hatuamini Kwenye Magonjwa Lakini Maswala Ya Kiafya Ni Imani Ya Mtu Mmoja mmoja Zaidi. Hivyo Huwezi Kuendesha Kundi Kwa Imani Yako Binafsi. Maana Imeandikwa, “MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI YAKE MWENYEWE” (Habakuki 2:4).
Hivyo Tumeweka Budget Pia Kwa Ajili Ya TAHADHARI NA MATIBABU Ikitokea Mtendakazi Au Watendakazi Wakapata Dharura.
Kiwango Tulichoweka Ni Sh. 10,000/= Kwa Kila Mtendakazi.
Hivyo Kwa Wote Ni: 50 x 10,000/= [500, 000/=]!
MAKADIRIO YA GHARAMA ZA MATIBABU NA AFYA NI 0.5 MILIONI.

JUMLA KUU YA BUDGET:
1.CHAKULA : 1.5 MILIONI
2.USAFIRI : 4 MILIONI
3.VIFAA : 2 MILIONI
4.AFYA : 0.5 MILIONI
JUMLA YA MAKADIRIO NI MILIONI 7

Mimi Sina Mdhamini Au Mtu Wa Kuifanya Hii Mission Iwezekane Isipokuwa Mungu. Na Mungu Atakutumia Wewe Kui-support Kazi Yake Ya Injili Kwa Hicho Kidogo Alichoweka Mikononi Mwangu Na Kwako.
Huu Ni Mwezi Februali, Na Pia Kuna Machi Pia, Kama Una Uchungu Na Roho Za Watu, “MUNGU ATAKUPA CHA KUTOA” (2Kor 9:10).

Usiache Kutuma Sadaka Yako Kwa Ajili Ya Huduma Ya Injili Pasaka Mkoani Tabora, Tutakuwa Na Timu Ya Wainjilisti 50, Na Itakuwa Kwa Siku 6, Tunahitaji Sana SADAKA YAKO, TABORA KWA YESU.
Tuma Kwa Mhazini, Eng Martha Shitindi [M-PESA: 0754 711 519]

Kwa Ushauri, Maoni, Mapendekezo, Maswali Au Lolote Kuhusu Huduma Hii, Wasiliana Nami:
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675 — with Agatha Mwangaba and 19 others

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »