HOW TO BE GREAT THROUGH CONSISTENCY IN PRAYERS

Andiko la msingi:
Danieli 6:10
“Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Daniel alikuwa na uwekezaji wa maombi kiasi kwamba aliposikia amri imetolewa aliendelea kuomba na kuwa jasiri.”

Kila mtu kama alivyokuwa anaomba Danieli anapaswa kufanya uwekezaji wa maombi.
Zaburi 32:6 Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.

Waefeso 5:15-16 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Kuna watu wanalala usingizi rohoni. Kama mtu hawezi kuomba lisaa 1 bila kuacha ameshalala rohoni.
Kama mtu akilala rohoni hawezi kuona kwa macho ya nje.

Ufunuo wa Yohana 3:18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Mungu anayeichunguza mioyo anaweza kuifunua mioyo ya watu kwako ili usiangukie kwenye trap.
Yeremia 17:9-10 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

Kumcha Mungu kunaongeza ufahamu wa Mtu.
Mithali 1:7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Zaburi 111:10 Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.
Kuna ufahamu ambao mtu anaupata kwa kumcha Bwana tu na sio elimu nyingine yoyote.

Mungu anayeinua watu anataka kila mtu awe mwaminifu kwa madogo na makubwa pia.
Luka 16:10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.

MAANDIKO MUHIMU:

 1. 1 Mambo ya Nyakati 4:9-10
  Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
  Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Yabesi alibadilisha maisha yake kwa maombi. Mungu anaweza kukupa yote unayoyahitaji as much as unayaomba

 1. Yakobo 4:2
  Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
  Ni aibu kukosa vitu kwa sababu tu hauombi.
 2. Yohana 16:23-24
  Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

Yesu alitoa ofa ya kuomba lolote kwa Jina lake ili tupewe.

 1. Luka 18:1
  Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
  Kila mwombaji anapaswa kuomba siku zote bila kukata tamaa.
  Kila mwombaji anafaa awe king’ang’anizi.
 2. Matendo ya Mitume 10:1-3
  Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!

Kornelio alimuomba Mungu daima.
Mbinguni wanaweka akiba ya maombi na sadaka. Kila mwombaji anapoendelea na maisha ya maombi anaanza kuwekewa rekodi mbinguni.


Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
31.01.2024

WhatsApp: 0655 466 675
Youtube: Pastor Dickson Kabigumila
Facebook: Dickson Cornel Kabigumila (iko verified na blue tick)
Instagram: @pastorkabigumila (iko verified na blue tick)
Tiktok: @kabigumila

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »