MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12-MAY [SIKU YA 3]

NGUVU YA KUUMBA MEMA TOKANA NA MABAYA NA MAGUMU YANAYOTUZUNGUKA

(THE POWER TO CREATE GOOD THINGS OUT OF BAD AND TOUGH SITUATIONS AROUND US).

Vijana watatu wakisimama eneo la jaani

Maandiko:

“Nayo NCHI ILIKUWA UKIWA, TENA UTUPU, NA GIZA LILIKUWA JUU YA USO WA VILINDI VYA MAJI; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu AKASEMA, IWE NURU; IKAWA NURU…”
(Mwanzo 1:1-31).

“Naye akawaambia, KATIKA HUYO MWENYE KULA KIKATOKA CHAKULA, KATIKA HUYO MWENYE NGUVU UKATOKA UTAMU”
(Waamuzi 14:14).

“Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, walikuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, NCHI ILE TULIYOPITA KATIKATI YAKE ILI KUIPELELEZA, NI NCHI NJEMA MNO YA AJABU. Ikiwa BWANA anatufurahia, ATATUINGIZA KATIKA NCHI HII ATUPE IWE YETU, NAYO NI NCHI YENYE WINGI WA MAZIWA NA ASALI. Lakini msimwasi Bwana, wala kuwaogopa wale wenyeji wa nchi, MAANA WAO NI CHAKULA KWETU; Uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, NAYE BWANA YU PAMOJA NASI; MSIWAOGOPE”
(Hesabu 14:6-9).

Mambo ya kujifunza:

i) Kila hali mbaya au ngumu inaweza kubadilika kama Mungu atapewa nafasi.

ii) Kila hali mbaya au ngumu inaweza kubadilika iwapo mwenye nayo ATABADILI MTAZAMO na kufikiri kuhusu suluhisho badala ya tatizo.

iii) Hali mbaya na ngumu inaweza kubadilika endapo mhusika ATAONGEA LUGHA YA IMANI BADALA YA LUGHA YA TATIZO ANALOPITIA!

iv) Hali mbaya na ngumu inaweza kubadilika iwapo mhusika ATACHUKUA HATUA PAMOJA NA ROHO MTAKATIFU kuikabili badala ya kuikimbia.

BAADHI YA HALI MBAYA NA NGUMU ZILIZOBADILIKA;

i) -Ukiwa kuwa utele kwa Neno la Mungu wakati wa Uumbaji.
-Giza kuwa nuru kwa Neno la Mungu wakati wa uumbaji
-Utupu uliokuwa juu ya nchi kuwa wingi kwa Neno la Mungu wakati wa uumbaji.

ii) Utasa wa (tumbo lililokufa la) Sara kugeuka Isaka

iii) Huonevu wa mwajiri Labani kugeuka UTAJIRI kwa mfanyakazi Yakobo baada ya miaka 14 ya kubadilishiwa mshahara mara 10.

iv) Mtumwa aliyesingiziwa ubakaji Yusufu kuwa Waziri mkuu Misri, na kuiponya nyumba ya baba yake isife njaa na kuleta wokovu wa dunia yake isife kwa njaa.

iv) Mwebrania Musa kukulia kwenye ikulu ya Farao badala ya kuuwawa kama watoto wengine wa kiume, huku mama yake akilipwa mshahara kwa kumnyonyesha mwanae!

v) Jua kusimama kwa amri ya mwanadamu Yoshua ili awapige na kuwamaliza Amaleki.

vi) Bahari ya Shami kugeuka lami kwa fimbo ya Musa badala ya kizuizi na kutumika kama silaha ya kuwameza maadui waliodhani wamewapata maana hawana pa kupenya.

vii) Mchunga kondoo Daudi kumuua askari mkongwe wa vita na jitu aitwaye Goliati.

viii) Wanawake wasio na asili ya Uisraeli ndani yao lakini WENYE IMANI Rahabu na Rutu kuingia kwenye orodha ya Yesu na kuwaacha wanawake waliodhaniwa wana vigezo zaidi yao wakiwa hawatajwi kabisa.
HAYA NI BAADHI YA MEMA YALIYOTOKEA MAHALI AMBAPO ULIONEKANA UBAYA NA UGUMU, BIBLIA IMEJAA MATUKIO MENGI YA NAMNA HII… JIKUMBUSHE ILI KUPANUA IMANI YAKO!

MAOMBI:

Asubuhi

1. Muombe Mungu akubadili moyo uachane na lugha ya HAIWEZEKANI maana pamoja na Mungu kila kitu kinawezekana.
(Marko 10:27, Yeremia 32:17,27).

2. Muombe Mungu abadili mawazo na maneno yako ili yapate kibali mbele zake na yatumike kubadili hali ngumu na mbaya badala ya kujenga ngome za hayo mambo kwa maneno yetu.
(Zaburi 19:14, Mathayo 12:34-37).

Mchana

1. Omba nguvu ya Mungu iukamate moyo wako usiogope Habari mbaya bali moyo wako ujawe na ujasiri wa kugeuza chochote.
(Zaburi 112:6-7, Hesabu 14:6-9b).

2. Omba Mungu auimarishe ushirika wako na Roho Mtakatifu maana kwa msaada wake tu ndipo unaweza kutenda makuu.
(Zaburi 60:12, Zaburi 18:25-32).

Jioni

1. Omba lolote unalotaka Yesu akutendee.
(Mathayo 8:1-5, Hosea 6:4).

2. Niombee mimi Mwl Dickson Cornel Kabigumila, Mungu aniimarishe katika kazi yake aliyonipa.
(Isaya 52:13, Zaburi 89:20-29).

3. Mshukuru Mungu kwa kujibu maombi yote.
(Marko 11:24, 1Yohana 5:14).

Tukutane kesho Jumamosi SIKU ya NNE,
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.

USIACHE KUTEMBELEA:
www.yesunibwana.co.tz

NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU, AMBAYO UNAGUSWA MOYONI, ITATOLEWA MWISHO WA MFUNGO

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »