About Us

Dickson Cornel Kabigumila ni mwalimu wa Neno la Mungu. Amekuwa akifundisha katika mashule, vyuo, makanisa na fellowship za Kikristo. Amekuwa akifundisha katika ibada, semina na makongamano mbalimbali ya kiroho kwa takribani miaka 5 sasa. Alimpokea Yesu kama Bwana na mwokozi binafsi wa maisha yake mwaka 2003 na kujazwa na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu sawa na isemavyo Matendo ya Mitume 10:38. Na amefanya kazi na mashirika na huduma mbalimbali za Kikristo kama vile TAFES, CASFETA, HUIMA, UKWATA na CHARISMATIC. Pamoja na huduma mbalimbali zinazoujenga mwili wa Kristo hapa Tanzania kama vile, MANA iliyo chini ya Mwl. Christopher Mwakasege, ambaye Mwl. Dickson hasiti kukiri kwamba amekuwa baba kwake na kwa kanisa la Tanzania, pia amefanya kazi na The Life Ministry, New Life in Christ na huduma ya kuwafikia wasiofikiwa kwa injili ya GKB. Na amewahi kuwa kiongozi wa Fellowship ya wanafunzi Wakristo wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, katika nafasi ya Mratibu wa maombi na pia kama Mwenyekiti. Na kwa neema ya Mungu, yeye ndiye mwanzilishi wa kipindi cha Mafundisho na uchambuzi wa Biblia katika siku za Jumatatu na Jumatano. Amezaliwa mwaka 1989, katika kijiji cha Chabuhora, kata ya Nyakakika, tarafa ya Nyabiyonza, Wilaya ya Karagwe, mkoa wa Kagera. Ni mtoto wa sita katika familia ya ndugu nane. Akiwa na dada zake watano na kaka wawili. Kwa kifupi huyu ndiye Mwl. Dickson Cornel Kabigumila…KARIBU.

4 thoughts on “About”

  1. Mwl Dickson Bw Yesu asifiwe! Mungu aibariki zaidi karama aliyokupa na kuikuza zaidi ili watu wote wa Mungu watambue kuwa hakika, YESU NI BWANA.

  2. Alex Emmanuel Bubelwa

    Ubarikiwe sana Mwalimu, nilivyokuwa naona mafundisho ya nguvu kwenye Facebook sikutarajia kama ungekuwa na umri kama huu! Bwana na azidi kukuinua.

  3. mwl Dick mimi ni jane nimepotezacm tangu tare18/1/2015———— leo naomba maombi yenu namba mpya ni 0758xxxxxx ya zamani ni0718xxxxxx napia naombA YAKO BARIKIWA (message modified by Admin for Privacy purpose)

Comments are closed.