FUMBO LIITWALO WATU (The mystery called men)

IBADA KUU YA JUMAPILI ABC GLOBAL KINZUDI HQ.

MWAKA 2024:MWAKA WA MAMBO MAKUU YASIYOCHUNGUZIKA WALA KUTAMBULIKANA NA MAAJABU YASIYOHESABIKA.

SOMO: FUMBO LIITWALO WATU (The mystery called men)

MHUDUMU: ASK. DICKSON C KABIGUMILA.

Zaburi 105:17 Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.

(He sent a man before them, even Joseph, who was sold for a servant)

Kesho haipo mbinguni ila ipo mikononi mwa mtu aliyetangulizwa na Mungu mbele yako. Hakuna bahati mbaya.

Maisha ni mepesi kama ukijua hii kanuni.

Mungu alimtanguliza Yusufu ili kuokoka taifa zima na njaa.

Siyo lazima kesho uinunue kwa hela. Unaweza kuinunua kwa kujua jinsi Mungu anavyofanya kazi. Wana wa Israeli walipoenda kununua chakula Misri walirudishiwa hela zao kwenye mifuko yao. (You can buy without money)

Kwenye kila hatua ya maisha ,kuna mtu amepewa majibu ya kesho yako ili uweze kuwa na ufanisi na kutimiza kusudi kwa urahisi.

Zaburi 2:8 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

Watu ndio urithi wa kumuomba Mungu. Mungu akikupa watu amekupa urithi mzuri.

Lazaro maskini alikuwa mtu wa rohoni lakini hakuwa na watu,akajishusha kula na mbwa.

Mithali 14:28 Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.

Unapokuwa na watu wengi umefanikiwa tofauti na ukiwa na watu wachache.

Kipimo kwamba Mungu anakuthamini anakupa watu. Thamani ikipanda Mungu anakupa watu.

Mungu akikuheshimu anakupa watu.

Mungu akikupenda anakupa watu.

Isaya 43:4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.

Maisha ya mtu yameamuliwa yawe served na makabila tofauti tofauti. Mungu ndiye aliyeanzisha kununua watu wa kila kabila, kila lugha, kila jamaa. (Ufunuo 5:9-10) ndivo hivyo anafanya kwa watoto wake.

Waebrania 13:2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.

Watu wanaweza kuwa wamepewa maagizo ya kukusaidia ila wakawa na sababu zao binafsi.

1 Wafalme 17:8-9 Neno la Bwana likamjia, kusema,

Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.

Mungu anaweza kutumia mtu asiyefanania kuinua maisha yako. Mama aliyepewa maagizo ya kumlisha Eliya nabii alikuwa mjane, tena anaokota kuni.

Aliyekuwa na mlo mmoja alimlisha nabii miaka 3 na nusu.

Mbinguni wanajua njia ya kumtoa mtu kwenye umaskini ni utoaji.

๐Ÿ“Œ Chochote kisichotosha kumaliza matatizo yako ni mbegu sio chakula. ๐Ÿ“Œ

Kwa nini tunahitaji watu?

1. Utajiri wetu na ustawi wa kiuchumi upo kwa watu.

Sehemu ya utajiri alionao Mungu ni watu.

Zaburi 24:1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Kila mahali penye neno la Bwana pana uwezo wa Bwana.

Luka 5:17

Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.

Watu wanawapa watu vitu wale ambao sehemu ya Mungu imewaangukia.

Watu walikuwa wanaenda kumwabudu Mungu na kumtolea dhabihu lakini sehemu ya dhabihu walimpa Sauli aliyepakwa mafuta.

1 Samweli 10:2-4 (KJV) Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?

Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; *nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao.*

๐Ÿ“Œ ISAYA 60:1-11.

Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Kila anayetaka ku flow kwenye miujiza ya kiuchumi hapaswi kuwa bahili. Wape watu mdai Mungu.

Mungu haruhusiwi kuweka vitu mahali pasipo na uwazi. Lazima uwape watu ili ubakie na nafasi ya kupokea kutoka kwa Mungu.

Mithali 11:24

Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.

___________________________________

Askofu Dickson Cornel Kabigumila

ABC GLOBAL DUNIANI

28.01.2024

WhatsApp: 0655 466 675

Youtube: Pastor Dickson Kabigumila

Facebook: Dickson Cornel Kabigumila (iko verified na blue tick)

Instagram: @pastorkabigumila (iko verified na blue tick)

Tiktok: @kabigumila

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More ยป

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More ยป

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More ยป