HAKUNA ASIYE NA UWEZO NDANI YAKE

HAKUNA ASIYE NA UWEZO NDANI YAKE

KISA CHA MWAMUZI GIDEONI, WAAMUZI 6:10-15

1. Tatizo ni kuaminishwa kwamba uwezo wa kugeuza maisha yetu unatokea nje yetu badala ya kuanza na uwezo ndani yetu kwanza! Gideoni aliangalia kote isipokuwa ndani yake…

2. Uwezo ulioko ndani ya mtu hauna msaada kama hatautambua na kuanzia hapo na alichonacho kwenda anapopatamani! Alichobeba Gideoni kilikuwa jibu la taifa zima lakini hakuwa na maisha yanayofanana na uwezo huo…

3. Uwezo ulioko ndani ya mtu umewekwa na Mungu tangu anaumbwa ili alete utofauti kwenye dunia yake, lakini kuna wakati unahitaji mtu wa nje akuambie ulichobeba kama vile Gideon alivyohitaji malaika kumuambia ana kitu tayari!

4. Unaweza kuwa na uwezo mkubwa mno lakini ukawa unaishi maisha ya chini mno kwa sababu tu hujui umuhimu na ukubwa wa ulichobeba kama ilivyokuwa kwa Gideoni

5. Unaweza kuwa na uwezo mkubwa unaoweza kulisaidia taifa zima litoke utumwani lakini usipojua hilo, utaishi chini ya kiwango halisi cha maisha yako kama Gideoni!

6. Kuna wakati unahitaji Neno kutoka kwa Mungu ili ulichobeba kiamke na kuanza kufanya kazi! Hakikisha unasikiliza na kufuatilia watu ambao wakisema kitu unasikia simba aliyeko ndani yako ameamka!

7. Aina ya familia uliyotoka na hali yake mbaya inaweza kufunga ufahamu wako usione uwezo mkubwa ulionao! Hiki kilimuathiri mno Gideoni…

Askofu Dickson Cornel Kabigumila

ABC GLOBAL DUNIANI

06.03.2024

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »