MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 5]- JULAI 2019

MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI ALIZOTUPA MUNGU ZILIZOTUZUNGUKA/ ZILIZO KWENYE MAZINGIRA YETU

Utangulizi

Jana tumepata muda wa KUOMBA kwa ajili ya hazina alizowekeza Mungu ndani yetu, ili Mungu atupe hekima na UPAKO maalum wa kuzitumia kwa faida katika miezi yetu sita ijayo ya mwisho wa Mwaka!

Hazina hizo zina nafasi kubwa ya kuamua ufanisi wetu si tu katika miezi yetu sita ijayo ya mwisho wa mwaka bali maisha yetu yote hapa duniani!

Naamini ulipata muda wa kuzipitia kwa kina na kuomba kwa zote kwa mujibu wa muongozo aliotupa Roho Mtakatifu.

Baada ya hazina tulizonazo alizowekeza Mungu ndani yetu, leo tutajifunza na kuombea RASILIMALI ZILIZO KWENYE MAZINGIRA YETU ambazo kama tukizitumia vizuri zitatufanikisha kwa miezi sita ijayo na maisha yetu hapa duniani!

Rasilimali hizo zilizotuzunguka, zinaweza kubadili maisha ya kila mmoja wetu kama akizitambua na kuzitumia kwa usahihi.
Rasilimali hizo ni;

1. Muda
Waefeso 5:14-16, Mhubiri 3:1

2. Watu
Isaya 43:3-4, Isaya 60:1-4, 10, Mithali 14:28, Luka 6:38

3. Pesa
Mhubiri 10:19, 1Timotheo 6:6-17

4. Fursa
2Wafalme 7:3-9, Mhubiri 9:11, 1Wakorintho 16:9

MAMBO YA KUOMBEA

ASUBUHI

*”Huku tukikomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu…”*
(Waefeso 5:14-17)

OMBA
-Mungu akusaidie kuwekeza muda wako badala ya kuuchezea na kuutumia vibaya

-Muombe Mungu akusaidie kuwa na moyo wa hekima, utakaokusaidia kuhesabu siku moja moja ya maisha yako na kuitumia kwa busara (Zaburi 90:12).

-Muombe Mungu akupe neema na upako utakaokusaidia kujua mambo yakupasayo kufanya ili ustawi katika maisha kama ilivyokuwa kwa wana wa Isakari (1Nyakati 12:32).

MCHANA

*”UTUKUFU WA MFALME NI WINGI WA WATU WAKE…”*
(Mithali 14:28).

OMBA

– Omba Mungu akupe watu wa kutosha kwenye kila eneo la maisha yako, watakaorahisisha maisha yako na kukupeleka mahali pa ustawi kwa miezi sita ijayo!

-Omba Mungu akupe mlango wa kugusa na kubariki maisha ya wengine, ili na wao waje waguse na kubariki maisha yako (Luka 6:38).

-Muombe Mungu akupe watu sahihi ambao watayabariki maisha yako (Isaya 43:3-4).

-Muombe Mungu akusaidie kuwa na amani na kila mtu ambaye hauelewani naye sasa (Waebrania 12:14).

-Omba Mungu akupe watu sahihi ambao watakuwa baraka kwako kwa miezi sita ijayo (Zaburi 2:8).

JIONI

*”…Fedha huleta jawabu la mambo yote…”* (Mhubiri 10:19).

-Muombe Mungu akusaidie kuheshimu kila fedha inayopita mikononi mwako, usiifuje au kuitumia nje ya malengo yako na ya huduma!

-Muombe Mungu akusaidie, upate miradi itakayokusaidia kuzalisha fedha zaidi.

*”…BAHATI NA WAKATI (FURSA) huwapata watu wote…”* (Mhubiri 9:11).

-Muombe Mungu akusaidie uwe tayari pale Fursa zitakapokuwa zinajitokeza, uzifaidi!

-Muombe Mungu ayafungue macho ya moyo wako kuona kila fursa ambayo wengine hawaioni (Waefeso 1:16-17).

-Muombe Mungu akupatie hekima ya KUTUMIA kila fursa uliyonayo kwenye maisha yako (Yakobo 1:5-7).

HONGERA KWA USHINDI NA HATUA ZA USHINDI,
WEWE NI MTU WA BARAKA KWA DUNIA YAKO,
UMEBEBA MASULUHISHO YA WENGI.

TUKUTANE KESHO SIKU YA SITA YA MFUNGO WETU,
USIKUBALI KUISHIA NJIANI, FUNGA SIKU ZOTE 10 KWA UAMINIFU.

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila.
26/07/2019

NB: *USIACHE KUMUOMBA MUNGU AKUSAIDIE KUPATA NA KUANDAA SADAKA NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU WA MIEZI SITA YA MWISHO WA MWAKA! SADAKA ITATOLEWA SIKU YA MWISHO YA MFUNGO.*

Mawasiliano zaidi:
Tovuti: www.yesunibwana.co.tz
WhatsApp: 0655 466 675
Instagram: @mwalimukabigumila

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »