SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA

Luka 16:10
[10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.

Mambo ya kujua kuhusu
Tendo la Ndoa kabla ya Ndoa
kwa anayetaka na anayefanya.

1. Wewe Sio #Mwaminifu
( Na Kama Umekuwa Dhalimu kwa jambo Dogo kama Mahusiano, Ujue utakuwa DHALIMU hivyo hivyo kwenye Ndoa )

2. Hauna #Upendo wa Mungu.
( Kwanini umeshindwa kuvumilia mwaka mmoja au miwili au mitatu)
1 Wakorintho 13:4-6
[4]Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
[5]haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
[6]haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

3. Unateswa na #Tamaa ya Mwili + Macho
( Kwahiyo Mtu anayetaka sana tendo la Ndoa usifikiri anataka upendo, ujue Leo kuwa anateswa na TAMAA )
1 Yohana 2:15-17
[15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
[16]Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
[17]Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

4. Hatendi #Mapenzi ya Mungu.
( Kwahiyo yeye hatadumu Kiroho, kiafya na Kimwili na Mahusiano yenu hayatadumu )

1 Yohana 2:17
[17]Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

huyu anayetaka tendo la Ndoa kabla ya NDOA tayari ni Mfu.

Yakobo 1:15
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

5. Anayetaka Tendo la NDOA kabla ya Ndoa, Sio #muoaji ni muharibifu.

Ndio maana Limeitwa Tendo la Ndoa
sasa kwanini analihitaji kabla ya Ndoa
maana yake sio mwaminifu, sio muoaji, no mchezaji.

6. Hana #Maono
Kama hawezi kutunza mwili wake na anashindwa kujizuia UJUE HANA MAONO

Mithali 29:18
[18]Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

Mtu anayetaka kufa kwa nguvu Anatoa wapi maono, Mtu anataka kuharibu mahusiano yake na Mungu, anatoa wapi maono.

Dada – Mkaka anakuomba ulale naye
ujue unawasiliana na kipofu.

7. Amepungukiwa na #AKILI tayari

Sasa unapoona mkaka anataka mlale kabla ya Ndoa, Ujue unawasiliana na Mtu aliyeanza kuchizika ( Ni kichaa, kwasababu hana akili kabisa )

Mithali 6:32
[32]Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

8. Yuko #Gizani

Kipofu akimuongoza kipofu mwenzake LAZIMA WAFIE SHIMONI.

Mathayo 15:14
[14]Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

9. Ni Ishara ya Kwanza kabisa
kwamba hamtakuwa waaminifu kwenye Ndoa

UTAZINIJE SASA
BAADA YA KUJUA HII KWELI

“ ukifanya hivyo baada ya kujua kweli utakuwa unafanya dhambi kinyume na Mungu ”

WEWE AMBAYE ULISHAANZA
na unataka msaada
nitafute kwa namba 0763706469

Ninajua Mtizamo wako UMEBADILIKA sasa
Mungu akubariki

*Pastor Ibrahim Amasi*
ABC-KAHAMA
0763 706469

LivingWord
@2019

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »