MFUNGO WA SIKU 10 WA MWISHO WA MWEZI TATU

(22/03/2019-31/03/2019).

NA MWALIMU NA MCHUNGAJI DICKSON CORNEL KABIGUMILA,

DAY 1, 22/03/2019

NGUVU YA UTAKATIFU

“Watakatifu WALIOKO DUNIANI hao ndio walio bora, ndio niliopendezwa nao”
(Zaburi 16:3).

“Bali kama Yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE. Kwa maana imeandikwa MTAKUWA WATAKATIFU KWAKUWA MIMI NI MTAKATIFU”
(1Petro 1:15-16).

” Lakini uasherati usitajwe kwenu KAMWE wala uchafu wowote wa kutamani, kama IWASTAHILIVYO WATAKATIFU”
(Waefeso 5:3).

“Kama vile alivyotuchagua katika Yeye kabla misinginya ulimwengu kuwekwa, ILI TUWE WATAKATIFU, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo”
(Waefeso 1:4).

Mambo ya kuzingatia:

1. Kuokoka ni kuingizwa kwenye FAMILIA TAKATIFU YA WATAKATIFU ambayo iko chini ya MUNGU MTAKATIFU ambayo UTAKATIFU NI MFUMO WA KAWAIDA WA MAISHA (1Petro 2:9, Waefeso 2:19, Wakolosai 3:12), hivyo KUISHI MAISHA MATAKATIFU unapaswa usiwe mzigo mzito kwako.
Kinapaswa kiwe kitu cha kawaida kabisa.

ASUBUHI
•Omba MUNGU AKUSAIDIE KUTEMBEA KATIKA UTAKATIFU kwa wepesi kama mtakatifu katika familia ya mbinguni.

•Kila tabia inayokuzuia kutembea katika utakatifu kama mwana wa Mungu, ipeleke mbele za Mungu na kuomba neema ya kuishinda

•Omba mbele za Mungu, akupe neema ya kuweza kutawala mambo unayosikia na unayotazama, maana hivyo ndivyo vinavyoathiri uwezo wako wa kuishi maisha matakatifu.

•Ombea moyo wako ujue na kukubali kuishi maisha matakatifu kama mfumo wako wa maisha (lifestyle) maana wewe ni sehemu ya TAIFA TAKATIFU ndani ya Kristo (1Petro 2:9).

•Omba uwezo na nguvu ya kutotenda dhambi maana uzao wa Mungu unakaa ndani yako, bali muombe Roho Mtakatifu akupe nguvu ya kujilinda dhidi ya mitego yote ya dhambi iliyoko hapa ulimwenguni (1Yohana 5:18-19).

2. Ni mapenzi ya Mungu TUWE WATAKATIFU kama Yeye Mungu alivyo; na anatuhimiza kuwa kama Yeye (1Petro 1:15-16), Mungu HAWEZI kutuambia tufanye au tuwe kitu ambacho hakiwezekani!!!!!

Hivyo ndani ya KILA ALIYEOKOKA kuna MBEGU YA UTAKATIFU ambayo, UNAHITAJI KUJITAMBUA UNAYO kisha mruhusu ROHO MTAKATIFU AIFUNUE NJE ULIMWENGU UIONE (Warumi 8:14,16,19).

•Omba Roho mtakatifu aikuze MBEGU YA UTAKATIFU iliyomo ndani yako, ifike mahali pa kuishi maisha matakatifu BILA KUTUMIA NGUVU AU KUJILAZIMISHA (Utakatifu uwe kitu cha kawaida kama kupumua au kuona njaa ilivyo kitu cha kawaida)!
•Mungu aliyetuita ni mtakatifu na wala ha-struggle kuwa Mtakatifu, anaishi UTAKATIFU kama mfumo wake wa kawaida wa maisha, Muombe akupe nguvu na uwezo wa kuishi maisha ya UTAKATIFU bila kutumia nguvu au kujiumiza, iwe ni automatic kama ambavyo Yeye Mungu hasumbuki kuwa mtakatifu (1Petro 1:15-16, Mathayo 5:48).

•Muombe Mungu AKUPE NGUVU YA KUJIEPUSHA NA UOVU ambayo watu wengi wanakosa; Nguvu hii itakufanya uishi maisha matakatifu kwa urahisi.
(1Yohana 5:18, Ayubu 1:1,8, Ayubu 2:3, Mithali 8:13).
Ayubu alikuwa na nguvu hii ya kujiepusha na uovu (Ayubu 1:1,8, Ayubu 2:3).
-Suleiman na watakatifu wa kizazi chake walikuwa na nguvu ya kujiepusha na uovu (Mithali 8:13),
-Watakatifu wa kizazi cha Yohana kipenzi cha Yesu (John the beloved), walikuwa na NGUVU YA KUJILINDA ili wasitende dhambi! Dhambi ilikuwepo na ulimwengu wote wa kizazi chao ulijaa dhambi na uovu (1Yohana 5:19) lakini wao walikuwa na nguvu ya KUJILINDA (KUEPUKA) NA KUTOTENDA DHAMBI (1Yohana 5:18).
•Iombe nguvu hii ya kuepuka uovu wa kila namna!
•Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kuona uovu na dhambi hata kabla haijawa dhahiri na akupe nguvu ya kutoitenda.

“Utakatifu unaanza pale unapojielewa wewe si kama wengine walioko nje ya Yesu. Umeingizwa kwenye Ufalme Mtakatifu wa Mungu mtakatifu, na kuishi maisha matakatifu ni wajibu wetu na si kujaribu kujitetea au kushusha viwango vyetu kwa chochote. Ukishadaka hiyo, Roho wa Mungu ataingia kazini KUKUTIA NGUVU uweze kuishi katika njia hiyo bila shaka, na udumu ndani ya Kristo.”

MFUNGO WA SIKU 10.

DAY 1

MCHANA

•Muombe Mungu akuumbie moyo safi na roho iliyotulia ndani yako (Zaburi 51:10).

•Omba Mungu akupe moyo wa nyama, na akuondolee moyo wa jiwe (Ezekieli 11:19, Ezekieli 36:26).

JIONI

• Omba nguvu na neema ya kuwa shahidi wa Yesu na kuutunza ushuhuda wake kila iitwapo leo.
(Matendo 1:8, Waebrania 4:16, 2Kor 3:1-3).

• Omba nuru kutoka kwa Bwana itakayokutenga na matendo yote ya giza yasiyofaa.
(Isaya 60:1-3, Mathayo 5:13-16, Yohana 9:5).

NB: Niombee mimi mchungaji Dickson, mke wangu Mercy, na kanisa la ABC, tuwe vielelezo kwa waaminio na hata wasioamini katika usemi (lugha yetu), imani, usafi, upendo, mwenendo wetu, tukae katika hayo siku zote ili kuendelea kwetu binafsi na kazi yake ya ABC viwe dhahiri. Mungu atusaidie kujitunza sisi na mafundisho yetu ili tuokolewe sisi na wale watusikiao pia (1Timotheo 4:12-16).

Umebarikiwa sana mwana wa Mungu, hongera kwa kukubali kufunga siku hizi kumi na sisi kila mwezi!

Tukutane kesho siku ya pili,
Pst. Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji kiongozi,
Assembly Of Believers Church ( ABC),
22/03/2019

 

Baki na sisi kwa Kusoma nyaraka nyingine kama

Picha na Video za Uchi na Ngono ,Namna ya kushinda (Muhimu Sana kwa Kijana)

MFUNGO WA SIKU 10 WA MWISHO WA MWEZI. MASAA 12 KUTWA. FEBRUARI 19-28/2019.

Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »