NGUVU ZA MUNGU
Zaburi 105:4
“Mtakeni Bwana na NGUVU ZAKE; utafuteni uso wake siku zote”
Kwenye andiko hili la msingi tunayaona mambo kadhaa;
1. Kuna uhusiano wa moja kwa moja na kumtafuta Mungu kila siku na kiwango cha nguvu zake utakachotembea nacho.
-UKIWA na consistency (muendelezo) wa ushirika na Mungu, utakuwa mtu mwenye nguvu za Mungu wakati wote, na UTAKUWA ukijazwa nguvu zake kila iitwapo leo, Bali UKIWA mtu wa mara moja moja, utakuwa na UPAKO wa msimu tu!
2. Nguvu za Mungu hazikunyeshei kama mvua au kukuangukia kama jua; Ni mpaka UZITAKE NA KUZITAFUTA!
Watu wote tuna haki sawa MBELE ZA MUNGU katika Kristo Yesu lakini ni wale tu walioamua KULIPA GHARAMA YA KUZITAFUTA NA KUZITAKA NGUVU ZA MUNGU ndio wanatembea katika UPAKO MKUBWA maishani mwao!
3. Hauwezi kutafuta nguvu za Bwana na usikutane na Bwana kwanza; Hivyo unavyotafuta nguvu za Mungu itakufanya umsogelee na kuwa karibu na Mungu, inakuza mahusiano na ushirika wako na Mungu.
HAKUNA MTU MWENYE KUWEKEZA KUTAFUTA NGUVU ZA MUNGU AMBAYE MAHUSIANO YAKE NA MUNGU YATAKUWA YA KUSUASUA, AUTOMATIC UTAJIKUTA UNAKUA MNO KIROHO PIA!
4. Ukilisoma hilo andiko unaona kuna neno NGUVU ZAKE ikiwa na maana Mungu ana nguvu zaidi ya moja (ana nguvu za aina mbalimbali).
Waefeso 6:10
“Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika UWEZA WA NGUVU ZAKE”
Hapa tunapata yafuatayo;
1. Biblia haituruhusu kuridhika na kiwango cha nguvu za Mungu; Inatutaka TUZIDI KUWA HODARI katika nguvu za Mungu.
Ukiona mtu anafurahia nguvu ya Mungu kidogo aliyonayo na hakazani kufika kwenye kimo, urefu, upana na kina cha Kristo, ujue huyu mtu amefilisika.
2. Tunaendelea kuona waziwazi kuwa UNAANZA NA BWANA halafu ndipo Uweza wa nguvu zake unaachiliwa juu yake.
Hii ina maana wote watafutao nguvu za Mungu, wana nafasi ya kukutana na Mungu na ukikutana na Mungu maisha yako yamegeuka.
AINA ZA NGUVU ZA MUNGU.
1. Nguvu za kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu (Matendo 1:8, Matendo 4:33).
2. Nguvu za uponyaji.
(Marko 5:28-30, Isaya 50:2).
3. Nguvu za Roho mtakatifu za kuzaa vitu vya kiungu tulivyobeba (Luka 1:35).
4. Nguvu za rohoni.
(Luka 1:80, Luka 4:14)
5. Nguvu za kutoa pepo (Luka 4:36, Luka 9:1, Luka 10:19).
6. Nguvu ya kuharibu kila vifungo na kamba za kuzimu (Luka 4:18, Isaya 10:27).
7. Nguvu ya kulinda vitu na mambo anayotupa Mungu.
(Luka 11:21).
8. Nguvu ya kuanza vitu na kuvimaliza.
(Luka 14:30, Wafilipi 1:6).
9. Nguvu ya kuzaa vitu na kuacha alama duniani.
(Isaya 26:17-18, Isaya 37:3,31).
10. Nguvu za kupata utajiri.
(Kumbukumbu 8:18, Warumi 10:12, Mithali 8:17-20).
11. Nguvu za jina la Yesu.
(Matendo 3:16, Wafilipi 2:9-11).
12. Nguvu za kufanya ishara, maajabu na miujiza.
(Matendo 5:12-16, Matendo 19:11-12, Warumi 15:19).
13. Udhihirisho wa nguvu katika Neno la Mungu (Waebrania 4:12, Matendo 19:20).
Mkristo wa Agano jipya anaamuriwa na Roho mtakatifu awe mtu wa nguvu na si maneno matupu.
Haitoshi kusema nimeokoka.
Haitoshi kutaja jina la Yesu, kitakachokutofautisha na WACHAWI, WAGANGA, WAABUDU SHETANI NA WAOVU WA DUNIA HII ni NGUVU KUBWA KULIKO YAO.
Ukikosa nguvu kubwa kuliko yao “watakunya juu ya kichwa chako”… Watakuharibia maisha, huduma, familia na kila ufanyalo.
Nataka uwe na upako kiasi kwamba kuzimu waombe YESU AKUCHUKUE MBINGUNI maana you are too much for them.
KAZANA KUTAFUTA UPAKO… UPAKO (NGUVU YA MUNGU) INAITIKA KWA WAOMBAJI, WAFUNGAJI NA WENYE UFUNUO WA AJABU WA NENO LA MUNGU.
Mungu akupe neema, ukutane na NGUVU ZA ALIYE JUU.
Ifikie mahali ugeuke kuwa NGUVU ZA MUNGU katika mwili.
MAOMBI
1. Muombe Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu (kuchukia udhalimu na kuipenda haki) yanayopelekea upakwe mafuta (UPAKO) wa kipekee kuliko walioko kwenye eneo lako la wito (Zaburi 45:7).
2. Muombe Mungu akusaidie kuondoa kila TABIA MBAYA (Mainzi mafu) inayozuia UPAKO usiwe JUU yako, huduma, biashara, kazi na kile ufanyacho (Yanavundisha MARHAMU/ MAFUTA/UPAKO) uliokuwa JUU yako (Mhubiri 10:1).
3. Muombe Roho Mtakatifu akuwezeshe KUONGEZA KIU NA SHAUKU YAKO kwenye KUUTAFUTA USO WA MUNGU, NGUVU NA UTUKUFU WAKE (Zaburi 105:4, Zaburi 63:1-4).
4. Muombe Mungu akujalie kuzitaka na kuzitamani AINA ZOTE ZA NGUVU ZA MUNGU (walau nilizotaja kwenye somo hili) kisha AKUSAIDIE KUZIOMBA NA KUZING’ANG’ANIA mpaka zionekane maishani mwako (Yohana 7:37-39, Isaya 44:3).
5. Usiache kuniombea mimi Pst. Dickson Cornel Kabigumila, familia yangu, kanisa la ABC ninalochunga, TUZIDI KUSIMAMA KWA USAHIHI NA UAMINIFU NA MUNGU hata mwisho wa uwepo wetu duniani (2Wathesalonike 3:1-3).
Wewe ni mbarikiwa mno,
Umebeba majibu ya mamilioni,
Tukutane kesho SIKU ya nane!
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
ABC GLOBAL.
USIACHE KUTEMBELEA:
www.yesunibwana.co.tz
NB: ENDELEA KUANDAA SADAKA YAKO NZURI YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO HUU, UTAKAYOITOA MWISHO WA MFUNGO.