MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -APRIL [SIKU YA 10]

KUISHI NJE YA UKANDA WA IBILISI

(LIVING BEYOND DEVILS REACH)

Ninasikia kuhusu maombi ya vita. Ni maombi maarufu ya kupigana na Ibilisi na majeshi yake.

Ni maombi maarufu siku hizi za mwisho kwa sababu Ibilisi naye ana bidii akitafuta WA KUWAMEZA (1Petro 5:8-9).

Kwahiyo kuna mapambano kupitia maombi ya watu waliooka na Ibilisi.

Nayapenda maombi ya vita na nayaheshimu.

LAKINI

Sifurahii MUDA MWINGI KUPOTEA KUPIGANA NA SHETANI kuliko muda mwingi kutumika KUBUNI, KUUNDA NA KUFANYA MAMBO MAKUBWA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU NA KUACHA ALAMA KWA DUNIA YAKO!

Ndio maana nataka upate siri za kukufanya usitumie muda mwingi KUPIGANA NA IBILISI.

Bali uishi maisha ambayo IBILISI ANAKAA CHINI YA MIGUU YAKO.

Nataka uzijue siri ambazo zitamfanya Ibilisi ASIWE NA EFFECT MAISHANI MWAKO.

EBU TUONE MAANDIKO AMBAYO YANATHIBITISHA KUWA UNAWEZA KUISHI MBALI NA IBILISI NA MAJESHI YAKE;

“Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya Ulimwengu, YEYE ANIFUATAYE MIMI HATAKWENDA GIZANI KAMWE, bali atakuwa na nuru ya uzima”

(Yohana 8:12).

Yesu anasema KUNA UWEZEKANO KWA AMFUATAYE KUTOKWENDA GIZANI KAMWE (Kutopita kwenye hila, mipango na agenda zote za Ufalme wa giza)!

Kama Yesu kasema hivyo, NI KWELI NA AMINA.

Angalia hili andiko pia;

“Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; Bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, WALA YULE MUOVU HAMGUSI”

(1Yohana 5:18).

Biblia inatuambia kuna MKAO AMBAO Mtu aliyezaliwa na Mungu (aliyeokoka) akikaa, YULE MUOVU HAMGUSI!

Mimi natamani kuishi maisha haya ambayo YULE MUOVU ANANIONA, NAMTIA HASARA, LAKINI HANIGUSI!

Angalia hii nayo;

“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na ng’e, na nguvu zote za yule adui, WALA HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU”

(Luka 10:19).

Hii ni kauli ya Bwana Yesu mwenyewe, anasema kuna mahali unaweza kukaa na IBILISI (NYOKA), MAKAMANDA WAKE (NG’E), NA NGUVU ZOTE ZA ADUI (MAPEPO/ ROHO CHAFU) WAKAWA HAWANA KABISA UWEZO WA KUKUDHURU!

Yesu aliishi kwenye LEVEL HII.

Na haya ni maneno yake;

“Mimi (Yesu) sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana YUAJA MKUU WA ULIMWENGU HUU, WALA HANA KITU KWANGU (Mimi na Yeye hatudaiani na hatuna chochote tunachofanana, hivyo HAWEZI KUNIFANYA CHOCHOTE WALA KUNIGUSA)”

(Yohana 14:30).

Yesu aliishi kwenye viwango hivi VYA KUTOGUSWA KABISA NA IBILISI.

Mpaka mwenyewe alipotangaza na kuruhusu UFALME WA GIZA UFANYE KAZI pale alipokuwa anakamatwa kuelekea kusulubiwa.

“Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni HAMKUNINYOOSHEA MIKONO, lakini hii NDIYO SAA YENU, NA MAMLAKA YA GIZA”

(Luka 22:53).

Yesu hakuguswa na kusumbuliwa na UFALME WA GIZA KABISA mpaka aliporuhusu mwenyewe ili ATIMIZE MPANGO WA WOKOVU.

Hiki ndo kiwango chetu, TUNAPASWA KUISHI KWA NAMNA AMBAYO KUZIMU NA IBILISI HAWANA EFFECT KWETU NA MAISHA YETU.

Ayubu naye aliishi maisha ambayo HAKUGUSWA KABISA NA IBILISI NA HAKUWAHI KUONA IBILISI AKIGUSA MAISHA YAKE AU CHOCHOTE…Aliishi kwenye ULIMWENGU WENYE SHETANI lakini bado IBILISI HAKUWAHI KUMGUSA AU KUMFANYA LOLOTE.

Utaniuliza najuaje hiyo?

Hiyo tunaiona kwenye maneno ya Shetani alipoulizwa na Mungu kuhusu Mtumishi wake Ayubu. Na Shetani ALISEMA SENTENSI AMBAYO INATUONESHA WAZI KWAMBA HAKUWA AKIWEZA KUMGUSA WALA KUGUSA MALI ZAKE AU WATU WAKE.

“…Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? WEWE HUKUMZINGIRA KWA WIGO PANDE ZOTE, PAMOJA NA NYUMBA YAKE, NA VITU VYOTE ALIVYO NAVYO? Kazi zote za mikono yake umenibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi”

(Ayubu 1:9-10).

Ibilisi anasema nini hapa? Anasema hivi, “KILA NJIA NINAYOJARIBU KUTUMIA ILI NIMGUSE AYUBU NA WATOTO WAKE NA MALI ZAKE, IMEKWAMA KWA SABABU KILA NILIPOKUWA NAJARIBU NAKWAMA MAANA KILA ENEO KUNA WIGO WA KUHAKIKISHA HAGUSWI WALA HADHURIKI”

Hiki ndicho ninachokizungumzia katika somo hili.

Kukaa maisha ambayo Ibilisi ANASEMA HUYO JAMAA ACHANENI NAYE kujaribu kufanya chochote kinyume chake ni kupoteza muda, mkono mzimamzima wa Mungu unamhifadhi!

Naamini hadi hapa umeamini kwamba KUNA UWEZEKANO WA KUISHI MBALI NA KILA UONEVU WA IBILISI katika kila eneo la maisha yako na kwenye kila kitu chako.

Ninayajua haya maisha; Ibilisi hawezi kunifanya kitu.

Nimeona nikushirikishe hii siri na wewe utoke kwenye kupigana uhamie level ya kutosumbuliwa kabisa na Ufalme wa Ibilisi!

Sasa zingatia mambo yatakayokusaidia kuingia viwango hivyo ambayo yanafuata hapa chini.

MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA UISHI MBALI NA UONEVU WA IBILISI;

1. KUISHINDA DHAMBI

“Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwakuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo”

(1Yohana 3:8).

Dhambi inafukuza uso wa Mungu.

Dhambi inaufanya mkono wa Mungu usipigane upande wako.

Dhambi inafanya sikio la Mungu lisisikie sauti yako.

(Isaya 59:1-2).

Habari njema ni kwamba UKIOKOKA UNAWEZA KUPEWA NGUVU YA KUICHUKIA DHAMBI JUMLA, NA KISHA KUPEWA NGUVU YA KUISHINDA JUMLA DHAMBI.

Ukiokoka na ukajisalimisha jumla kwa Roho mtakatifu na Neno lake, UNAKUFA KWA HABARI YA DHAMBI NA KUWA HAI KWA MAMBO YA HAKI (1Petro 2:24).

“Kuendelea kucheza na dhambi ni kucheza na Ibilisi. Na kucheza na Ibilisi ni kucheza na uharibifu, mauti na kuibiwa kila kilicho chako”

Ukiishinda dhambi umejitoa kwenye ukanda wa Ibilisi.

2. KUISHI MAISHA YA HAKI

“Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri na watoto wa Ibilisi nao. MTU YEYOTE ASIYETENDA HAKI HATOKANI NA MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake”

(1Yohana 3:10).

Usipotenda haki umejitenga na Ufalme wa Mungu.

Na ukijitenga na Ufalme wa Mungu tayari UMEJIUNGA NA UFALME WA GIZA.

Unaweza kusema simpendi Shetani na NAVUNJA KAZI ZAKE.

Lakini kama unafanya biashara bila kujali haki, na unafanya chochote bila haki, ujue UMEMWALIKA IBILISI.

Maana Ibilisi ni mpinga haki na hakubali haki. Usipotenda haki umempa nafasi ya kukuhangaisha.

3. KUTOISHI MAISHA YA IMANI.

“Lakini MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI; Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. LAKINI SISI HATUMO MIONGONI MWAO WASITAO NA KUPOTEA, BALI TUMO MIONGONI MWAO HAO WALIO NA IMANI YA KUTUOKOA ROHO ZETU”

(Waebrania 10:38-39).

Kuna imani maalumu ambayo INAJENGWA KWA NENO LA MUNGU LA KUTOSHA ambako mtu unaamua KILA KITU CHAKO KIENDESHWE NA NENO TU… Hii ni imani ambayo INAKUTENGA NA YANAYOTOKEA KWA WENGINE (Wasitao na wapoteao: Wanapotezwa na Ibilisi)!

Imani DEEP ambayo unaikuza kila siku kwa kuzama jumla kwenye Neno… Hii inamfanya Ibilisi AACHANE NA WEWE NA MAISHA YAKO JUMLA!

BIBLIA INATUAMBIA IMANI INAPASWA KUFANYIWA MAZOEZI NA KULISHWA ILI IKUE.

Lisha imani yako kwa Neno la kutosha la Mungu na kuomba kwa Roho mtakatifu.

Pia tenga muda SIKILIZA MATENDO MAKUU AMBAYO MUNGU AMETENDA KWA WENGINE (SHUHUDA) na imani yako itapanuka na Ibilisi atapoteza utawala juu yako.

4. UJUE IBILISI AMESETWA CHINI YA MIGUU YA WANA WA MUNGU WANAOJIELEWA.

“Na Mungu wa amani ATAMSETA IBILISI CHINI YA MIGUU YENU UPESI.”

(Warumi 16:20).

Sasa usiniambie Mungu atamseta Ibilisi chini ya miguu yangu nikifika mbinguni; Mbinguni hakuna Ibilisi wala pepo.

Hii inazungumziwa hapahapa duniani.

Ni suala la kujielewa na kujua hilo ni jambo limefanyika ulipookoka.

Shetani amewekwa chini ya miguu yako.

Wachawi, waganga na nguvu zote za kuzima zimewekwa chini ya miguu yako HAPAHAPA DUNIANI.

Ukiona wanasumbua ni kwa sababu hatujakaa sawa kwenye maeneo fulani fulani, tukikaa sawa, malango ya kuzimu hayana uwezo wa kutufanya chochote!

Biblia inasema FALME ZOTE ZA GIZA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO zimetiishwa chini ya MIGUU YA KRISTO KWA AJILI YA KANISA (Waefeso 1:19-23).

Lakini hapo Yesu alipo na anapomkanyagia Ibilisi ndipo tulipo na tumemkanyaga pamoja naye (Waefeso 2:6).

USIKUBALI IBILISI ATOKE CHINI YA MIGUU YAKO.

Endelea kushikilia kile Neno limesema.

Ibilisi na Ufalme wake wanapaswa kuwa chini ya miguu ya WAAMINI.

Ni wajibu wako kuwakanyagia huko wasitoke.

5. TEMBEA KATIKA UPENDO.

“Jilindeni katika upendo wa Mungu…”

(Yuda 1:21).

Upendo wa Mungu ni ulinzi kwake anayedumu ndani yake.

Ukitembea katika Upendo UNALINDWA MBALI NA MKONO WA IBILISI NA MAJESHI YAKE MAOVU.

Nikuombe uangalie Upendo wako na uchochee upendo wako.

Upendo kwa Mungu na Upendo kwa Watu.

Kumbuka kanuni hii ya Upendo;

“HUWEZI KUSEMA UNAMPENDA MUNGU USIYEMUONA ILHALI HUMPENDI NDUGU YAKO UNAYEMUONA”

(1Yohana 4:20-21).

Mimi “nakuhimiza udumu katika upendo na kazi nzuri” (Waebrania 10:24).

Ukidumu katika UPENDO umedumu katika Mungu na ukiwa katika Mungu hakuna wa kukugusa.

(1Yohana 4:16, Warumi 8:31).

Kila mtu ambaye AMEZAMA KWENYE NENO NA KULIRUHUSU LIMTAWALE ATAKUWA MTU WA UPENDO (1Yohana 2:5).

MAOMBI

1. Muombe Mungu akusaidie utembee katika UTAKATIFU (mbali na DHAMBI) na adui asikuguse wewe na watu wa nyumbani kwako, kama ilivyokuwa kwa Ayubu aliyekuwa mcha Mungu, akalindwa na familia yake huku Mali zake zikiongezeka (Ayubu 1:1-10).

2. Muombe Mungu akusaidie kutembea katika Upendo, kwa maana mtu wa upendo hukaa katika Mungu (mahali ambako Giza/ Shetani halimo ndani yake: 1Yohana 1:5-7), Upendo ni ulinzi DHIDI ya Ibilisi na kazi zake, hukufanya ukae ndani ya Mungu, Ibilisi asikoweza kukugusa (1Yohana 4:3-8)!

3. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kukumbuka kila siku ya kuwa Ibilisi ameshasetwa CHINI ya miguu yako (Warumi 16:20), na ya kuwa Shetani na nguvu zake zooooote una nguvu na mamlaka ya kuzikanyaga na haziwezi kukudhuru kabisa (Luka 10:19, Luka 9:1-2)!

Kwa mwezi Huu tunaishia hapa,

Umebarikiwa.

WEWE NI SHUJAA, WEWE NI MTU MKUU.

HONGERA KWA KUFUNGA SIKU HIZI KUMI ZA MWISHO WA MWEZI WA NNE.

Pst. Dickson Cornel Kabigumila,

Mchungaji kiongozi,

Assembly Of Believers Church (ABC),

01/05/2019.

Nikusihi usiache kutembelea tovuti yangu ya mafundisho na kujiunga (subscribe) kwa email ili kujiunga na wale ambao wanatumiwa mafundisho kwenye email zao mara mbili hadi tatu kwa wiki,

NB: SADAKA YA KUAMBATANISHA NA MFUNGO, INATUMWA LEO, NAAMINI ULISHAMUOMBA MUNGU NA UMEIANDAA NA KUITAMKIA NENO!

ITUME KWENYE MOJAWAPO:

M-PESA: 0753 466 675

TIGOPESA: 0655 466 675

CRDB: 01J 2084559100 (Dickson Cornel Kabigumila)

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »