MFUNGO WA WA SIKU 10WA KILA MWISHO WA MWEZI. [SIKU YA NANE ]

 

NEEMA YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI

(THE SPECIAL GRACE OF GOD IN TIMES OF NEED).

Kwenye dunia hii tunayoishi, mahitaji yapo na yataendelea kuwepo.

Lakini Mungu wetu hakuna kitu ambacho hajakipa suluhu katika Neno lake.

Kwenye maisha haya uhitaji na mahitaji vipo mpaka Yesu anarudi.

Na mahitaji yapo ya aina na namna nyingi.

Kuna wenye mahitaji ya kiuchumi, mahitaji ya kiafya, mahitaji ya amani, na mahitaji mengine ya namna mbali mbali.

Mungu wetu katika Kristo Yesu ameitoa neema hii maalum ya kutusaidia na kututoa kwenye mahitaji mbali mbali!

Ukiisoma Waebrania 4:16, imeandikwa;
“Na tukikaribie KITI CHA NEEMA kwa ujasiri, ili tupate rehema, NA KUPATA NEEMA YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI…”

°Neema hii ndiyo iliyomsaidia MJANE WA SAREPTA WAKATI WA NJAA KALI KATIKA ISRAELI ZAMA ZA NABII ELIYA… wakati akiwa amebakiza mlo mmoja pekee, Mungu alimtuma Eliya kwake na Alipofaulu mtihani wa utoaji, ALIPATA MAHITAJI YA CHAKULA KWA MIAKA MITATU NA NUSU YA UKAME (1Wafalme 17:7-16).

Wakati akiwa hajui cha kufanya, akiwa anataka ale mlo pekee uliobaki na afe na mwanae, NEEMA YA MUNGU YA KUMSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI ilimfikia japo kupitia mtihani wa utoaji na kumuamini Mungu kwa kidogo anachokihitaji zaidi, ALIPOLIAMINI NENO LA MUNGU LIKAMTOA KWENYE UANGAMIVU (Zaburi 107:20)!

°Mwanamke mjane ambaye mme wake nabii alikufa na kuacha deni kubwa kiasi cha watoto wake kutaka kuchukuliwa utumwani, ALIKUWA KATIKA HALI NGUMU MNO, Lakini NEEMA YA MUNGU ILIMTOA kupitia maelekezo ya nabii Elisha aliyoyatendea kazi (2Wafalme 4:1-7).

°Mwanamke Mshunami, Mtoaji aliyempa Elisha na mtumishi wake mahali pa kulala kila walipokuja mjini kwake, ALIKUWA NA UHITAJI WA MTOTO, KWA NEEMA AKAPATA… MTOTO AKAFA na kuwa katika hali ngumu sana, lakini NEEMA YA MUNGU YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI ilimsaidia na MTOTO AKAFUFUKA NA KUISHI TENA (2Wafalme 4:8-37).

°Neema hii ilifanya kazi wakati wa Musa pia;

i) Wakati wanafuatiwa na maadui (jeshi la Farao) na mbele kuna bahari ya Shamu, katika UHITAJI HUO NEEMA YA MUNGU ILIWAPA SULUHU (Kutoka 14:21-31).

ii) Walipokuwa na uhitaji wa maji jangwani, NEEMA YA MUNGU INAYOSHUGHULIKA NA MAHITAJI ILIWAPA MAJI KWENYE MWAMBA (Zaburi 105:41).

iii) Walipohitaji nyama, Mungu aliwapa kware, walipohitaji mikate, Mungu aliwapa mana kwa neema yake maalum ya kuwatoa watu kwenye uhitaji (Kutoka 16:8-22).

Ukiangalia hali zote hizo, HAKUKUWA NA MAZINGIRA YA KIBINADAMU YA KUWASAIDIA… NI NEEMA YA MUNGU YA KUTATUA MAHITAJI YA WATU WAKE NDIYO ILIYOKUWA KAZINI!

°Hata wakati wa huduma ya Bwana Yesu, neema hii ya ajabu ndiyo ILIYOHUDUMIA MAHITAJI YAKE NA KILA KITU KWENYE HUDUMA YAKE!

•Maelfu walikula mahali ambako hakuna chakula hadi wakasaza vikapu kumi na viwili (Yohana 6:1-12)!

Kodi ililipwa kwa shekeli toka kwenye kinywa cha samaki, uhitaji ule ulihudumiwa kimiujiza na BWANA YESU (Mathayo 17:27)!

•Punda ambaye hajapandwa alipatikana na kuletwa kwa Yesu bila hata malipo yoyote wakati Yesu alipokuwa na uhitaji wa punda wa kuingia naye Yerusalemu ili kutimiza unabii (Luka 19:30-31)

•Petro alikamata maelfu ya samaki mchana kweupe baada ya usiku kucha kutoambulia chochote, ilikuwa ni matokeo ya Neno la neema lililotamkwa kwake na Yesu (Luka 5:1-10).

•Malaika walikuwepo kila muda kuhudumia mahitaji yake (Marko 1:13).

•Hata alipohitaji mafuta ya kuuandaa mwili wake kwa maziko, alitokea mwanamke aliyesamehewa dhambi na kuiosha miguu yake kwa machozi na kuipaka mafuta na kumuandaa kwa maziko (Yohana 12:3-7)!

KWENYE MAISHA YA BWANA YESU HAPA DUNIANI, NEEMA HII MAALUM YA MUNGU YA KUMSAIDIA KILA WAKATI WA UHITAJI ILIKUWA TELE!

Na hivi ndivyo Mungu anavyotaka watoto wake wote tuishi. Kila alilolifaidi Bwana Yesu ni urithi wetu pia (Warumi 8:16-17). Maana sababu kubwa ya Mungu kutuokoa ni ILI TUWE KAMA YESU (TUFANANISHWE NA MFANO WA MWANAE) HAPA DUNIANI (Warumi 8:29)!

Hii neema maalum ni yangu, ni yako na ni yetu sisi tulionunuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu!

Usikubali kuishi maisha ambayo neema hii huioni ikikufanyia kazi kila wakati.

MAMBO YANAYOFANYA NEEMA HII IFANYE KAZI;

i) MAOMBI YA IMANI KWA MUNGU
(Waebrania 4:16, Mathayo 7:7-10).

ii) KUTOKUMUWEKEA MUNGU MIPAKA KATIKA UTENDAJI WAKE/ KUAMINI KWAMBA HATA MWAMBA UNAWEZA KUTOA MAJI, AU MIKATE MITANO NA SAMAKI WAWILI WANAWEZA KULISHA MAELFU YA WATU MUNGU AKIHUSIKA, AU MAJI YANAWEZA KUWA DIVAI TENA TAMU YESU AKIHUSISHWA!
•Mungu wetu anaweza kufanya mambo makubwa mno zaidi ya tuombayo na tuwazayo (Waefeso 3:20).
•Hakuna lisilowezekana kwake (Luka 1:37, Mwanzo 18:14)
•Mkono wake si mfupi hata asiokoe (Isaya 59:1-2)
•Akili zake hazichunguziki (Isaya 40:28).
Hivyo usimuwekee MIPAKA kama wana wa Israeli walivyofanya jangwani (Zaburi 78:41).

iii) KUPANDA (KUTOA) KWA WATUMISHI WA MUNGU

-Kanisa la Filipi lilitamkiwa Mungu kuwapa kila wanachokihitaji (Wafilipi 4:19), baada ya wao kupanda/ kumbariki Mtumishi wa Mungu Paulo na kuhudumia mahitaji yake (Wafilipi 4:14-18)!

-Mjane wa Sarepta, alipata suluhu ya UHITAJI wake wa CHAKULA baada ya yeye kumlisha kwanza nabii wa BWANA, Eliya (1Wafalme 19)!

-Mwanamke Mshunami aliyekuwa na uhitaji wa mtoto, ingawa umri wake na mmewe ulishawatupa mkono, WALIPOJITOA KUHUDUMIA MAISHA YA MTUMISHI WA MUNGU ELISHA, KWA KUMPA MAHALI PA KULALA NA CHAKULA, NDIPO HITAJI LAO LILIPOTATULIWA (2Wafalme 4:8-37).

UKIYAZINGATIA HAYA MAMBO MAKUU MATATU: KUOMBA, KUTOA KUHUDUMIA MAHITAJI YA WATUMISHI WA MUNGU NA KUTOMUWEKEA MUNGU MIPAKA YA KUTENDA, UTAISHI KWENYE NEEMA HII YA KUKUSAIDIA NA KUKUVUSHA WAKATI WA MAHITAJI!

MAOMBI

ASUBUHI

1. Muombe Mungu akupe neema yake maalum ambayo itahudumia mahitaji yako “on time” kila yanapojitokeza hata kama kibinadamu unakuwa umefika mwisho wa akili zako na huna njia (Waebrania 4:16).

2. Muombe Mungu akuthibitishe kama kondoo wake na ahakikishe haupungukiwi na kitu (Zaburi 23:1-6).

MCHANA

1. Muombe Mungu aachilie malaika zake watakaohudumia kila uhitaji wako hata mahali ambako hakuna namna ya kibinadamu ya kupata mahitaji (Marko 1:13).

2. Muombe Mungu aguse watu wenye vitu unavyovihitaji aliowaandaa kukuhudumia kwa vitu na Mali zao (Luka 8:1-4).

JIONI

1. Muombe Mungu akusaidie kuwa na furaha, utulivu na amani MOYONI hata kama una uhitaji, vitakavyokufanya uombe na kupeleka haja zako MBINGUNI badala ya kusumbuka na kujitesa kibinadamu (Wafilipi 4:4-7).

2. Muombe Mungu akujaze kila unachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake katika Kristo Yesu (Wafilipi 4:19).

NB: TUOMBEE MIMI MCHUNGAJI DICKSON NA MKE WANGU MERCY, TUNA UHITAJI WA TSH. MILIONI MBILI NA LAKI SABA, INAYOPASWA KUPATIKANA KABLA YA TAREHE 01/04/2019, NA UKIGUSWA KUTOA KWA AJILI YA UHITAJI HUO, RUKSA KUSHIRIKI BARAKA HIYO KWA KUHUDUMIA MAISHA YETU KAMA WATUMISHI WA MUNGU, MUNGU AKUBARIKI UNAPOSIMAMA NASI KWA MAOMBI AU SADAKA YAKO AU VYOTE VIWILI!!

Umebarikiwa mno,
Wewe ni wa thamani na ni jibu kwa dunia yako!
Tukutane kesho siku ya tisa.

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »