Mnenaji: Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila.
Tukio: Semina Maalum ya Wadada
Tarehe: 14/02/2016
Utangulizi
⚡Nafsi imegawanyika katika sehem kuu tatu.
1)Hisia (Emotions & Feelings)
2)Maamuzi na machaguo (choices and decisions)
3)Akili (Intellect part)
Na katika somo hili tunajifunza kuhusu hisia.
1)HISIA
Hisia zipo ndani ya mtu tayari na zinaamka zikipata reaction kutoka nje.
Kuna aina mbili za hisia
a) Positive feelings
mfano: furaha, amani, kushangilia nk
b) Negative feelings
mfano: kulia, huzuni, uchungu nk
Vyote hivi vipo ndani ya mtu tayari lakini hadi vipate reaction kutoka nje ndio vitaonekana.
Hisia zinatokana na taarifa kutoka kwenye milango mitano ya ufahamu.
Yaani: Hata Mungu aliyetuumba sisi kwa sura na mfano wake ana hisia hizi za aina mbili:
i)Hasi
Mfano: “Hasira ya Bwana ikawaka”
Au “Mimi ni Mungu mwenye wivu”
Ama
“Wala msimhuzunishe Roho mtakatifu”
Hizi hisia hata Baba yetu anazo lakini anajua namna ya kuzicontrol!
ii) Chanya
“Mungu ni pendo”
Au
“Furaha ya Bwana ni nguvu yetu” ikiwa na maana anafurahi pia.
Lakini anajua namna ya kuzitawala hisia zake.
Hivyo basi, si tatizo kuwa na hisia chanya.
Bali hisia hasi usipojua namna ya kuzitawala na kuzimilki zitakuharibia maisha na watu wengine wanaokuzunguka.
Kumbuka: Hauwezi kuomba ili hasira isiweko kabisa ndani yako, ila unaweza kuomba “hasira isikutawale” (Waefeso 4:26).
Na ni wajibu wako kumnyima nafasi Ibilisi kukulisha taarifa mbaya na kukujeruhi ili kuamsha “hisia hasi” ndani yako ili ufanye dhambi na matukio mabaya!
Jambo jingine la muhimu kujua:
Vichocheo vinavyoamsha hisia hasi (hasira, uchungu, majeraha ya nafsi, visasi) yanakuja kupitia MILANGO MITANO YA FAHAMU.
Unachoona
Unachosikia
Unachogusa/hisi
Unachonusa
Unacholamba
Kama si kizuri, HISIA HASI zitaamka ndani yako na unaweza kufanya mambo ya ajabu.
Jiandae, uko duniani, utaona mengi mabaya ya kuumiza, utasikia taarifa mbaya, utahisi, utagusa na hata kunusa vitu vinavyokera na kuboa.
Mwitikio wako ndio utakaoamua nini utafanya na nini kitajengeka ndani yako.
Ili kushinda hisia mbaya, na majeraha ya nafsi tunapaswa tujue kanuni za Kibiblia za kutawala milango yetu mitano ya fahamu na kila kinachoingia ndani yetu kupitia hiyo!
kwahyo ili tuweze kujicontrol kwenye negative feelings zisituaffect maisha yetu na kuona hatuna sababu yoyote ya kuishi kwasababu ya tarifa uliyosikia au kuona ikaaamsha hisia zako tunapaswa kuwa na taarifa nyingi za neno la Mungu ili ziweze kubadilisha mazingira ya nje.
Hasira, Wivu, huzuni, uchungu vyote hivi vinapaswa viwe controlled na neno la Mungu.
Mungu akusaidie kutembea juu ya kila changamoto kutokana na wingi wa neno lililojaa ndani yako na lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu..
❤❤ vitu viwili vinavyokaa karibu na moyo wa mtu
a) Yesu (neno)
Ufunuo 3:20 msaada ambao upo muda wowote.
ukimkataa Shetani then umemkubali Yesu
b) Dhambi
Mwanzo 4:7
ukimkubali shetani then umemkataa Yesu.
Yesu yuko karibu na moyo wako kwa mujibu wa Ufunuo 3:20, akisubiri umpe nafasi akusaidie.
Lakini pia dhambi iko mlangoni kwa moyo wako ikisubiri uliache Neno na agizo la Mungu iingie ndani yako.
Kama ilivyokuwa kwa Kaini (Mwanzo 4:7-8)
Ni wajibu wako kuruhusu nini kiingie na kipi kisiingie MOYONI MWAKO hasa UNAPOPATA TAARIFA MBAYA kutoka kwenye mazingira yako, watu wako, ndugu, mme, mke, watoto, biashara yako nakadhalika.
Ayubu alipopata TAARIFA MBAYA kuhusu wanae, mifugo, mali zake na hata afya yake, HAKUTENDA DHAMBI WALA KUMUWAZIA MUNGU KWA UPUMBAVU (Ayubu 1:22).
Alijua namna ya KUKABILI TAARIFA KUTOKA NJE.
Biblia inasema alichofanya ni “KUMSIFU MUNGU” akisema “JINA LA BWANA LIBARIKIWE”
Ni wajibu wako kujipanga kwa Neno, kwa kumuomba Mungu, na kupata nguvu ya kukabili kila HABARI MBAYA.
“Mwenye haki HATAOGOPA HABARI MBAYA, MOYO WAKE UIMARA UKIMTUMAINI BWANA”
(Zaburi 112:6-7).
Kadri ambavyo UNAKABIDHI MOYO WAKO KWA BWANA… UNA UHAKIKA WA KUTOTETEREKA HABARI MBAYA NA MABAYA YAKITOKEA.
Lakini kadri unavyokuwa unaombea vitu na maisha yako (unavikabidhi kwa Bwana kama Ayubu alivyokuwa akifanya ibada kwa ajili ya wanae na kuwatolea sadaka), unajikuta UNAJUA MUNGU YUKO KAZINI, BILA KUJALI NINI KINAKUTOKEA!
Waebrania 5:7 ” Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule,awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.”
hapa tunaona Yesu pia alilia.
wanawake na mabinti wengi huwa tukiumia ni wepesi sana kulia…
Yaan haijalishi umeumizwa kiasi gani usiseme siwezi kuomba nooooo nenda mbele za Mungu kwa machozi na kulia Mungu anasikia aisee.
Stephano pia alilia.
1 Peter 5:7
” huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
⚡Mungu anajishughulisha sana kwa mambo yetu sio mambo yake ni yetu kwahyo kazi yetu ni kumtika yeye fadhaa zetu zote
Fadhaa ni chochote cha huzuni, kusikitisha, kinachochukua amani yako, kinachokufanya usifurahiw maisha na kisichokupa raha nafsini mwako.
Mwambie Mungu fulani (mtaje jina) amekuwa mwiba kwangu.
ongea na Mungu mwambie fadhaa zako zote
Mathayo 11:28
kuna vitu vwili ambavyo vipo hapo
a) Mungu hataki mtu asumbuke yaani unapaswa uishi maisha ya raha, luxurious life
b) Mungu hataki ulemewe. Mwambie hilo linalokulemea kwamba umejaribu peke yako umeshindwa.
Yakobo 5:12 inasema, “Je mtu wa kwenu amepatwa na mabaya? AOMBE. Ana moyo wa kuchangamka na AIMBE ZABURI”
Hii ina maana siku unazokutana na taarifa mbaya au matukio mabaya… BREKI YA KWANZA NI KWA BWANA KUMUELEZA KWA UWAZI NA BILA KIFICHO… UNAVYOJISIKIA… ULIVYOUMIA… KAMA NI KULIA LIA KWELI… KAMA NI KUSHTAKI SHTAKI SANA TU… Lakini hakikisha unatumia TAARIFA MBAYA KAMA MWALIKO WA KUOMBA… Ibilisi hatakuumiza kamwe wala kukuua kama wengine.
Unapoomba, kusali na kushukuru, AMANI YA MUNGU ITAKUFUNIKA NA KUPONYA “MOYO WAKO NA NAFSI YAKO (NIA YAKO)” (Wafilipi 4:6-7).
Na moyo na nafsi zetu kumbe zinaponywa na KUOMBA, KUSALI NA KUMSHUKURU MUNGU badala ya kumlaumu au kulaumu watu au matukio.
Kama tukio limetokea na bado HALIJAKUATHIRI SANA NA KUKUONDOLEA UCHANGAMFU… Huo ni muda mzuri wa KUIMBA ZABURI (Kuanza kumsifu na kumuabudu Mungu)!
Kuna nguvu katika kuabudu na kumsifu Mungu katikati ya jaribu na changamoto.
Paulo na Sila gerezani walisifu na kumuabudu Mungu MILANGO YA GEREZA IKAFUNGUKA KWA UPAKO ULIOSHUKA JUU YAO.
Nakuona ukimsifu na kumuabudu Mungu badala ya kulia na kuomboleza kila hali na taarifa mbaya zijapo na ninamuona Mungu akikuvusha kwenye kila jaribu, pito na gereza katika jina la Yesu!
⚡2 Wakorintho 4:18” tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana, kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”
chochote kile ambacho kinaonekana au kimeshaokea kwenye mazingira ya nje tayari ni cha muda maadam tu kinaonekana basi ni cha muda tu sio cha kudumu.
Hivyo haijalishi umefanyiwa kitu gani kikaamsha negative hisia ndani yako( uchungu, huzuni, masikitiko, kukosa amani) maadam tu kinaonekana basi ni cha muda tu yaani lazima kitaondoka.
Hapa Biblia inasema tusitazame vinavyoonekana bali tutazame visivyoonekana.
Na visivyo oonekana vinahitaji imani yaani unaangalia vitu jinsi ambavyo neno la Mungu linasema.
🔒Yote yaliyosikiwa au yaliyoonekana haijalishi yamebeba ujumbe gani mbaya kiasi gani hayo ni ya muda tu kwasababu yameshaonekana.
🎄unapopata zuri lolote kwenye maisha yako ni muda wa weww kutoa muda wako mwingi sana kukiatamia kwenye maombi.
Next levels New devils.
kwa kadiri unavyopata mafanikio na mazuri ndivyo ambavyo na shetani anazidi kukukarbia ili apate nafasi, na mara nyingi sana tunajisahau tunapopata yale tuliyoyategemea.
💊 ukiona kitu kizuri kimetokea kwenye maisha yako ndio muda wa kuomba kuliko kawaida.
” Udhanipo kuna amani ndipo uharibifu huja”
1 wakorintho 16:9 ” kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wapo wengi wanipingao”
kwahyo jua kwamba kwenye kila mlango mkubwa uliofunguliwa kwako wapo wengi(hawana idadi) wakupingao.
Ufunuo 12:13-16
Ufunuo 12:4b “na yule joka akasimama mbele za yule mwanamke aliye tayari kuzaaa,ili azaapo amle mtoto wake”
unaona huyu mwanamke anategemea kupata mtoto yaani taarifa njema, lakini yule joka anasubiri azae tu ili amle mtoto wake.
Chochote ambacho unatamani kukizaa kiatamie kwenye maombi ili shetani asikile kwenye elimu yako, kazi yako, ndoa yako, huduma yako, biashara yako nakadhalika.
Ufunuo 12:4 inasema “Ibilisi (joka) alikuwa amesimama mbele ya mwanamke mwenye mimba anayetaka kuzaa ili amle mwanae akimzaa”
Hii ina maana kuna vita kati yako na Ibilisi isiyokoma.
Unapoomba muujiza usifikiri Shetani anakuchekea, anasubiri uje huo muujiza auharibu kabla hujaufaidi!
Angalia “mwanamke anafurahia kuwa anakwenda kuzaa mtoto” asijue Ibilisi yuko hapo karibu anasubiri kuumeza huo muujiza.
Ndio maana watu wanaomba wanapata waume, halafu ndoa (mtoto aliyezaliwa) inakuwa mbovu na inavunjika.
Mtu anaomba kazi, akifika kazini kazi inakuwa uwanja wa vita na anaweza kuamua kuacha (mtoto ameliwa na joka)!
Daka hii:
“Kila muujiza unaotaka kuuzaa Ibilisi anausubiria ili aule”
Ndio maana WATU WANAANZISHA VITU VINAKUFA.
Biashara unaanza vizuri na una uhakika unakwenda kutoka, INALIWA NA JOKA.
Hii ni sababu ya kukufanya UDUMU KUOMBA MPAKA YESU ANARUDI.
HAKUNA BREKI YA MAOMBI RAFIKI YANGU kama unataka vitu vizaliwe!
1Wakorintho 16:9 inasema “Nimefunguliwa mlango mkubwa na wa kufaa sana lakini wako wengi wazuiao/ wanipingao”
Hii ina maana kila ukiona mpenyo, kitu fulani kimetokea, umepata mme, mke, baraka, huduma imekua, umepata mtoto… JIANDAE, KUZIMU NZIMA ITAAMKA KUJARIBU KUUA HUO MLANGO MZURI WA KUFAA.
Ni wajibu wako KUKESHA UKIOMBA ILI MWIZI AJAPO ASIINGIE KWAKO!
UAMUZI NI WAKO.
Unawajibika kuamua ni aina gani ya mawazo uyaruhusu yatawale maisha yako either positively au negatively.
2 Wakorintho 10:3-5
Jinsi ya mwili ni kuangalia vitu vinavyoonekana au taarifa zinasemaje. Yatupasa tuamue kutoka ndani sawasawa na neno lililopo moyoni ili tuwrxe kureact na taarifa mbaya ambazo tunaziona nje
Ni wajibu wako kutiisha kila wazo lako.
Matendo 5:1-11
Waefeso 4:26-27
Yakobo 5:13 — upatwapo na baya lolote cha kwanza kufanya ***OMBA***
Wafilipi 4:6-7.
cha mwisho pima mawazo yako.
Zaburi 19:14
na ukisoma Wafilipi 4:8 inatufundisha yapi ya kutafakari
1)Yaliyo ya kweli
2)Yaliyo ya staha/ sitirika, bila uchafu
3)Yaliyo ya haki
4)Yaliyo safi
5) Yenye kupendeza
6)Yenye sifa njema
7) Yenye wema wowote
8)Yenye sifa yoyote nzuri
Chochote utakachokitafakari nje ya hzi point nane basi achana nalo lisikuumize kichwa.
Waza na kutafakari aina hizi tu za mawazo.
Mengine nje ya hapo yaangushe na kuyapangua kwa jina la Yesu!
Mwisho kabisa, ni mapenzi ya Mungu tuwe na furaha kila saa ,sekunde, dakika na kila wakati.
Isaya 12:3
“Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu”
Mungu anahitaji furaha yako ili umwabudu.
Isaya 55:12
“Maana mtatoka kwa furaha, mtaongozwa kwa amani ….mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo (hali ngumu zinazozuia wengine kwenu zitakuwa fursa), na miti ya kondeni (wanadamu) itawapigia makofi (watawacelebrate)”
Yohana 16:23-24
“……. hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu iwe timilifu”
Kusudi la Mungu kukujibu maombi yako ni ili ufurahi.
Yesu anawajibika na furaha yako yaani yupo comitted kuhakikisha kila muda unafurahi (Wafilipi 4:4).
Ndiyo maana hakufia dhambi tu msalabani bali pia “HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU” (Isaya 53:4).
Kwa hiyo maombi ni opportunity ya kukufanya ufurahi.
Hesabu 23:19
“Mungu si mtu , aseme uongo…..
so ikiwa Mungu amesena na umeona kwenye neno lake lazima atimize”
Nikutakie uanafunzi mzuri.
Urudie na kurudia na kurudia na kisha UYATENDE MOJA BAADA YA JINGINE, mpaka utakapokuwa MASTER WA HISIA ZAKO!
Mwl D.C.Kabigumila
Assembly Of Believers Church (ABC).