WAJUZI WA KARAMA ZINAA IMETAJWA KWAO

 

_Na. Mwl. Nickson Mabena_

*“hata hamkupungukiwa na karama yo yote,* mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;”
1 Wakorintho 1:7

•Bwana Yesu Asifiwe,
Ninayo Furaha kukukaribisha kujifunza kupitia somo hili fupi ambalo Roho Mtakatifu ameruhusu TUJIFUNZE KATIKA WAKATI HUU!.

•Kwanza naomba rejea kwenye somo nililolipa kichwa cha UJUMBE ‘KUHANI MWENYE MAVAZI MACHAFU’ , ukiunganisha ujumbe uliopo kwenye somo hilo pamoja na somo hili HAKIKA UTAPATA KITU KAMILI!

-Kanisa la Korintho ni miongoni mwa Makanisa yaliyopata kuandikiwa Barua na Mtume Paulo, huku wao wakiandikiwa Barua mbili ambazo tunazifahamu kama WARAKA WA KWANZA NA WARAKA WA PILI!.

-Katika Sura ya Kwanza Paulo anatueleza Sifa za Kanisa hili la Korintho,
Kwenye mstari wa saba anatutajia Sifa nyingine ya kuwa HAWAKUPUNGUKIWA KARAMA YOYOTE!

-Kwa hiyo, ninaweza nikasema kwamba hili KANISA LILIKUWA LIMEBARIKIWA KUWA NA KARAMA NYINGI SANA!

•Nizungumzie kwa ujumla wa wake ‘KARAMA , HUDUMA NA VIPAWA’ kwamba KANISA HILI LILIKUWA VIZURI!.

Kwa hiyo, hawa watu walikuwa wataalamu sana kwenye;-

•Kuimba
•Kucheza
•Kunena kwa Lugha
•Kutabiri
•Kutenda MIUJIZA
•Imani
•Aina za Lugha & Tafsiri
•Kuponya

N.k

Lakini,

Pamoja na KUWA ‘HAWAKUPUNGUKIWA’ KARAMA YOYOTE;

Paulo anatueleza habari zingine kuhusu Kanisa hili;

1.Ni WATU WA MWILINI.

“kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; *tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?”*
1 Wakorintho 3:3

-Humo humo Kulikuwa na WATU WA MWILINI KABISAA; tena WANAOENENDA KWA JINSI YA KIBINADAMU!

•Ikafika hatua wakawa wanajitambulisha kwa Majina ya Watumishi waliowahubiria INJILI,
Wengine wanadai ni wa Apolo wengine wa Paulo.

-Leo hii ukimsikia mtu anajitambulisha sana kwa jina la Mchungaji wake au kwa jina la Dini yake basi ujue huyo ni MTU WA MWILINI!

-Kuna watu wanajua bhana kuwatukuza ‘mababa’ zao wa Kiroho kuliko hata ALIYEWAFIA MSALABANI;

‘Paulo’ anawauliza JE! HIYO DINI NDIYO ILIYOKUFIA MSALABANI?

2.NI WACHANGA KIROHO.

“Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, *kama na watoto wachanga katika Kristo.”*
1 Wakorintho 3:1

-Unabishana na mtu humu mtandaoni kuhusu mambo ya KIROHO, kumbe tatizo ni UCHANGA!

Mbaya zaidi umkute ni Mchanga ASIYETAKA KUKUA.. hapo ni shughuli;

-Ukiona unasumbuliwa na TABIA ZA MWILINI , ujue wewe ni MCHANGA, unatakiwa KUKUA!

-Usipokua, utasumbuka sana.

•Hawa Jamaa pamoja na UJUZI WA KARAMA ZOTE, bado walikuwa ni WACHANGA eti!

3.ZINAA IMETAJWA KWAO

*“Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa*, na *zinaa* ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.”
1 Wakorintho 5:1

•Jambo hili ndio hasaa limenisukuma KUANDIKIA SOMO HILI;

•Wale watu tulioambiwa kuwa HAWAKUPUNGUKIWA KARAMA YOYOTE, leo hii tunaambiwa kuwa HABARI IMEENEA KWAMBA KWAO KUNA ZINAA!.😢

•Tena ZINAA isiyokuwepo hata kwa MATAIFA!.

Biblia inasema

“Lakini uasherati *usitajwe kwenu kamwe,* wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
Waefeso 5:3

-Kwa hiyo KITENDO tu cha ZINAA Kutajwa kwao ni ‘DOA’ kubwa kwa Kanisa bila kujali WANAZO KARAMA NYINGI KIASI GANI!

-Sipo hapa ku discourage KARAMA; hapana, bali NIPO HAPA KUMSAIDIA MTU MMOJA AMBAYE ANAFIKIRI KUWA KARAMA NDIO KIPIMO CHA UTAKATIFU!

-Kanisa Linaweza likawa lipo vizuri sana kwenye eneo la HUDUMA, KARAMA NA VIPAWA lakini bado ‘ZINAA IKATAJWA KWAO’

-Wewe UNAWEZA UKAWA MJUZI WA KARAMA , LAKINI BADO UNATESWA NA ZINAA pamoja na tabia zingine za MWILINI.

•Jamani Wapendwa, KARAMA NI NZURI MNO MNO; lakini zisitumike kama ‘shuka’ la kufichia UCHAFU unaofanyika kwenu!

•Kanisani kwenu mnaweza kabisa mkawa ni ‘WAJUZI WA KARAMA ZOTE’ lakini wengi wenu MKAWA BADO WACHANGA, WATU WA MWILINI huku MKISUMBULIWA NA ZINAA!

•Fatilia, Wengi walioringia ‘VIPAWA’ wakasahau kabisa mambo ya KUKUA KIROHO waliishia Kubaya sana;
Kama hawakuwa na viburi basi WALIANGUKA KWENYE ZINAA!

•Hata sitaki niringie UANDISHI na UHUBIRI Nilionao, alafu UASHERATI UKATAJWA KWANGU;
*SITAKI KABISAA*!

•Paulo mwenyewe alisema “ANAUTESA MWILI WAKE NA KUUTUMIKISHA; ISIWE AIISHA KUWAHUBIRI WENGINE YEYE AWE MTU WA KUKATALIWA”

•HAKIKISHA UASHERATI HAUTAJWI KWAKO, hata kama wewe ni ‘SOLO’ kwenye Kwaya yenu!.

•UNAWEZA UKAWA MJUZI WA KARAMA FULANI, BADO UKAWA MCHANGA NA MTU WA MWILINI UNAYETESWA SANA NA ZINAA!

ZINAA ISITAJWE KWAKO

Naomba niishie hapo,
Ubarikiwe,

Mwl. Nick ( Nickson Mabena)
0712265856
(WhatsApp#)

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »