Tumewekwa huru na yesu…..>2

http://yesunibwana.files.wordpress.com/2012/05/jesuswithhissheep.jpg?w=239

TUMEWEKWA HURU NA YESU ILI KUWAWEKA HURU WENGINE>>> Wiki iliyopita nilikuwa nafanya COUNSELLING kwa dada mmoja ambaye alikuwa amekata TAMAA ya kuishi na alikuwa na kiu sana ya KUJIUA maana alishachoka kuishi na hakuwa na sababu ya kumfanya aendelee kuishi…Alikuwa ameichoka dunia na kila aliyemo, aliiona dunia si mahali pake tena, hakuwa na rafiki au ndugu aliyemwamini tena, kwa kifupi MAISHA HAYAKUWA NA THAMANI WALA MAANA KWAKE…Alikihitaji kifo kuliko uhai!
Halafu Mungu alimpa neema ya kukutana na kaka mmoja ambaye ni rafiki yangu aliyenieleza kuhusu huyu dada, nami nikamwambia kwa ujasiri mkaribishe aje tuonane, Huyu hawezi kufa wala kuharibikiwa na maisha, Msalaba wa Yesu ulishaweka mambo yote sawa…Mungu ni mwema sana, Yule dada alikubali kuja, nikakaa naye chini ktk uwepo wa Bwana, akaeleza mambo yake yote kwa uwazi na nikamshauri na kumweleza kile ambacho Mungu anasema kuhusu kesho yake na kisha tukamwitia YESU…Roho Mtakatifu alikuwepo na Nguvu zake, akamgusa na kumuweka huru kabisa! Pia alikuwa na matatizo ya MOYO, ASTHMA, Mapafu nk lakini yote haya YESU WA NAZARETH aliyabeba pale pale na kulithibitisha lile Neno la Mathayo 8:17, “Mwenyewe ameyajitwika udhaifu wetu, ameyachukua Magonjwa yetu”…Ni wiki moja nzima sasa, na huyu binti ana furaha, amani na ushindi ndani ya Kristo Yesu…Anayafurahia Maisha na Uhai…maaana Yesu alikuja ili tuwe na UZIMA kisha tuwe nao tele (Yoh 10:10)…Mwl Anakusalimia! ###http://oneyearbibleimages.com/Image445.jpg

Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »