ILI KUWEKEZA VIZURI MAISHA YAKO (5)
5. Jiongezee Uwezo
• Utawekeza vizuri maisha yako kama utawekeza vizuri ndani yako. Ubora wa utu wako wa ndani utaamua ubora wa maisha yako.
• Wekeza maarifa na ufahamu ndani yako, vitafungua macho yako na kukufanya uone maisha kwa sura ya tofauti.
• Utaweza kutimiza mambo katika maisha kulingana na uwezo ulionao. Uwezo wa kiakili, uwezo wa kupambanua mambo, na uwezo wa kufanya mambo (ujuzi)
• Kila siku una nafasi ya kujiongeza na kujiboresha, Hakuna mwisho wa ukuaji, unaweza kuendelea kukua kwa kadiri unavyotaka.
• Utakuwa wa faida duniani kulingana na uwezo ulionao. Ongeza thamani yako kwa kujiongezea ujuzi, maarifa na uwezo.
KWA WAOAJI TU
“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni