“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza kabisa kuiangusha ndoa siku moja. Ni mwanandoa asiye na akili anayesubiri mmewe/mkewe aje kumwambia kosa lake kisha ndipo aombe msamaha ilhali moyoni mwake alikuwa anajua amekosea. Kukubali kosa mapema na kuomba msamaha wa dhati papo hapo ni siri ya ndoa nyingi zilizodumu. Kusameheana kwa moyo wote na kutotunza rekodi za makosa ya mwenzio ni silaha ya kipekee kwenye ndoa bora… Kumbuka Ndoa ya Kikristo inahusisha wanandoa wawili wenye mapungufu lakini wenye Mwokozi aliyekamilika, Yesu Kristo anayeweza kuifanya ndoa isizame nyakati za misukosuko na dhoruba
HEKIMA ZA NDOA 4
“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA