Petro alipomtazama Yesu [alipoweka jicho lake kwa Yesu] altembea juu ya MAJI [Juu ya kile ambacho kina uwezo wa kuuondoa uhai wake]…Lakini alipotoa jicho lake kwa Yesu na kuweka Jicho lake kwenye Mawimbi ya Maji yaliyokuwa yakipanda na kushuka miguuni mwake, AKAANZA KUZAMA.
Mara zote tunakuwa na uwezo wa kuzitiisha changamoto za maisha, majaribu, misukosuko ya maisha na magumu pale tunapokuwa tumeweka AKILI ZETU NA UFAHAMU WETU KWA YESU…Ila huwa tunaanza KUZAMA[kuzidiwa na kumezwa] pale tunapoamua kuzitegemea akili zetu, mbinu zetu, wanadamu wenzetu na kanuni za kibinadamu badala ya Mungu aliye yote katika yote…Ila habari njema ni kwamba, Pale unapogundua wapi ulipokosea na kumgeukia Mungu na kuutaka Msaada wake huwa anakuja mara moja na kukunusuru kama Yesu alivyokuja pale Petro alipopiga kelele, “BWANA NIOKOE, NAZAMA”
Hata kama unapitia ugumu kiasi gani, hata kama changamoto uliyonayo ni kubwa mno, hata kama madaktari wanasema huwezi kupona, hata kama hali yako haina majibu kwa yeyote na kokote, ninayo habari njema kwako, Yuko mmoja ambaye huwa ana kauli ya Mwisho juu ya hali zetu, Jina lake anaitwa MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, MSHAURI WA AJABU, MFALME WA AMANI…YESU KRISTO WA NAZARETH!
HEKIMA ZA NDOA 4
“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA