"Kristo yesu ndani yangu; tumaini la utukufu" (wakolosai 1:27)

Yesu ndani yangu

Yesu Kristo Yuko NDANI YANGU, Amejaa Kwenye ROHO YANGU Ili NIWE IBADA NA DHABIHU KWA MUNGU Peke Yake… Yesu Kristo Amejaa Kwenye NAFSI YANGU Ili Kila MAAMUZI Niyatendayo Yawe Sawa Na NENO LA MUNGU…Yuko Katika NIA YANGU Ili Niyafanye Na Kuyatenda MAPENZI YAKE TU Hata Kama Itanigharimu Heshima Mbele Ya Wanadamu, Na Hata Uhai Wa Mwili Wangu… Yesu Kristo Yuko Ndani Ya Kila Eneo Langu Linaloshughulika Na AKILI, UFAHAMU, MAARIFA, HEKIMA, UFUNUO Nakadhalika; SIWEZI KUWAZA KAMA MWANADAMU WA KAWAIDA, NAYAWAZA YALIYOKO JUU KRISTO ALIKO (Ndio Maana Sishangai Kutofautiana Na Watu Wanaowaza Na Kuona Kawaida Maana Mtu Wa Mwilini Hawezi Kuyapokea Mambo Ya Rohoni)… NINA AKILI AMBAZO SIWEZI KUZIELEZEA KWA KADRI ZILIVYO KUU NA ZA JUU “Kwa Maana Ninayo NIA YA KRISTO [THE MIND OF CHRIST]”… UBONGO WANGU WOTE WA MBELE, KATI NA NYUMA AMEJAA YESU NA UTUKUFU WAKE; SIWEZI KUPATA TATIZO LOLOTE KWENYE MFUMO WANGU WA FAHAMU AU KIUNGO CHANGU CHOCHOTE…Uzima Wa Kristo Unatiririka Katika Kila IMPULSE Na Utukufu Wake Unatembea Katika Damu Yangu, Kwenye Kila SELI, Kila TISHU, Kila KIUNGO, Kila MFUMO Ulio Katika Mwili Wangu Na Katika Kila Eneo La UHAI WANGU… Nimejaa Yesu, Nimejaa Nguvu Zake, Nimejaa Uzima Wake (Zoe), Nimejaa Nuru Yake, Nimejaa Asili Yake (His Nature), Nimejaa Kauli Zake, Nimejaa Mtazamo Wake (Insight), Nimejaa Hasira Yake Dhidi Ya Shetani Na Kazi Zake Za Kuchinja, Kuiba Na Kuharibu… Nimejaa Huruma Na Upendo Kwa Kila Roho Isiyomjua Kristo!
SI MIMI NINAYEISHI BALI KRISTO YESU NDANI YANGU, NA UHAI HUU NILIONAO KATIKA MWILI WANGU NINAO KATIKA IMANI YA MWANA PEKEE WA MUNGU ALIYEJITOA NA KUFA KWA AJILI YANGU!

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »