Kujeruhiwa kusikugeuze kuwa kiumbe tofauti na wewe! KONDOO

“Kujeruhiwa kusikugeuze kuwa kiumbe tofauti na wewe! KONDOO akijeruhiwa na mnyama mkali au nyoka machungani, huwa hageuki hayawani au nyoka pia, anabaki kuwa KONDOO ALIYEJERUHIWA… Kama mwana wa Mungu, utambulisho wako ni UPENDO, MSAMAHA, FADHILI, UTU WEMA, REHEMA kama Baba yako wa mbinguni alivyo, bila kujali UMEJERUHIWA KIASI GANI…”

Pastor Dickson Kabigumila

TUTAFAKARI MAANDIKO HAYA CHINI 👇

Isaya 53:7-9

[7]Alionewa, lakini alinyenyekea,

Wala hakufunua kinywa chake;

Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,

Na kama vile kondoo anyamazavyo

Mbele yao wakatao manyoya yake;

Naam, hakufunua kinywa chake.

[8]Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;

Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?

Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;

Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

[9]Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;

Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;

Ingawa hakutenda jeuri,

Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

Kuliishi NENO kunaweza kuwa kugumu kibinadamu, lakini huu ndio wito wetu, kuwa kama YEYE aliyetuita katika mwenendo wetu wote! UTAKATIFU SIO KUTOKUIBA, KUZINI TU, NI PAMOJA NA KUKUBALI AMRI ZAKE KUWA UTII WETU WA KILA SIKU…

Yohana 14:21,23

[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

[23]Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Ni maombi yangu kwa Bwana Yesu kwamba mimi (kwanza) halafu na wewe, tusipoteze utambulisho wetu kwa sababu ya KUJERUHIWA, KUUMIZWA AU KUTENDEWA VIBAYA…

SISI NI BARUA TUNASOMWA,

SISI NI CHUMVI YA DUNIA

SISI NI NURU YA ULIMWENGU

Mathayo 5:14-16

[14]Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

[15]Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

UKUU UNAANZA NA KUKUBALI MOYO UGEUZWE NA KWELI UNAZOZIJUA,

Pastor Dickson Cornel Kabigumila

ABC GLOBAL DUNIANI

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »