KUSUDI KUBWA LA KUUMBWA KWAKO NA KUOKOLEWA (MWISHO WA UKRISTO BROILER);

 

“KUSUDI KUBWA LA KUUMBWA KWAKO NA KUJA KWENYE MWILI, NI KUHAKIKISHA HUKOSI MBINGUNI, MENGINE YOTE HAYA MENGINE YA KUACHA ALAMA NYINGINE CHANYA, KUIGEUZA DUNIA, NA KULETA UTOFAUTI YANAJENGWA JUU YA HILO! USIWE NA AKILI MBOVU KAMA WALIZONAZO BAADHI YA VIJANA WA KIZAZI CHA SIKU ZA MWISHO, AMBAO WAO WAKO TAYARI KUFANYA CHOCHOTE NA YEYOTE ILIMRADI KINAWAPA PESA, UMAARUFU NA JINA, HATA KAMA KITAWAWEKA NJIA PANDA YA KUITETEA IMANI YAO KWA YESU, WAO WAKO TAYARI KU-COMPROMISE ILIMRADI TU WABAKI NA FURSA! MFANO MDOGO, KIJANA WA KISASA, ANAWEZA KUWA ” MC” WA MASHEREHE, ATACHEZA MIZIKI YOTE, ATAIMBA NA KUIMBISHA ANAOWASHEREHESHA KWA NYIMBO ZA BONGO FLEVA AU ZA KIMAREKANI, ATATUMIA LUGHA ZA NAMNA NAMNA, UONGO NA VINGINE ILI AONEKANE NI MTU ANAYEJUA KUFURAHISHA WATU… HII HAINA TOFAUTI NA KAMA DANIELI NA WENZIE WANGEAMUA KULA CHAKULA CHA MFALME, NA KUSEMA “HATA MUNGU ANAJUA TUKO BABELI, SUALA LA UHUSIANO WETU NA MUNGU SI KULA WALA KUNYWA, TUNAMPENDA MOYONI, DON’T JUDGE US BY THE OUTWARD THINGS”…. MWINGINE ANAWEZA KUULIZWA ” LIVE” KWENYE TV KAMA EAST AFRICA TV (CHANNEL 5) AU CLOUDS TV, YA KUWA “HIVI NI KWELI KWAMBA YESU PEKEE NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA? NA KAMA NI HIVYO JE WATU WENGINE WA IMANI TOFAUTI, WASIOKUBALI UBWANA WA YESU, HAWATAENDA MBINGUNI?” UTAMSIKIA ANAVYOJIKANYAGA “HILO SWALI MTAWAULIZA WACHUNGAJI” AU “NO COMMENT” YAANI HAWEZI KUTUMIA HIYO FURSA “KUISEMA KWELI” ANATAKA DUNIA IMPENDE! ANATAKA ULIMWENGU USIWE KINYUME CHAKE… NANI KATUDANGANYA YA KUWA KUOKOKA NI KUWAFURAHISHA WATU WOTE? NANI KATUDANGANYA TUKIOKOKA SERIOUS TUTAPENDWA NA DUNIA NA WAIPENDAO DUNIA? NANI KALIDANGANYA KANISA LA SIKU ZA MWISHO YA KUWA TUMEKUJA DUNIANI “KUWA MULTI MILLIONAIRES” NA KUWA NA PESA NYINGI KAMA BILL GATES NA WARREN BUFFETT? YESU ALISEMA “AMELETA UPANGA NA SI AMANI” ALISEMA “AMEKUJA KUFARAKANISHA MTU NA BABA YAKE” KUNA MAHALI UKISIMAMIA VIWANGO VYA INJILI, UTAONEKANA MNOKO, ANTI-SOCIAL, UNAJIINUA, UNAHUKUMU, UNAJIFANYA MTAKATIFU SANAAA… NA BILA KUWA TAYARI KWA SHUTUMA HIZO NA HATA KUFA IKIBIDI, BILA KUSHUSHA VIWANGO VYA INJILI NA UTAKATIFU, WEWE HUJAIJUA INJILI NA THAMANI YAKE… YESU HAKUTUOKOA ILI TUKUBALIANE NA ULIMWENGU, BALI ULIMWENGU UVUTWE KWAKE KWA KUYAANGALIA MAISHA, MISIMAMO NA VALUES ZETU KAMA WATU WALIOKOMBOLEWA… SASA WEWE JIFANYE UNATIMIZA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO, KWA KUJIPENDEKEZA KWA WATU, WAKUPENDE, WAKUKUBALI, WAKU-FOLLOW, NA MAUJINGA MENGINE, BADALA YA KUSEMA KWELI NA KUIISHI KWELI, HAKIKA UTAPATA HASARA YA NAFSI YAKO SIKU ILE YA MWISHO..
KUSUDI LETU KUBWA HAPA DUNIANI, NI KUISHI KWA AJILI YA KRISTO, KUKEMEA, KUONYA, KUSEMA KWELI HATA KAMA INAUMA ILIMRADI IMESUKUMWA NA UPENDO… HILI NDILO KUSUDI LA KUUMBWA KWETU, HILI NDILO KUSUDI LA KUOKOLEWA… LET EVERY BELIEVER AND CHRISTIAN WAKE UP TO THIS REALITY IN JESUS NAME…”
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
12/04/2019

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »