MAMBO MAKUBWA ( 3 ) YANAYOMPA NGUVU SHETANI

Kwa mujibu wa kitabu cha
#Wakolosai 2:14-15
[14]akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;[15]akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Yesu alimuondolea nguvu zote shetani, alizivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo ( useless, powerless, functionless – shetani hana kitu tena )
Ufunuo wa Yohana 1:18
[18]na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Funguo zinawakilisha mamlaka na nguvu na utawala ( kwahiyo shetani hana nguvu tena, hana utawala tena , wala hana mamlaka tena ) Yesu alimnyang’anya na kwa mujibu wa Waefeso 1:22
[22]akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
(Yesu alifanya haya yote kwa ajili ya kanisa )The number 3 - Numbers picha (22189072) - fanpop
SASA KWANINI MISSION (3) ZA SHETANI
( KUIBA , KUCHINJA NA KUHARIBU ) ZINAFANIKIWA JUU YA MAISHA YA WATU WALIOOKOKA
Shetani yuko bize anaharibu ndoa, Afya za watu, huduma, biashara n.k
Yafuatayo ni mambo YANAYOMPA Shetani nguvu za kufanya kazi

1. UJINGA

Watu wengi , iwe ni walokole , Watumishi wa Mungu, waombaji, wazamiaji, waimbaji #hawayajui kabisa kabisa mapenzi ya Mungu. Fahamu zao ni Kama za wanadamu wa kawaida japo wanadai wameokoka
Na mara nyingi utawaona wanajijumlisha kwenye mambo maovu utakuta wanasema ” sisi ni wanadamu, leo kwako kesho kwangu, tangulia tunakufuata ”
Naomba niongee kauli ngumu
” Mungu hakukuleta Duniani ili uje kusubiri siku ya kufa , uko hapa kuyafanya mapenzi ya Mungu ”
Zaburi 82:5-7
[5]#Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.
[6]Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
[7]Lakini #mtakufa kama #wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
Isaya 5:13-14
[13]Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa #kukosa kuwa na #maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.[14]Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.
Kuzimu imeongeza tamaa yake ; inakula , inaiba , inachinja, inaharibu kila siku kwasababu ya UJINGA
” Tafuta kuyajua mapenzi ya Mungu kila siku , fungua biblia yako isome ”

2. HOFU

Warumi 8:15
[15]Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
Hofu inaleta roho ya utumwa kwa watoto waliolipiwa gharama zote za uhuru ( watoto wa Mungu walipaswa kuwa ni watu wenye ujasiri unaowashangaza watu ).
Mithali 28:1
[1]Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. ( Yesu aliyeko ndani yako ni Mkuu Sana kuliko yule aliyeko duniani )
1 Yohana 4:4
[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
” Hofu ni utumwa , inaleta roho ya utumwa kwa watoto huru wa Mungu ”

3. VINYWA ( KINYWA )

Shida ya watu waliookoka, kinachowaponza watu wengi waliookoka, ni midomo yao, vinywa vyao
Wengi tunajua kuropoka ( profanity )
Kuropoka ni kuongea kwa ujasiri kitu ambacho hakipo kabisa kwenye Biblia
Na kwasababu hiyo magonjwa yamepata makazi, mauti imepata nguvu, uharibifu umejipatia sifa kwasababu kwa #midomo
Mtego mkubwa wa Maisha yako uko kwenye mdomo wako
#Mithali 6:2
[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
#Mithali 18:21
[21]Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
Haya ndio mambo yanayoharibu Maisha
Ya watu wengi waliookoka, na ndiyo yanayompa Shetani nguvu , ambaye alinyang’anywa nguvu zote.
God bless you.
Pastor Ibrahim Amasi
ABC KAHAMA
LivingWord|2020
Make a Living

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

KWA WAOAJI TU

“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »