MANTLE AND TRANSFER(VYA KIUNGU NA USAMBAAJI WAKE)

MANTLE AND TRANSFER
(VYA KIUNGU NA USAMBAAJI WAKE)

Pichani ni Apostle Johnson Suleman na mimi Bishop Dickson Cornel Kabigumila

JAMBO LA KWANZA
•Kuna muunganiko kati yetu kwa “dhabihu na kuwekewa mikono” na kwa MIMI KUSIKILIZA MAFUNDISHO YAKE KWA DHATI KWA MIAKA KADHAA SASA NA KUYAISHI

MFANANO WA NEEMA

 1. Wote wanaheshimu waliowatangulia (mababa wa imani na wakubwa waliotangulia kulipa gharama mbele yao kabla yao, na wenye matokeo kwenye kazi ya Ufalme kiasi cha kuwataja kwa majina na kukiri mguso na athari zao na si kujifanya WAMEFIKA HAPO BILA MCHANGO WA WENGINE)
 2. Wote wawili wanautambua mwili wa Kristo na wanautetea na kuulinda mwili wa Kristo hata kama hawataeleweka au wakipoteza watu kwa kusimama upande wa mwili wa Kristo!
 3. Wote wawili ni wasema kweli hata kama ni kwa maneno makali, mazito, magumu lakini iwapo ukweli huo utaponya taifa, kanisa au maelfu ya maisha, watausema kama ulivyo!
 4. Ni watu wenye “upako wa vita” (wana upanga) ambao ukilazimika kula hawauzuilii, watautoa kwenye ala na wanajua muda gani wautoe na muda gani wakae kimya!
 5. Watu wa bidii ya kazi, ukiwafuatilia watu hawa wawili wanafanya kazi kwa bidii sana kama vile hakuna tena maisha kesho!
 6. Ni watu wanaoamini kwenye utoaji mno na kubariki maisha ya wengine hata kwa kidogo cha mwisho walichonacho!
 7. Watu wa Neno kwelikweli, ukiwasikiliza wakiwa wanafundisha utahesabu maandiko mpaka uchoke! Ni walaji wa Neno sirini ili waje kulicheua hadharani
 8. Watu wanaoamini mno kwenye karama za Roho Mtakatifu, miujiza, na matendo makuu ya Mungu yasiyochunguzika! Wanamchukua Mungu na Neno lake kama alivyo na kuthubutu, na vitu vya ajabu hutokea! Wamekataa kufundisha na kuhubiri Neno bila nguvu nyingi na dalili za Roho!
 9. Watu wa maombi, watu dhaifu mbele za Mungu, wanaojua kuililia rehema na huruma za Mungu sirini, na majasiri na watata mbele za Shetani na watu!
 10. Watu wa kujenga watu kuwa bora kwenye maeneo yote, hawakubali mtu akae nao na awe wa kawaida kiroho, kiakili, kiuchumi, kihuduma, na kimguso! Watu wote wanaoambatana nao kwa dhati hugeuka kuwa watu wa ajabu!
  Wana neema ya KUJENGA WATU WAKUU
 11. Wote wawili wanaamini kwenye mafanikio ya kiuchumi na kimaisha kama zao la mafanikio ya rohoni hasa mahusiano sirini na Mungu kwenye Neno, maombi, mifungo, kukua kiakili kwa vitabu na kila jukwaa la maarifa linalopatikana! Kwa hawa watu, hawakubali mwamini awe masikini hata kwa bahati mbaya, wanaamini mamlaka ya Neno kugeuza maisha ya mtu na wanazo shuhuda za maisha yao na watu wao!
 12. Watu hawa wanaamini kwenye ubaba wa kiroho na kujiweka chini ya neema nyingine, wote wawili wako chini ya mababa na wote wawili wanalea wengi kama wana kwenye matawi na kama mtu mmoja mmoja!
  Kwao wanaamini kama hauna mtu anayeweza kukulea na kukuwajibisha hautakwenda mbali unakotakiwa kuwa kwa sababu hauna unayemhofu usipopiga hatua au kuwa na matokeo, na hauna wa kumuiga anayekuzidi!
 13. Wote wawili ni prophetic, wanasikia na kuona rohoni kwa Roho wa Mungu, wanaweza kuyajua mambo ya watu, mwili wa Kristo, nchi na dunia yao na wakilazimika kuyasema wazi yanatokea hata ukipinga au kukataa kwa sababu waliyosema hayaendani au kufanana na uhalisia!
 14. Watu hawa ni watu wanyenyekevu na wako simple mno, hawajui kuinua mabega, wanajua Mungu aliyewapa au kuwaleta mbele za watu, ANGEMPA AU KUMLETA MWINGINE YEYOTE MBELE ZA WATU MAHALI PAO!

NINAO ZAIDI YA 40 WENYE PICHA ZAO OFISINI KWANGU AMBAO WAMENIATHIRI, NITAKUWA NAWEKA MMOJA MMOJA HADI PICHA ZOTE OFISINI KWANGU ZIISHE…
Bishop Dickson Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
13.02.2024

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »