SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (SIKU 30 ZA MFUNGO).

Day 8, 12/01/2016.
“ROHO NYINGINE”
“Lakini mtumishi wangu Kalebu kwakuwa alikuwa na ROHO NYINGINE NDANI YAKE, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoiingia; na uzao wake wataimilki”(Hesabu 14:24)
Roho nyingine ni roho isiyo ya dunia hii.
Roho isiyo sawa na ya wanadamu wengine.
Ni roho ya ajabu toka kwa Mungu.
Inayomfanya mtu asiwe sawa na watu wengine.
Inampa kuwa jasiri na kuishi mbali na juu ya matatizo, hali, majaribu na hali ngumu zinazowatisha wanadamu wengine.
Anaweza kuona au kusikia hali au tukio lakini moyo wake hauyumbi,
Haogopi,
Hatetereki,
Yuko imara akimtumaini Mungu!
Zaburi 112:6-8
“Kwa maana HATAONDOSHWA KAMWE; Mwenye haki atakumbukwa milele. HATAOGOPA HABARI MBAYA; MOYO WAKE U IMARA UKIMTUMAINI BWANA. Moyo wake UMETHIBITIKA HATAOGOPA hata awaone watesi wameshindwa”(Zaburi 112:6-8).
Huyu ndo mtu mwenye “ROHO NYINGINE”
Haogopi chochote,
Hamuogopi yeyote,
Haogopi tukio lolote!
Kile ambacho wengine wanakiita “majitu” yeye anakiita “chakula”
Kile ambacho wengine wanakiita “amekufa ananuka sasa” yeye anakiita “Lazaro amelala, twende tukamuamshe”
Kile ambacho wengine wanakiita “Goliati, jitu na shujaa asiyeshindika” yeye anasema “nitapewa nini nikiliua hili?” Hawazi kuhusu CV ya jitu bali atakachopata akiliua!
Hatarajii kufa/ kuuliwa na jitu… Anajua kuna mshindi mmoja na huyo mshindi ni yeye!
Ni maombi yangu kwa Mungu utapokea “roho nyingine”
Roho ambayo inakufanya uishi kwa NENO bila kujali hali na mazingira mengine.
Hii ndiyo prayer point ya day 8.
Sasa mkaombe
Mkishapitia hayo maandiko.
Mkipata hiyo kitu mmetoka.
Namshukuru Mungu ninayo hiyo ROHO NYINGINE kitambo sasa, utukufu kwa Mungu pekee!
Natamani wote muwe nayo
Mpaka ifikie hatua Mungu mwenyewe akutaje na kusema mtumishi wangu ….. KWAKUWA ANA ROHO NYINGINE…
Another spirit
Isiyo ya dunia hii
Isiyojali na kuyatazama yanayoonekana bali kile alichosema Mungu tu
2Wakorintho 4:18
Niwaache mtafakari na kuomba.
HII NI PRAYER POINT YA JANA 12/01/2016.
Samahani kwa mnaofuatilia japokuwa hamko kwenye group maalum ya Mfungo.
Nilikuwa busy na maandalizi ya semina, nimeanza semina jana na watu wa TAG Matete kwa mchungaji Chesco Kinemo.
Mbarikiwe.

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »