Marafiki wa mwl tuendelee kupeana shuhuda ambazo Mungu wetu amekuwa akitufanyia nianze na mimi juzi nilienda Brela kwa ajili ya kuregister kampuni yangu. Ukweli sikuwa najua kitu isipokuwa ile tu google iliweza nielekeza namna so nimefika nikakuta watu wengi halafu wapo busy naamini walikuwa wanajua kila kitu na nikaingia chumba mojawapo nikapewa maelekezo wapi naweza pata form nikashuka mpaka stationary nikamkuta kaka mmoja nikaona hebu ngoja tu nimuulize aweze kunipa japo mwongozo yule kaka alinisaidia kwa moyo wote nakunipa moyo akaniambia umeamua utafika mbali nikachukua contact zake akaniambia twende ukalipe ili upate cheti cha usajili nikasita nikamwambia kuna mambo nayaweka vizuri nilipofika nyumbani sharp nikamalizia kesho yake asubuhi nae pia alikuwa hajapata cheti chake tukashirkiana kifupi jana niliweza maliza kusajiri kampuni yangu, sasa nimengia mitaani kwa ajili ya kusaka wateja. Mwl mpaka sasa najisikia vema na wengine wenye mawazo ya kuanzisha kampuni wasiogope. Mwl barikiwa sana naomba uendelee kupewa mafunuo ya ajabu ilikuwafikia wengi nawapenda wote amen
(Jane wa Dar es Salaam)
Huyu alichukua hatua kutokana na mfululizo wa Chakula cha Washindi: Upako wa Kufanya zaidi ya wengine!
HEKIMA ZA NDOA 5
“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza