VIJANA WENZANGU KWENYE HUDUMA

VIJANA WENZANGU KWENYE HUDUMA

NI NANI ALIYEKUTENGENEZA ILI UONGOZE/ UTAWALE/ UWE NA MATOKEO KWENYE ENEO LAKO?

ANDIKO NANGA

Kutoka 2:14

[14]Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? …

And he said, Who made thee a prince and a judge over us? …

Haya ni maswali aliyoulizwa MTUMISHI KIJANA mwenye shauku, kiu na njaa ya kuleta ukombozi na majibu kwa watu wake Israeli…

•Wito alikuwa nao

•Shauku nzuri alikuwa nayo

•Nia njema alikuwa nayo

•Moyo mzuri wa kuleta mageuzi alikuwa nao

•Nguvu alikuwa nayo ndiyo maana aliweza kumuua Mmisri

LAKINI

Alikutana na swali gumu na zito kadri alivyoendelea na harakati zake za HUDUMA YA UKOMBOZI NA KULETA MASULUHISHO kwa watu wa Mungu!

Hiki ndicho kinachowatokea WATUMISHI WENGI VIJANA! Wito wanao, shauku njema wanayo, kiu sahihi wanayo, na nguvu za Mungu wanazo, lakini cha ajabu MATOKEO HAYAONEKANI au hayafanani na jasho wanalovuja!

Swali hili aliloulizwa Musa ukisoma kwa tafsiri ya Kiingeleza inasema, “NI NANI ALIYEKUTENGENEZA NA KUKUWEKA UWE MTAWALA NA MKUU…?”

UTAGUNDUA HAYA

1. Kuwa na wito au jambo zuri kwa ajili ya Ufalme haitoshi

2. Kuwa na nguvu (upako) haitoshi

3. Kuwa na nia njema ya kugusa na kuathiri dunia yako kwa viwango vikubwa haitoshi

4. Unaweza kuanza kabisa huduma, ukapata matokeo kwa sehemu kama Musa alivyoua askari mmoja wa Kimisri, lakini mbele UTAKUTANA NA UPINZANI utakaokuuliza UMETENGENEZWA NA NANI? NANI AMEKUWEKA WAKFU/ AMEKUSIMIKA/ AMEKUTAMBULISHA ROHONI kwenye unachofanya…

5. Utagundua kuna FALME, MAMLAKA, WAKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO WABAYA kwenye ulimwengu wa roho ambao wanakagua KAMA UMETENGENEZWA/ UMEANDALIWA/ UMEWEKWA HAPO NA MIKONO HALALI YA KIMAMLAKA ROHONI

6. Hizi mamlaka za kiroho zinazouliza umefikaje hapo, zitakuuliza maswali kwenye tabia yako! Zitakuuliza maswali kwenye uchumi wako na wa huduma! Zitakuuliza maswali kwenye ukuaji wa huduma au kanisa la mahali unalochunga! Ukikosa UTAMBULISHO WA NANI ALIKUTENGENEZA/ ALIKUWEKA NA KUKUTHIBITISHA kwenye unachofanya, utapoteza huduma kama Musa alivyolazimika kukimbia Misri… Utakimbia ndoa yako, utakimbizwa na umasikini, shutuma, tuhuma na majanga mengine yanayoua huduma!

7. Tafuta mikono iliyo hodari ikutengeneze na ikufinyange, ikufanye kuwa chombo cha thamani kimfaacho Mungu kwa kila kazi njema! Wapo watu wa mbinguni kati ya wanadamu wenye neema ya KUTENGENEZA NA KUWAFANYA WATU KUWA WAKUU NA WAAMUZI kwenye huduma na maeneo mbalimbali ya ushawishi…

Ni vyombo vilivyotengenezwa pekee ndivyo humfaa BWANA kwa kila kazi njema! Usitake kujifanya, kaa chini ya baba akufanye! Kaa chini ya jemedari akufundishe vita na akurushe kama mshale ukaathiri dunia yako!

2 Timotheo 2:20-21

[20]Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.

But in a great house there are not only vessels of gold and of silver, but also of wood and of earth; and some to honour, and some to dishonour.

[21]Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.

If a man therefore purge himself from these, he shall be a vessel unto honour, sanctified, and meet for the master’s use, and prepared unto every good work.

HATARI YA HUDUMA UJANANI

1. Unahisi kukaa chini kuandaliwa ni kama kucheleweshwa kuingia shambani kuchapa kazi! Hivyo mchakato wa kukaa chini kujifunza au kudumu kuwa mwanafunzi chini ya mtu unauona kama kumilkiwa, kutawaliwa, kufanywa mtumwa, hivyo unakwenda kabla hujawa tayari, ukiwa huna cheti cha kuhitimu, na ukiulizwa swali, “NI NANI ALIYEKUTENGENEZA AU ALIYEKUWEKA UWE MKUU NA MTAWALA KWENYE HUDUMA…” unakosa majibu na unaishia kufeli au kuwa na huduma inayochechemea isiyo na matunda!

2. Vijana wengi wanahisi wanajua vingi tayari kwa vile tu wanaweza kupata vitabu, video au kuwafuatilia watumishi maarufu wa mitandaoni na mataifa mbalimbali, wasichojua ni kwamba HAKUNA KITUO CHA TUTION kinachotoa cheti cha kuhitimu elimu ngazi yoyote!

3. Vijana wengi wanafikiri huduma ni kuomba masaa mengi au kufunga kavu siku kadhaa pekee! Hawajui kwamba hayo pekee sio tishio kwa Ibilisi na Ufalme wake, ndio maana Shetani alikuja kumjaribu Bwana Yesu aliyefunga 40 kavu kabisa…

Wewe jidanganye ufikiri sikio kwa vile linasikia basi linaweza kuendelea kuwa bora bila kujishikiza kwa kichwa, halafu siku likikatwa au kutengwa na kichwa ndipo litajua ulazima na umuhimu wa kushikanishwa na kichwa ili kuendelea kusikia na kuwa hai! Omba sana, funga mno, lakini HAKIKISHA UNA KICHWA ULICHOSHIKANA NACHO KINACHOKUFANYA UENDELEE KUWA HAI!

Nisikuchoshe kijana mimi na akili zangu za kizee,

Naitwa Bishop Dickson Cornel Kabigumila,

Mtu mwenye majibu ya kizazi changu,

ABC GLOBAL DUNIANI,

06.07.2023

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »