MAENEO MATANO YA KUJIJENGA KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 25
LAKINI UNAWEZA KUYAJENGA HATA KAMA UNA MIAKA 50 TAYARI
Bishop Dickson Cornel Kabigumila
1. ENEO LA KUSUDI NA WITO
YEREMIA 1:5, ISAYA 49:1-6
•Hakikisha umejua kwa kina nini ambacho umeumbwa kukifanya duniani na kisha anza kukifanya tokea hapo hapo ulipo na unapoweza! Itakusaidia kujikosoa, kujirekebisha, kujiboresha nakadhalika! Hadi unafikia miaka 35 hauna bahati nasibu kwenye maisha! UNALO JAMBO LA KUFANYA NA MAISHA YAKO DUNIANI, JITAFUTE.
2. UKISHAGUNDUA KUSUDI ENEO LA PILI NI WATU SAHIHI WA KUAMBATANA NAO KWENYE HILO JAMBO/ WITO WAKO!
•Wawe wacha Mungu kwelikweli, wanaotii na kuheshimu kanuni za Mungu na amri zake!
•Wawe na maono makubwa wanayoyafukuzia au wanafanya mambo makubwa tayari ili wakupe hamasa na changamoto ya kutokuwa mtu wa kawaida!
•Wawe watu wanaoamini kwenye mambo makubwa na wanataka kuacha alama kwenye kizazi chao na vingi vijavyo! Mtu yeyote anayekubaliana na ukawaida au uwastani abakie kuwa mlaji/ mnufaika wa ulichobeba na si rafiki yako!
3. HAKIKISHA UMESOMA VITABU KADHAA (WALAU 10) KUHUSU NDOA NA FAMILIA NA KUJIKOSOA MAENEO YOTE AMBAYO HAUKO VIZURI ILI UKIINGIA HUKO USIJE UKAONGEZA IDADI YA TALAKA NA WATOTO WA MITAANI!
•Ndoa si bahati nasibu wala si kamari, ina kanuni za kiungu na za kawaida za kuishikilia hadi mwisho! No luck, no gamble, it is a principled institution.
•Usidanganywe na wanaosema ndoa haina mtaalam wala fundi, hao ni walioingia choo cha jinsia nyingine, they are too late to make some changes! Ndoa inaanzia kwenye aina ya mtu unayemchagua kuwa mke/ mume, haianzii siku mkitangazwa madhabahuni na kupewa vyeti
•Malezi ya watoto sio bahati hata kidogo! Sio muujiza hata kidogo! Sio neema tu hata kidogo! ANAKUA SAWA NA ANAVYOLELEWA- Mithali 22:6.
•Kila mtoto anayemfurahisha babaye, ana mama bora mno anayesimamia viwango! Kila mtoto aliye mzigo kwa mama, ana baba mjinga aliyeoa mwanamke kwa uzuri, umri, elimu, familia anayotoka, jina na kadhalika BILA KUWAZA MALEZI YA WATOTO WATAKAOWAZAA YATAKUWA KWENYE MIKONO YA MTU WA NAMNA GANI!
Mithali 10:1, Mithali 28:7
Taasisi ya ndoa na familia ndiyo inaamua jamii itakuwa ya namna gani! Kila ukikosea hapa unaongeza matatizo kwenye jamii!
Taasisi ya ndoa na familia ndiyo inaamua kanisa litakuwa na heshima au aibu kiasi gani mbele za dunia kila tukifeli! Ukikosea, umeleta aibu na matusi kwa kanisa!
Taasisi ya ndoa na familia ndiyo inaamua aina ya viongozi wa serikali na mifumo ya nchi, ukikosea hapa, umeliletea taifa balaa! Umeliingiza taifa matatizoni kwa ujinga wako!
4. UWE UMESOMA VITABU, UMEANGALIA VIDEO MAMIA, UNAFUATILIA WALIOFANIKIWA, MATAJIRI, NA WENYE MATOKEO NA KUPATA MAARIFA YA KUTOSHA KUHUSU PESA, MALI, UTAJIRI NA MAFANIKIO KWA UJUMLA!
Mtu hawezi kuwa zaidi ya alichonacho kichwani! Hata angeombewa, akatiwa mafuta, akatabiriwa, akawekewa mikono, KAMA KICHWA HAKINA TAARIFA SAHIHI, UPAKO WOTE HUU UNAPOTEA BURE!
Kwenye eneo la fedha hakuna muujiza zaidi ya kujichimbia na kujua kila unaloweza kuhusu fedha inavyofanya kazi! Nje ya hapo, PESA NA WEWE HAMTAISHI ENEO MOJA! PESA INAWAHESHIMU WANAOJUA KUIFUGA.
5. HAKIKISHA UMEKULA VITABU VINGI, VIDEO NYINGI SANA NA KILA MATERIAL UTAKAYOPATA KUHUSU MASUALA YA UONGOZI.
•Kila kitu kinafeli au kufanikiwa kutokana na uimara au ubovu wa uongozi.
•Kila nchi inakuwa masikini au tajiri kutokana na uimara au ubovu wa uwezo wa kiuongozi wa mwananchi mmoja mmoja.
•Tatizo la Afrika yetu si umasikini ni viongozi wabovu.
•Tatizo la talaka nyingi leo, ni mke na mume wasio na quality za uongozi wa mtu binafsi!
• Mtu aliyejijenga vizuri kwenye eneo hili la uongozi, ni suala la muda atakuwa na MAISHA YA UTUKUFU DUNIANI!
Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL