Biblia chanzo cha maarifa

Kuna zile MESEJI ZA MIZAHA kwenye MITANDAO zinazosema, “Shetani akikuona unashika BIBLIA anaumwa na kichwa, akikuona unafungua na kuanza kusoma ANACHANGANYIKIWA NA KUZIMIA. Jitahidi kila siku usome Biblia tena kwa sauti ili asikiapo sauti yako huenda AKAPATA STROKE NA KUANGUKA KABISA KATIKA MAISHA YAKO” Hii meseji ina ukweli wa Jambo moja la muhimu, SHETANI HATAKURUHUSU USOME BIBLIA NA KUPATA MAA

RIFA/ WAZO LA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO… Na kama akishindwa kukuzuia KUSOMA NENO atajitahidi USOME KAMA GAZETI NA USIPATE UFUNUO/ MAARIFA YATAKAYO BADILI MAISHA YAKO (Ni lazima Uombe Uwepo na Msaada wa Mungu na uzibe mianya ya adui kujihudhurisha na pia hakikisha umekaa mahali pa utulivu na pasipo mwingiliano)… Ndio maana IDADI KUBWA YA WAKRISTO (zaidi ya 80%)HAWASOMI BIBLIA hata kwa walau dakika 15 kati ya masaa 24 ya siku… Na waliobaki, 15% wanasoma BIBLIA kwa mazoea, wanasoma ule MUDA WAMECHOKA AKILI NA MWILI, Hasa ule muda wanataka KULALA, tena kwa Kuchukua Biblia na kufunua vuu, popote patakapofunuka wanasoma…Kwa style hii Mimi na wewe tutakuwa na TOFAUTI KUBWA YA UFUNUO kama FARASI NA KOBE na kila siku utaishia kunishangaa kwa UFUNUO usioisha… Wale 5% waliobaki ndo MASHUJAA wanaosoma Biblia Muda wakiwa vema kiakili na kimwili, tena wakiwa katika hali ya Maombi na wakitamani na kutaraji kupata Ufunuo/ Maarifa yatakayo badili maisha yao na ya wengine… Na wakipata MAARIFA/ UFUNUO wanayatendea kazi na WANASTAWI NA KUCHANUA… Kazi ni kwako wewe msomaji!
Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin
Share on whatsapp
Share on telegram

KWA WAOAJI TU

“Ni Hekima Ya Mungu Kumpa Mwanadamu MALIGHAFI [Raw Materials] Ili Yeye [Mwanadamu] Afanye Sehemu Yake KUZIFANYA KUWA BIDHAA HALISI [Products]… Mungu Anakupa MTI Na Ni

Read More »

usioe kwa sababu

“Usioe kwa sababu unawaka tamaa, hivyo unaoa ili usiendelee kutenda dhambi nje. Dawa ya tamaa si kuoa. Dawa ya tamaa ni kukubali kuwa tamaa inakutesa,

Read More »