“Dhambi ina tabia mbaya sana! Inaweza kukuruhusu kuendelea kuimba, kutoa sadaka, kuhudhuria kanisani, kujihesabia haki kwa kuwacheka na kuwasema wale ambao dhambi zao zimefichuliwa au zimeonekana wazi, huku wewe unaendelea kuteketea ndani kwa ndani, kimya kimya unazidi kudidimia kwenye shimo la uharibifu!! Kuna mambo ambayo dhambi haiwezi kukuruhusu kuyafanya, nayo ni kuwa na maombi endelevu (maana ukiwa na maombi kila siku bila kukoma, itakosa pa kukaa)… Dhambi pia haiwezi kukuruhusu uwe na mifungo endelevu ya kila wiki maana pepo watakosa chakula na watakonda na kukuachia… Dhambi haiwezi kukuruhusu kusoma neno la mungu au kufuatilia mafundisho kwa utulivu na usikivu maana hakuna nguvu ya dhambi itakaa ndani ya moyo wa mtu aliyeliruhusu neno kumgeuza… Haya matatu niliyotaja mwishoni, ni dawa ya dhambi yoyote unayohangaika nayo… Ukiyafanyia kazi, ni suala la muda tu, utakuwa huru jumla toka kamba za dhambi yoyote ile…”
HEKIMA ZA NDOA 3
“Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko