“Hakuna UKUU kwa ajili ya maonyesho au kwa ajili ya sifa binafsi! Mungu anapoamua kumfanya mtu kuwa MTU MKUU ni kwa sababu KUNA KILIO CHA WATU WAKE kinapaswa kutatuliwa kupitia HIYO NAFASI utakayopewa na Mungu kwenye hicho unachofanya! Mungu anapoamua KUMFANYA MTU AWE MKUU ni ili AJIBU MASWALI YA DUNIA YAKE NA KILIO CHA WATU WAKE! Usipojua hili utautaka ukuu kwa ajili ya umaarufu, jina, na mambo yako binafsi, kitu ambacho si msingi wa UKUU! Mungu HUINUA WATU ILI WAKOMESHE VILIO VYA WATU WENGINE. Mungu huibua watu kutoka kusikojulikana au kusikotarajiwa na kuwapa JUKWAA ili tu WAFUTE MACHOZI YA KIZAZI CHAO AU DUNIA YAO… Usipokuwa na mtazamo huu, MUNGU HATAKUINUA, HATAKUPA NAFASI KUBWA, HATAKUTAMBULISHA KWA WENGI, NA HATAKUZA JINA LAKO”
ANDIKO
1 Samweli 9
16 Kesho, wakati kama huu, NITAKULETEA MTU KUTOKA NCHI YA BENYAMINI, nawe MTIE MAFUTA ILI AWE MKUU juu ya watu wangu Israeli, NAYE ATAWAOKOA WATU WANGU NA MIKONO YA WAFILISTI; maana NIMEWAANGALIA WATU WANGU, KWA SABABU KILIO CHAO KIMENIFIKIA.
- Mungu anaweza kuleta mtu kutoka kokote (kabila lolote likiwemo lenu, wilaya au mkoa wowote ukiwemo wenu, taifa lolote ikiwemo Tanzania) kama alivyoleta mtu kutoka kabila la Benjamini ambalo kikawaida kiti cha Ufalme si chao ni Yuda!
- Unahitaji MAFUTA kuweza kuwa kile mbingu zinataka uwe, kipawa hakitoshi, usongo na kiu havitoshi
- Kila atakayepewa kitu (ukuu) na Mungu ni ili atatue jambo fulani, kwa Sauli ilikuwa ni ili awasaidie watu wake Israeli dhidi ya Wafilisti!
Kila huduma, kila kipawa, kila kipaji ulichonacho, ni kwa ajili ya wengine sio kwa ajili yako. - Mungu akiwaangalia watu wake na machozi yao, huwa anatuma mtu na kumpa kitu kitakachotatua jambo husika, kwenye mchakato huo wa kuyatatua mambo ya wengine, ndipo UKUU ULIPO
Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
15.02.2024