Luka 1:5 inasema kitu kuhusu Kuhani Zekaria, na Mke wake Elisabeth…na kuna mambo kadhaa ya kujifunza;
1.Zekaria alikuwa kuhani, lakini Elizabeth alikuwa wa Kabila la Lawi
Hii inaonesha wazi ya kuwa, hawa watu [Zekaria na Elizabeth] walikuwa watu wanaoishi kwenye SAME PURPOSE…Zekaria alikuwa Kuhani, aliyetumika madhabahuni, na ili huduma yake na wito wake na kusudi la Mungu kwake litimie, alihakikisha anampata mtu ALIYEKO KWENYE SAME DIRECTION na yeye, ndio maana Elizabeth alitokea kabila ya Lawi; Kabila ambalo Mungu alilitenga lote liwe linatoa makuhani na watu wa madhabahuni…ili iwe rahisi kwa Zekaria kutumika vema kwenye KUSUDI LA MUNGU ilibidi awe na mtu mwenye maono kama yake!
[NINYI WAKAKA NA WADADA MNAOPENDA KUANGALIA PHYSICAL MATERIALS, BADALA YA SPIRITUAL CONTENTS MTAKUJA KULIA KARIBUNI]…Mke ni Msaidizi wako katika kulitimiza kusudi la Mungu…Ataitwaje mke, wakati wewe unakwenda kulia na yeye anakwenda kushoto? Malengo na mipango yenu iko tofauti…mtafika? ni sawa na kujaribu kwenda Mbagala ukiwa na rafiki anayekwenda posta, HAUTAFIKA!
kumbuka: “WAWILI HAWAWEZI KWENDA NJIA MOJA WASIPOPATANA[kama hawana same destination]”
2.Wote wawili [Zekaria na Elizabeth] walikuwa WATU WA HAKI, WALIOSHIKA MAAGIZO YA MUNGU, NA KWENDA MBELE ZAKE SIKU ZOTE BILA LAWAMA
WALIKUWA WATU WA HAKI;
Usije kufanya kosa kubwa la kuwa na mahusiano na mpango wa kuolewa na mtu ambaye SI MPENDA HAKI NA ANAYESIMAMIA HAKI KATIKA MAMBO YOTE.
Biblia inasema, “Kwakuwa UMEIPENDA HAKI NA UMECHUKIA UOVU, MUNGU AMEKUPAKA MAFUTA(AMEACHIA UPAKO JUU YAKO) YA SHANGWE KULIKO WENZAKO WOTE”
Kama una mahusiano na mtu ambaye hata diploma, degree, masters au phd yake ameipata kwa njia ya WIZI WIZI…KWA KUDESA, Huyo hawezi kuwa mwaminifu kwenye maisha pia…”ALIYE MWAMINIFU KATIKA MADOGO, MUNGU HUMPA NEEMA KATIKA MAKUBWA PIA”
Mkaka/Mdada mwenyewe anataka MFANYE NA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA…WAKATI NI LA NDOA…Huyu HAMWOGOPI HATA MUNGU ANAYEZUIA UASHERATI NA UZINZI…KAMA HAMWOGOIP MUNGU, ATAKUOGOPAJE WEWE? NDOA ZINATUNZWA NA UAMINIFU NA UPENDO…KAMA HANA UPENDO WA DHATI KWA MUNGU, KIASI CHA KUVUNJA TARATIBU ZA MUNGU, ATASHINDWAJE KUVUNJA TARATIBU ZA NDOA ALIYOIASISI MUNGU? TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA!
WALISHIKA MAAGIZO YA MUNGU
Hakikisha huyo dream boy/girl wako naye ameiva kiasi kwamba kwake MAAGIZO YA MUNGU/ NENO LA MUNGU ndiyo yanayotawala mfumo wake wa maisha…kama ana-COMPROMISE kilicho kwenye Neno la Mungu…Hatashindwa ku-COMPROMISE hata kwenye ahadi zenu za ndoa…BE CAREFUL [MWENYE MASIKIO NA AYASIKIE MANENO HAYA AMBAYO ROHO ALIAMBIA KANISA]
WALIKWENDA MBELE ZA MUNGU PASIPO LAWAMA
Kama uko kwenye mahusiano na mtu wa LAWAMA…Umenaswa pabaya…hasa yule ambaye anapenda kuwalaumu watu wote isipokuwa yeye mwenyewe na mapungufu yake!
Mtu wa lawama HAFAI…ATAKUTESA HUKO KWENYE NDOA KAMA UTAAMUA KWENDA NAYE HUKO!
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
AUGUST 29, 2012.
KWA WAOAJI TU
“Ukimuona Mwanamke Ambaye AMEKAMILIKA TAYARI [Product] Ujue Kuna Mwanaume Mwingine Ambaye AMEINGIA GHARAMA Kumfanya AHAME TOKA KWENYE MALIGHAFI [Raw Material] Mpaka Kuwa Vile Alivyo… UKIONA